M23 Wanashikilia miji mingapi na ipi hadi sasa? idadi ya jeshi la waasi ni kama wangapi?
Du! Mkuu sijui kwa nini imetokea nikamkumbuka yule waziri wa habari wailiyokuwa iraq ya saadam hussein maarufu kama komedi/comic ally.
Swali langu la msingi vipi kuhusu zana za kivita walizo nazo hawa wapiganaji wetu? Maana kuna siku wameonekana kwenye tv wamejazana kwenye p/up double cabin la UN. Je hii haiwezi hatarisha maisha yao zaidi?
umetupatia habari njema sehemu kubwa uliyosema imebidi niende kwenye source zangu at least 90% upo sahihi,turushie picha hata moja tuu kuonyesha hali halisi ilivyo,
una habari zozote kwanini Malawi wamechelewa kufika Goma?
Naomba unitajie fursa zilizoko hapo hasa upande wa madini?
Ndugu zanguni hasa Watanzania,
Mimi ni mtanzania ninafanya biashara zangu huku DRC Goma kwa muda mrefu. Ninaishi hapa GOMA na nimekuwa nikisafiri kwenda sehemu mbalimbali ndani ya DRC.
Nimekuwa nikifuatilia mijadala kuhusu mgogoro wa M23 na serikali ya DRC, nimegundua watu wengi hawapo informed on what is going on.
Sasa kwa wale wenye swali au chochote wanachotaka kujua kuhusu mgogoro huu, mapigano yanayoendelea, na ushiriki na mapokeo ya WaKongo kuhusu JWTZ, mnaweza kuniuliza.
Nipo hapa kwa karibu miaka kumi na mbili sasa, bila sahaka nina kitu kipya ambacho huenda ninaweza kuwahabarisha.
Hapo Goma,kuna mahusiano mazuri kati yenu wabongo na wanyarwanda hivi sasa?ukiwa mji wa mashariki mwa Congo,idadi ya raia wenye asili ya Rwanda ikoje hapo?Kuna kabila lolote la hapo lenye uhusiano wa damu na wanyarwanda au wote walioko hapo ni wahamiaji?
Nashukuru kama ume assess na kugundua ninachozungumza kinakaribiana na ukweli. Naomba tusaidiane hiyo 10 % ambayo si sahihi ili niwe records zangu vizuri. Upande wa pili, Sijajua kwanini Malawi walichelewa kuwasili GOMA. Na kuhusu fursa za madini hata kama hupendi kusikia nitakueleza tu. Hapa biashara kubwa ni madini, karibu tuwe wengi kaka.
You are a good man. Tunaitaji watu kama wewe JF sio hoa......kazi kubwa kulinda matumbo yao.
asante kwa taarifa na uniwie radhi kwa kukudhiki hapo mwanzo, kwa taarifa nina fununu kuwa kjeshi letu pia kwa sasa linawafundisha wanajeshi wa congo kule arusha..... kulingana na taarifa ni kwamba ndo hao baadhi wanaonyesha uhai wa jeshi la congo kwenye uwanja wa mapigano
Leo asubuhi tumesikia kuwa mpaka sasa askari 7 wa Tanzania wamekufa huku kwetu tunajua mmoja tu, hebu tueleze ukweli.
Kwa nini nchi kubwa km kongo ishindwe vita na nchi ndogo km Rwanda unasemaje kuhusu hili.
Unafikiri vita ikiisha Tanzania ina fursa gani kiuchumi, ukizingatia kuwa bidhaa kutoka Tanzania kwenda Goma lazima zipite Rwanda iliyopandisha ushuru pia hakuna maelewano na Tz.
Je kuna njia nyingine kupitia Burundi kutokea Kigoma kwenda Kongo DRC na km ipo unashuri nini serikali yetu.
Iyo amri labda umepewa mwenyewe. Muache mdau aelimishe watu kuhusu mgogoro huu ili wajue umuhimu wa kuruhusu jeshi letu kusaidia huko au tunabebwa na agenda za kimataifaUmenena vyema kuwa wewe ni mtanzania ambaye umelowea Goma. Inaonekana huna habari na amri ya JWTZ kuwa sisi wananchi haturuhusiwi kuongelea masuala ya vita ya huko Congo mpaka kwa kibali chao. Angalia usije ukaingia matatizoni na jeshi letu kwa kuongelea vita ambayo tayari kuna katazo la chombo chetu cha ulinzi na usalama.
Kama unafuatilia vizuri jamaa walifanikiwa kuwa-push back na mapigano yakasimama kabisa. UN iliamua kuwa yafanyike mazungumzo ya kumaliza mgogoro huu. Hapo ndipo majeshi hayo yalitakiwa kurejea makwao. Kumbuka hiyo ilikuwa ni initiative ya SADC.
Mbona unaonekana km mtu uliyeenda shuke na unajua mambo hasa socialogy na polotical, we unafanya biahsra kweli au ni intelenjesia wetu unafanya kazi yako? hebu tueleze una muda gani unafanya u-FBI huko< tunakuomba usiwe kama mmarekani snoden. Naamini huwezi kuwa businessma huko kwa mtutu uliopo huko siyo rahisi. una uelewa mkubwa.
Ndiyo maaana nasema kwa yale niyawezayo nitayajibu. RDC ni kubwa na mgogoro ni complex. Sikusudii kudanganya.
nimepitia mkuu na nashukuru kwa majibu yakonkunda kwa sasa yupo under house arrest huko rwanda. Ana uhusiano mkubwa na m23 kwani yeye andiyo mwanzilishi wa cndp(the national congress for the defence of the people (kwa kifaransa congrès national pour la défense du peuple) ambalo ndiyo chumbuko la m23. Hebu pitia uzi huu kwa ujumla nimejaribu kuelezea uhusiano wa m23 na nkunda laurent