FLASH HIDER
JF-Expert Member
- Jul 13, 2012
- 397
- 508
- Thread starter
- #321
Karibu sana kamanda
Dah huu uzi nao ni mzuri kuna mengi ya kujifunza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah huu uzi nao ni mzuri kuna mengi ya kujifunza
Mimi kutoa maoni haya sio kwamba sitambui maumivu yaliyotokana na Genocide....ilikua ni maumivu makubwa...mauaji mabaya sana pia.....Watusi walikufa...wahutu wengi pia waliuawa na RPF.....Vita popote pale ni mbaya...Na sisi watanzania ndio maana kila siku tunaiombea nchi yetu Amani.......Ila hii ishu mnatakiwa kuiangalia kwa jicho pana na la mbali zaidi ili kuzuia Genocide nyingine au vita nyingine hapo baadaye......Unatakiwa kuiangalia katika mtazamo mpana wa PEACE ,FORGIVENESS AND RECONCILLIATION......Hao FDLR ni watu wa kwenu...Rwanda ni nchi yao.....Amani ya kudumu ni kuongea......Sasa mnataka waendelee kubaki Congo wajipange zaidi>? Au mnataka mkatengeneze majeshi yenu kule Congo kama M23 ili kuwapiga FDLR na ku destablize amani ya Congo? Kumbuka Congo ni Sovereign state............
Hiyo ni 100% pasipo hata na shaka, ila nahofu huu mjadala unakoelekea, tutakosa kilichokusudiwa.
Yes...There you are FLASH HIDER kila nchi ina sovereignty yake...haiwezekani kabisa wewe unakitetea kikundi kinacho de stabilize nchi ya mwenzako......How comes watetezi wa Rwanda ndio wanaitetea M23? That means Rwanda=M23....Simple arithmetics.
Unajua unachokisema?kusaidia FDLR ni kusaidia wauaji wa kimbali,which means you are a supporter of genociders.
Nakubaliana na wewe moja kwa moja lakini sidhani kama suluhisho pekee ni mtutu wa bunduki. Tuache utamaduni wa visasi.
Freeland ni zaidi ya mwalimu. Bila shaka anaweza kutujuza mengi hapa. Tumtumie jamani, elimu haina umri wala wakati.
janja yenu ya kuuhadaa ulimwengu kwa genocide hamna asiyoijua tena, chanzo kikubwa cha mauaji ya kimbari ya rwanda 1994 yaliyoua wahutu na watusi ni kagame na uchu wa madaraka wa watusi
Matatizo ya Congo hayataweza kuisha kwa kutumia bunduki...kuna haja na ulazima wa serikali zinazohusika kukaa katika meza ya mazungumzo....Rwanda wazungumze na hao FDLR ....kitendo cha kutotaka kuongea nao kinasababisha security threat hata Rwanda na DRC.....Kabila amejitahidi kuongea na wapinzani wake M23...Why PK hataki kuongea na FDLR???
Hizo fununu na mimi nimezisikia sana. Unajua DRC ni nchi kubwa kiasi kwamba kuna maeneo hayajawahi kabisa kukaliwa na mtu. Majeshi ya UN yamekuwa wakiweka kambi zao katika maeneo hayo. Kuna uwezekano mkubwa hayo yanafanyika au yalikuwa yanafanyika.
Ni wazi kuwa Rwanda walikuwa wanam-support Nkunda. CNDP (kikundi cha NKUNDA)kilikuwa kinadai kuwa kinalinda maslahi ya Watusi (Wanyamulenge) waliokimbia Rwanda miaka ya 60. Hivyo ajenda hiyo ndiyo ilichukuliwa na Rwanda katika kuhalalisha support yao kwa Nkunda. Ukisoma uzi huu, kuna sehemu nimeeleza kwa kirefu mgogoro huu.
Kilicholeta utofauti wa utendaji wa Majeshi ya UN ya awali na haya ya sasa kwanza ni uzalenda na nia ya dhati ya kutaka kumaliza matatizo ya wa cONGO waliyonayo hawa wanajeshi wa sasa (JWTZ). Inasemekana hapo awali unaweza kusikia watu wanabakwa, badala ya kuchukua hatua hao jamaa wanakuja na kuanza kuchukua video kwa ajili ya kuonyesha kwao. Wacongo hawawapendi kabisa jamaa hao.Pili nimeambiwa kuwa hawa wamepewa nguvu zaidi ya kisheria na UN kuweza kushambulia. Yaani kaka kuna tofauti kubwa sana.
Hakuna anae isaidia FDLR mpaka sasa, suala hapa nini njia muafaka wa kumaliza matatizo na kikundi hiki kilichopo DRC karibu miaka 20 sasa. Ukipendekeza mazungumzo basi wewe kuna wadau (hasa PK) anakuona una support Genocide.
Hakuna anae isaidia FDLR mpaka sasa, suala hapa nini njia muafaka wa kumaliza matatizo na kikundi hiki kilichopo DRC karibu miaka 20 sasa. Ukipendekeza mazungumzo basi wewe kuna wadau (hasa PK) anakuona una support Genocide.
Mkuu nimeona katika ukanda huu wahusika wakuu wa mgogo ro wa DRC ni TZ, RWANDA na UGANDA. Vipi kuhusu BURUNDI??
Mbona wao hawatajwi tajwi katika huu mgogoro maana nachojua wana matatizo sawa na Rwanda hasa ya uhutu na utusi na pia ni jirani wa karibu sana na Congo.
Lakini watu wengine mnapenda kuandika ilimuradi umeandika,ungejua yanayo tendeka goma usinge kua unaongea hayo,watu warwanda wanapiga mzigo kama kawaida kama vile hakuna vita kwa jirani yani hata Gisenyi mji ambao uko mpakani watu wanavuka mpaka kilasiku wakienda goma na wagoma wakiingia gisenyi yani maisha niya kawaida.
Mkuu FLASH RIDER huyu MUKAMMASIMBA ni idara ya intrllijensia ya Rwanda na si mtu mmoja bali seversl people uding the same ID.Sidhani kama mjadala umelenga katika kuleta ushabiki wa vita inayoendelea. Mimi si mwuumini wa vita kabisa.Kama ungekuwa huku GOMA ndiyo ungeona madhara ya vita. Hebu fikiria hapo Kariakoo mchana wa saa tano asubuhi mabomu matatu tanatua, nini madhara yake kwa maisha ya watu, mali na akili za watu hao. Huku hayo mambo nimeyashuhudia watu wakifiwa na watoto na ndugu zao, wanapata walemavu na mali zao kuteketea kwa gharama ya POLENI SANA. Hii ni kwa raia, achilia mbali wanajeshi ambao kwa mujibu wa mazingira yao ya kazi, suala la kifo lipo mkononi kwa maana wamejitolea maisha yao kwa mani ya DRC. Asikwambie mtu, maisha ndiyo kila kitu. Msishabikie vita ndugu zangu.
hilo nalo neno, mkuu mfanyabiashara tunaomba msaada wako katika hili
Mkuu FLASH RIDER huyu MUKAMMASIMBA ni idara ya intrllijensia ya Rwanda na si mtu mmoja bali seversl people uding the same ID.
Its easy to note.
kagame na watusi wenzake ni janga katika eneo la maziwa makuu