Uliwezaje kutongoza kwa mara ya kwanza?

Uliwezaje kutongoza kwa mara ya kwanza?

KJ07

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2021
Posts
2,370
Reaction score
5,381
Habari za wakati huu

Nimeona nilete mada muhimu kama hii mezani kwani kutongoza ni point muhimu sana iwe kwa mwanaume na hata kwa mwanamke japo ni nadra kusikia mwanamke katongoza na wanaume wengi tunawachukulia wanawake wanaotutongoza kama ni wameshindikana ila ukweli hauko hivo kwani mapenzi hayana mwenywe kila mtu anaweza kamatika.
kwahiyo hebu jarib kushea na wana jukwaa siku ya kwanza unatongoza ilikuwaje.
je uliona aibu au ulikuwa jasiri?
karibuni kwa mawazo.
 
Habari za wakati huu

Nimeona nilete mada muhimu kama hii mezani kwani kutongoza ni point muhimu sana iwe kwa mwanaume na hata kwa mwanamke japo ni nadra kusikia mwanamke katongoza

Naomba kuwasilisha
Kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe miaka zaidi ya 30 iliyopita nimetongoza wiki iliyopita. Siku zote nilikuwa natongozwa mimi. Nilivaa ujasiri maana aliuteka moyo wangu ghafla. Kazi kazi.
 
Kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe miaka zaidi ya 30 iliyopita nimetongoza wiki iliyopita. Siku zote nilikuwa natongozwa mimi. Nilivaa ujasiri maana aliuteka moyo wangu ghafla. Kazi kazi.
duh umetixha mkuu kama ni kweli
 
Nilichambwa mbele ya rafiki zangu niliabika mimi,niliaibika sana!.
Sikia tu mtoto wakike amesimama mbele yako,mguu mmoja mbele, kiunoni kajivika kanga kana kwamba anataka kukata mauno! Halafu ananesanesa halooo!! Lile neno la "UNIKOME" nilikuwa nalisikia kuanzia kiambishi awali cha Kati na kiambishi tamati!,mzizi wa neno,na ndipo nilijua hilo neno ni sentensi ya kujitegemea na iliyijitosheleza!.
Nilikuwa mnyonge kama nimemwagiwa maji!.. kitoto cha watu kimefura,ule mtaa niliacha kwenda kwa wiki kadhaa.😂
 
Nilichambwa mbele ya rafiki zangu niliabika mimi,niliaibika sana!.
Sikia tu mtoto wakike amesimama mbele yako,mguu mmoja mbele, kiunoni kajivika kanga kana kwamba anataka kukata mauno! Halafu ananesanesa halooo!! Lile neno la "UNIKOME" nilikuwa nalisikia kuanzia kiambishi awali cha Kati na kiambishi tamati!,mzizi wa neno,na ndipo nilijua hilo neno ni sentensi ya kujitegemea na iliyijitosheleza!.
Nilikuwa mnyonge kama nimemwagiwa maji!.. kitoto cha watu kimefura,ule mtaa niliacha kwenda kwa wiki kadhaa.[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] bange
 
Nilijipa ujasiri kumtongoza demu flan hiv ......nikaambulia matusi........

Kufupisha story ....nilianza kumkwepa ....ila now.....anajileta mwenyew
 
Aiseee sisi madomo zege tunazungukaga saaana.....
Unamuonesha msichana kuwa unampenda yeye ndo aaamue....

Siku moja ingawa haikuwa ya kwanza kwa kweli hii miguu siyo ya kuiamini saaana...inaweza kukuumbua hahaaaaa...ilikuwa inagongana hatari
 
Pia niliwahi kutongozwa na msichana...aisee kuna wasichana wanatongoza huchomoi hata kama una misimamo yako hahaaa
 
Back
Top Bottom