Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

MUKAMASIMBA bado nasubiri jibu lako kwa swali langu hapo juu

Mkuu nashukuru sana kwa swali hilo,rwanda ilisha toa msamaha kwa FDLR atakaye rudi rwanda na kujisalimisha na wengi wamekuja zaidi ya 10000 fighters na kua integrated nchini,sasa hao waliobaki ni wale ambao hawataki kurudi kwa maana kwamba bado wako na zile itikadi za kiuaji na wengine wanazuiliwa na hizo nchi za france na UN kurudi ili siri zao zisijulikane lakini iliisha julikana kwani kuwepo kwao huko inafanya kazi iendelee,mimi sio kwamba na support kupigwa FDLR kama wapinzani wa kawaida bali hapa tunaongelea watu wenye itikati za mauaji ya kimbali.
 
Tuwatizame wanaojiita waasi wa Congo, M23, CNDP na FDRL wanaosababisha Kagame aanze kututukana, FDRL ni kikundi cha wanamgambo wa kihutu ambao ni adui wakubwa wa kagame na ndugu zake watusi.

Baada ya halaiki wakatimkia Congo amabako hata leo wanaota kumtimua Kagame madarakani hawa ni wahutu raia wa Rwanda wanaompinga Kagame.

Hawa M23 wametokana na CNDP kilichaanzishwa na jamaa yao Museveni na Kagame, Jenarali Nkundabatware mwaka 2006 huko Kivu.
 
Mimi nimeamua kuacha kubishana/kujadiliana na MUKAMASIMBA. Anataka kunilazimisha nianze kuwachukia watusi wakati ndiyo rafiki zangu na tunafanya nao kazi hapa. Hawa wa hapa GOMA ni wawazi sana kuhusu Rwanda na M23. Sijui huyu bwana hard core anautoa wapi.

QUOTE=juve2012;7695049]MUKAMASIMBA bado nasubiri jibu lako kwa swali langu hapo juu
[/QUOTE]

Sorry,nichukie mimi mwenyewe kwani ni mimi mwenye visa na wewe,sio wote tena mimi sio mtusi.
 
Hawa MONUSCO kazi yao kupora madini na kuuza ughaibuni, na wala soyo kulinda raia wa Congo kama walivyotumwa na Umoja wa Mataifa.
 
ndio hapo sasa!kwa sera za mheshimiwa huyu,ina maana tuanze kufuatilia mipaka kwa empire za zamani zilizozingatia mipaka ya kikabila.Sasa sijui waluo,wamasai,wapare,wamakonde,na nchi nyingine kwenye makabila yaliyosambaa kwenye nchi zaidi ya moja nayo yakifuata sera hizi leo sijui itakuwaje!

Mimi ninachotaka kukueleza ni kwamba rwanda wao walikua na mipaka yao kwani walikua na ufalme imara sana na kulikua kunaitwa rwanda,lakini baada ya kuona hawa wanyarwanda wagomvi ndio wakaamua kukakatakata kakabaki kadogo lakini hawakuweza kuwahamisha wananchi walibaki katika maeneo hayo,nikusema congo kuna wahutu nawatusi lakini jamaa wamekomalia watusi tu.
 
Naona unaanza kudanganya sasa.
Kabla ya kukata mipaka inakuwa je Rwanda ilikuwepo? sasa huu ni usanii sasa, yani nchi zingine hazikuwepo ila Rwanda ilikuwepo ndo ilikatwa mipaka?

hebu nenda kwa research uangalie ufalme wa rwanda,rwanda ilikuwepo tangu zamani,na kinacho onyesha rwanda ni mipaka ya ufalme wa rwanda walikua organised tangu zamani kwani mtemi mkwawa hakua na eneo alilio kua akitawala? sasa hapo zamani palikua rwanda kingdom na mipaka yake ilifika congo kivu na uganda ufumbira.
 
Hawa MONUSCO kazi yao kupora madini na kuuza ughaibuni, na wala soyo kulinda raia wa Congo kama walivyotumwa na Umoja wa Mataifa.

