Uliwezaje kufungia vyeti kabatini kisha ukajiajiri?

Hii nimeielewa Mkuu [emoji109]
 
Wakuu mje kunitia moyo. Mimi nimemaliza form six mwaka huu. Ila naona ndoto yangu ya ujasiriamali ni kubwa kuliko kupoteza miaka 3 chuo na kozi zisizona uhalisia.
shule nenda miaka mitatu sio mingi itakusaidia kutengeneza marafiki ambao wengine wanaweza kuwa fursa kwako na pia kiwango chako cha uelewa kitakuwa kikubwa.
 
baada ya kazi kwisha ghafla niliomba kazi sehemu mbalimbali bila mafanikio na mwisho nilipolipwa nssf yangu nikalipia kodi ya ofisi nikachukua computer nyumbani sehemu nyingine nikalipa kodi ya nyumba shughuli ikaanza kwa kuanza biashara ya ushauri wa wajasiriamali wadogo na benki jamii ikiwa ni pamoja na kuwashauri kuhusu mikopo.
ilipita miaka minne sijapata mteja wa maana lakini uongo nikitumia printer mbili moja ilikuwa scanner iliyogeuka kuwa photocopy machine kwa kuscan na kuprint kwenye printer nyingine maisha yalienda.
ikatokea kazi moja ya NGO moja nikajazana watu zaidi ya 10 na kwa bahati nikashinda ndipo nilipoanza kusogea.
hivyo inahitaji uvumilivu na kuamini unachotegemea kufanya.
bado kunachangamoto sijasimama vizuri lakini maisha yanakwenda ndugu yangu wala sifikirii kuomba kazi tena labda offer iwe ya maana na lazima anayeniajiri aniruhusu kufanya shughuli zangu zinapotokea vinginevyo akwende na kazi yake.
 
Mbona kitu simple tu!
Mfano mimi nina degree ya public relation
Lakini kutokana na kukosa ajira nikaamua kuwa muuza majeneza na vumbi la Kongo
biashara ya mazishi inalipa ila jamii haielewi kirahisi lazima watakwita mjenzi huru! huko nyuma nilishawahi kumshawishi mtu atengeneze business plan yake na nikamweleza jinsi inavyolipa. watu wanajaribu kufanya ila bado hawajafikia kile ambacho mimi naamini kinalipa kwa kiasi kikubwa.
nashawishika kufanya ila do! familia haitanielewa na kabila langu ndo utata kabisa!
 
Niliweza kwa kua na uthubutu na kingine sikupenda kujiajiri venye kua mtumwa wa mwingine hiyo kitu niliikataa

Na kingine bana ukiwa napenda pesa na kufikia malengo ya kua na maisha mazuri jamani..niliona kama ajira itanichelewesha tu..
 
Naomba shavu la u-spika
 
Nilikuwa nikichukia sana nilipokuwa namuona baba yangu akiamka asubuhi na kurudi jion akisema anakwenda kazini mara nyingine tusimuone wiki au mwezi mzima nyumbani akiwa safarini.
Kuna siku mzee alikuwa busy na kazi sometimes tunamsaidia home sasa my young bro akamuuliza'hivi hizi kazi zitaisha lini?'
 
Unamawazo yenye misingi ya woga usio na maana na wewe ni zao la shule cheti sio shule elimu,nimemaliza elimu ya juu miaka mitano iliopita na mpaka leo sijafuata cheti changu chuoni,kwa mshahara upi hapa tz?
Huufahamu ujasiriamali wewe endelea kusubiri mshahara wako mwisho wa mwezi.
 
Kujiajiri yataka ujasiri mwingi sana hasa kwa wenye elimu ya vyeti hupata shida sana kuingia kwenye kujiajiri no hadi kuja kuzoea

Adui mkubwa wa kuanza kujiajiri ni AIBU na UOGA uliopitiliza ukivishinda hivi lazima utusue tu na baada ya kujiajiri kinachotakiwa ukishinde ni KUKATA TAMAA kwani kwenye kujiajiri kuna changamoto kubwa sanaaa, ukishinda hivyo hakika umaskini utausikia tu.
 
point
 
100%!!
 
Kama anapiga kilimo cha umwagiliaji haina shida
 
very true,,,,,, nimekuelewa sana
 
Hongera kwa uthubutu na kudumu. Uko vizuri, uwa kabisa na usikubali roho ya kuajiliwa ikuingie tena.
Halafu kufikiri muajiri anaweza akakupa muda , hiyo ni impossible.

Hilo la kumiliki na kukomboa muda wako wa kuutumia unavyotaka, ndio bonasi mojawapo kubwa ya kuwa mtu aliyesimama kwenye shughuli zake.
 
Hongera sana Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…