Uliwezaje kufungia vyeti kabatini kisha ukajiajiri?

Evvy jr

Senior Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
148
Reaction score
189
Habari yenu wakuu, ni matumaini yangu mu wazima wa afya.
Kumekua na misemo na dhana kwamba wasomi wengi hawapendi au wanashindwa kujiajiri, na hutegemea kuajiriwa tu au kazi za mteremko. Mliojiajiri hebu tuambieni mliwezaje kufungia hayo magamba ndani kisha mkaingia mtaani .
 
Nilikuwa nikichukia sana nilipokuwa namuona baba yangu akiamka asubuhi na kurudi jion akisema anakwenda kazini mara nyingine tusimuone wiki au mwezi mzima nyumbani akiwa safarini.
 
Nilikuwa nikichukia sana nilipokuwa namuona baba yangu akiamka asubuhi na kurudi jion akisema anakwenda kazini mara nyingine tusimuone wiki au mwezi mzima nyumbani akiwa safarini.
Ni utumwa sana unashindwa kukaa karibu na familia kisa kazi za watu, ni bora uwe mbali na familia kwa kitu ulichojiajiri mwenyewe kuliko kaz ya kuajiria
 
Shida ikikomaa Aibu na aupga huondoka. Kinacho sababisha watu washindwe kujiajiri ni Uoga mkuu na Aibu kuu watu waliyo nayo. Aibu ya watanionaje.

Kujiajiri ni kugumu sana na inahitajika uvumilivu wa kiwango cha mwisho kabisa.

Bila uvumilivu bora tu mtu akatafute kaza za kufanya.

Watu wengi hujiajiri huku wanatuma application za kazi maana yake hapo unakuta uvumilivu usha washinda
 
Kwangu mm vitu ni vingi mnooo vilivyopelekea kuvitunza vyeti vyangu kwenye sanduku LA chuma,..lakini hivi ndivyo nilianza navyo;

•Uthubutu
•Kuvua aibu/kutojali nitaonekanaje
•Kujiamini kuwa nitaweza
•Hamu ya kutimiza malengo..n.k.
 
Wakuu mje kunitia moyo. Mimi nimemaliza form six mwaka huu. Ila naona ndoto yangu ya ujasiriamali ni kubwa kuliko kupoteza miaka 3 chuo na kozi zisizona uhalisia.
Nakushauri tafuta course inakayokujengea knowledge ya biashara zaid.Miaka 3 sio mingi wakati unazidi kujenga idea's zaidi ndipo ujiajiri.Utajifunza kutengeneza business plan,Jinsi ya kumanage kodi,utunzaji fedha kitaalam nk. Umesoma combination gn advance
 
Mbona kitu simple tu!
Mfano mimi nina degree ya public relation
Lakini kutokana na kukosa ajira nikaamua kuwa muuza majeneza na vumbi la Kongo
 
Kujiajiri kunatokana na kuona kitu ambacho wengine hawakioni. Ni kujikana na kuona kila changamoto ni hatua kufikia mafanikio. Ktk nchi ya Tanzania the big Challenge is taxation. Wakati ukiwaza ufanye nini TRA wao wanawazakukukamua kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…