Ndio maana vita hazitaisha kongo hata tz ikianza kusikia utamu wa kupora haitatoka huko wataoa wacongomani na kuzamia huko.
 
Kama wewe siyo Mtusi basi hao watusi unaowatetea kwa hoja nyepesi unawasababisha waanze kuchukiwa na jamii kubwa ya watu. Kama si mtusi basi huwezi kuwa mtetezi mzuri. Inawezekana wenyewe wanajua ukweli ndiyo maana wamekaa kimya.


Sorry,nichukie mimi mwenyewe kwani ni mimi mwenye visa na wewe,sio wote tena mimi sio mtusi.[/QUOTE]
 
Wewe una kitu na TZ nadhani. Au ndiyo maana PK hataki nchi ya RDC itawalike aendelee kula mali ya DRC? Muwaache jamani waCongo, nao ni watu, wana nchi yao na mambo yao.

Ndio maana vita hazitaisha kongo hata tz ikianza kusikia utamu wa kupora haitatoka huko wataoa wacongomani na kuzamia huko.
 
Mkuu FLASH HIDER tunashukuru sana kwa taarifa unazotupatia,mimi binafsi umenifungua macho.Maswali yangu ni: 1.vipi kuhusu vikundi vingine vyenye silaha kama FDLR navyo vinanyang'anywa silaha?
2.Mbali na kunyang'anywa maeneo waliyokuwa wameyakalia je kuna maafa gani mengine makubwa ambayo M23 wameyapata?
3.Je kuna askari wa Rwanda waliouawa ambao walikuwa wanapigana sanjari na M23?
4.Vipi kuhusu Sultani Makenga na viongozi wenzie kuna ambaye kakamatwa au kuuawa au wamekimbilia wapi?
 
Last edited by a moderator:
sasa wewe ndio wazimu imekupanda eti rwanda iongee na fdlr? Sahaukabisa hiyo haita wezekana,kingine m23 haija chapwa hatakidogo wameondoka wote tena wazima wa afya njema,fib imeumizwa sana yani hasira nizote,wewe uliza goma wakupe mkanda wote uache kuongelea kitandani watu huko wanaumia sio mchezo.

kuna goma ngapi? Labda ya goma ya kigali
 
Bado nasema MUKAMASIMBA hajielewi, ukiongea uwongo unatakiwa uwe unakumbuka vizuri.
MUKAMASIMBA anamaanisha kwamba M23 wamepelekwa na Kagame kule DRC ili kupambana na FDLR ili wawazuie wasije wakarudi Rwanda(wawa-disturb FDLR).
Kwa upande mwingine MUKAMASIMBA anasema b4 mipaka haijagawanywa na wazungu watu walikuwa wana-move tu ndiyo watutsi wakawa wameenda Kivu mipaka ilivyogawanywa wakawa wako huko kivu, (wahutu hawakwendaga Kivu b4 mipaka haijagawanywa) Sasa kama watutsi wa DRC wako huko Kivu wanaleta fujo hukko nyie Rwanda (tutsi MUKAMASIMBA) inawahusu nini kama hao huko DRC (M23)wakipigwa tu kwa sababu wanaleta fujo, wanauwa watu, wanabaka watoto/wamama, uwizi wa madini, uwizi wa mali za innocent civillians??
Au unamaanisha Jaluo wa Kenya akifanya uvunjifu wa sheria/amani huko Kenya then Akapigwa TU ina maana Jaluo wa TZ na Serikali yake waende huko Kenya wakawasaidie wajaluo wenzao kwa sababu wajaluo wanapigwa huko Kenya??

Hawa watutsi waliohamia Uganda, Kenya, Kigoma/Kagera TZ, Burundi mbona hawaleti fujo/vita?? Mbona Hakuna M23 huko??
Au kwanini huwaongelei hao???

M23 ni wanyarwanda raia hai wa Rwanda tena watutsi waliovamia DRC kwa ajili ya KUIBA Diamond na rasilimali nyingine kwa manufaa ya Rwanda.
Rwanda ina Rasilimali gani mpaka sasa inayojulikana??

MUKAMASIMBA wewe ni Al Saif wa Kagame na nadhani unakesha kwenye jf kumtetea Kagame tatizo ni kwamba unachanganyikiwa hujui hata uliandika nini b4 au hii ID ya MUKAMASIMBA inatumika na more than 1 user.
 
Last edited by a moderator:
hivyi ninvyoandika ninaangalia tv hapa, miji yote ambayo ilikuwa imekaliwa na m23 imekwishachukuliwa na fardc. Kanzia kiwanja, rumangabo, katale, kibati (ulichukuliwa siku nyingi) yote ipo chini ya fardc. Wamebakiza mji wa bunagana ambapo ni mpakani kabisa na uganda. Bila shaka kufikia kesho mtasikia m23 imekwisha. Tuombe yasitokee tena mauaji kwa jwtz maana naambiwa wanafanya kweli huko front.

ulitabiri kweli mzee. Bbc leo wametangaza bunagana imechukuliwa na majeshi ya drc na m23 wamekimbilia uganda
 
bado nasema mukamasimba hajielewi, ukiongea uwongo unatakiwa uwe unakumbuka vizuri.
mukamasimba anamaanisha kwamba m23 wamepelekwa na kagame kule drc ili kupambana na fdlr ili wawazuie wasije wakarudi rwanda(wawa-disturb fdlr).
Kwa upande mwingine mukamasimba anasema b4 mipaka haijagawanywa na wazungu watu walikuwa wana-move tu ndiyo watutsi wakawa wameenda kivu mipaka ilivyogawanywa wakawa wako huko kivu, (wahutu hawakwendaga kivu b4 mipaka haijagawanywa) sasa kama watutsi wa drc wako huko kivu wanaleta fujo hukko nyie rwanda (tutsi mukamasimba) inawahusu nini kama hao huko drc (m23)wakipigwa tu kwa sababu wanaleta fujo, wanauwa watu, wanabaka watoto/wamama, uwizi wa madini, uwizi wa mali za innocent civillians??
Au unamaanisha jaluo wa kenya akifanya uvunjifu wa sheria/amani huko kenya then akapigwa tu ina maana jaluo wa tz na serikali yake waende huko kenya wakawasaidie wajaluo wenzao kwa sababu wajaluo wanapigwa huko kenya??

Hawa watutsi waliohamia uganda, kenya, kigoma/kagera tz, burundi mbona hawaleti fujo/vita?? Mbona hakuna m23 huko??
Au kwanini huwaongelei hao???

M23 ni wanyarwanda raia hai wa rwanda tena watutsi waliovamia drc kwa ajili ya kuiba diamond na rasilimali nyingine kwa manufaa ya rwanda.
Rwanda ina rasilimali gani mpaka sasa inayojulikana??

mukamasimba wewe ni al saif wa kagame na nadhani unakesha kwenye jf kumtetea kagame tatizo ni kwamba unachanganyikiwa hujui hata uliandika nini b4 au hii id ya mukamasimba inatumika na more than 1 user.

huyu mukamasimba tatizo lake ni ufinyu wa shule kama bosi wake kagame! Hajui hata anachokisemea
 
Mkuu FLASH HIDER naomba nikupe ushauri mdogo tu
ukikutana na post ya MUKAMASIMBA, Koba au murutongore (kwasasa keshalamba BAN) hawa wametumwa kuvuruga na kutetea post zozote zitaoihusu Rwanda au Tutsi (chochote kitakachowahusu Watutsi)
nimeshangaa kuna post MUKAMASIMBA anadai kuwa Rwanda lilishakuwa na utawala wa eneo kubwa likamegwamegwa
Hapo hataki kufafanuaila ni kuukandamiza uongo wake kwanimara zote tulishamwambia Historia inawakataa Watutsi hasa kwenye Maziwa Mkuu na DRC kuwa hawa watu ni wageni na hizi Nchi si zao wanazotaka kuzitawala, Mch. Mtikila alishawaeleza kuwa nia yao sio nzuri kwa Mbantu na hata sisi Watanzania ndio maana leo wanapokea kipigo na bado wanaficha ukweli
24153476.jpg
Hizo Nchi zilikuwa ni za waTwa na Wahutu yeye Mtutsi ni mgeni.
It is said the Hutu arrived in central east Africa somewhere in the 1st century. Before then, the land was inhabited by the Twa. The Twa were pushed out and forced to flee by the Hutu. The Tutsi invaded around the 15th century. They came from the horn of Africa.
The Tutsi, or originally Cushite, people migrated to Rwanda from the southern Ethiopian highlands, and were much taller and thinner in physique than the Bantu or Twa. Throughout the entire history of their population of Rwanda, the Tutsi have never exceeded 15% of the population. Despite their lack of numbers, the Cushite people arrived as conquerors. The Cushite were cattle-herding warriors, and they impressed their power upon the Bantu (and Twa) of the region.

By the 15th century, the Cushite had gained complete rule. They established an pyramid-style political structure, with the head being an Mwami, a king of supposedly divine origin. The reign of the Tutsi Mwami over Rwanda continued for several hundred years very successfully. Hutus who were wealthy enough were accepted as part of the elite along with the Tutsi, while poorer Hutus lived quite comfortably to themselves, provided they pay a tax to the Mwami. In brief, the Tutsi were in power and as such elevated themselves to higher class than the Hutus
History of Hutu – Tutsi Relations | The Rwandan Genocide
Si ajabu sasa wanataka kutawala na kwetu baada ya kuwadhulumu WaTwa na WaHutu

Kuhusu M23 mpaka kesho tutapata jibu la hivi Vita kwisha
maana kipigo cha JWTZ Bisii ameenda muuliza M7 ni kweliau wanaota? zimebaki kilometa 5 tu kuifikia Bunagana
955219_orig.jpg

Bisii" The Bisiimwa's vehicles enter Uganda. (photo: Goodluck Musinguzi/NewVision Uganda)
Just head this news on BBC World News Radio, and now cross-posting the following report written by Goodluck Musinguzi, published at NewVision*, UGANDA that, the rebel leader crossed Uganda in a convoy of two vehicles as UN forces and Congolese forces led by South Africans reached within five kilometres towards his political base.
A Uganda security officer confirmed the development and said Bisiimwa was being questioned by the security operatives at Bunagana at Uganda-Congo border.
Source: [update] M23 leader Bertrand Bisiimwa in Ugandan - wavuti.com

 
Kama nimeelewa sawa anachokisema mukammasimba maana yake ni kuwa kama M23 watakuwa wamekimbia na majeshi ya Sadc na Monusco yakadharau uwepo wa FDLR tunaweza kushuhudia mauajii mengine ya kimbari dhidi ya watutsi wanaoishi Congo na hasa hao waaeneo ya kivu ya kusini, kama ni kweli hii haileti maana
 
Ndio maana vita hazitaisha kongo hata tz ikianza kusikia utamu wa kupora haitatoka huko wataoa wacongomani na kuzamia huko.
Mkuu Mukamasimba Watanzania hatuna hulka/kawaida ya kupora rasilimali za Mataifa mengine, pili - Tanzania ina wanawake/wasichana wa kila sampuli - chaguo lako, Watanzania si limbukeni wa kutekwa na wanawake wa nchi nyingine mpaka akajikuta amezamia kabisa - kama ni suala la nyumba ndogo atatafuta hapa hapa sio kukimbilia nchi za wenzetu.
 
Ukwaju ndugu zako FDLR or Congolese wakijaribu kufanya walichofanya 1994 Rwanda huo ndio utakuwa mwisho wa utawala wa Kabila na mwanzo wa utawala wa Banyamulenge Kinshasa.
 
ninasikia mademu wa huko kongo wanahusudu sana wabpngo, eti ni kweli?
halfu nasikia vijana wa huko wanajiremba sana , unaweza kuta mtu anakaa kwenye kijinyumba cha ushenzi lakini amevalia kipapaa sana,, n hayo tu,naomba kueleweshwa
 
Back
Top Bottom