Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

umetupatia habari njema sehemu kubwa uliyosema imebidi niende kwenye source zangu at least 90% upo sahihi,turushie picha hata moja tuu kuonyesha hali halisi ilivyo,

una habari zozote kwanini Malawi wamechelewa kufika Goma?

Naomba unitajie fursa zilizoko hapo hasa upande wa madini?
 
Hayo magari wanayo na pia yale kama vifaru pia yapo. Sijui ni kwanini lakini hata wanajeshi wa DRC, India na Pakistan wanatumia magari hayo hayo kwa movement kutoka eneo moja kwenda lingine. Usinifananishe kaka mimi na yule Waziri wa Ulinzi wa Iraq, nitake radhi bwana Pache.

Du! Mkuu sijui kwa nini imetokea nikamkumbuka yule waziri wa habari wailiyokuwa iraq ya saadam hussein maarufu kama komedi/comic ally.

Swali langu la msingi vipi kuhusu zana za kivita walizo nazo hawa wapiganaji wetu? Maana kuna siku wameonekana kwenye tv wamejazana kwenye p/up double cabin la UN. Je hii haiwezi hatarisha maisha yao zaidi?
 
umesema m23 wapo bunagana mpakani na uganda ikiwa na maana wanaweza kukimbilia uganda na sio rwanda.kwani wamesambaa kiasi gan?
 
Nashukuru kama ume assess na kugundua ninachozungumza kinakaribiana na ukweli. Naomba tusaidiane hiyo 10 % ambayo si sahihi ili niwe records zangu vizuri. Upande wa pili, Sijajua kwanini Malawi walichelewa kuwasili GOMA. Na kuhusu fursa za madini hata kama hupendi kusikia nitakueleza tu. Hapa biashara kubwa ni madini, karibu tuwe wengi kaka.

umetupatia habari njema sehemu kubwa uliyosema imebidi niende kwenye source zangu at least 90% upo sahihi,turushie picha hata moja tuu kuonyesha hali halisi ilivyo,

una habari zozote kwanini Malawi wamechelewa kufika Goma?

Naomba unitajie fursa zilizoko hapo hasa upande wa madini?
 
asante kwa taarifa na uniwie radhi kwa kukudhiki hapo mwanzo, kwa taarifa nina fununu kuwa kjeshi letu pia kwa sasa linawafundisha wanajeshi wa congo kule arusha..... kulingana na taarifa ni kwamba ndo hao baadhi wanaonyesha uhai wa jeshi la congo kwenye uwanja wa mapigano
 
Ndugu zanguni hasa Watanzania,

Mimi ni mtanzania ninafanya biashara zangu huku DRC Goma kwa muda mrefu. Ninaishi hapa GOMA na nimekuwa nikisafiri kwenda sehemu mbalimbali ndani ya DRC.

Nimekuwa nikifuatilia mijadala kuhusu mgogoro wa M23 na serikali ya DRC, nimegundua watu wengi hawapo informed on what is going on.


Sasa kwa wale wenye swali au chochote wanachotaka kujua kuhusu mgogoro huu, mapigano yanayoendelea, na ushiriki na mapokeo ya WaKongo kuhusu JWTZ, mnaweza kuniuliza.

Nipo hapa kwa karibu miaka kumi na mbili sasa, bila sahaka nina kitu kipya ambacho huenda ninaweza kuwahabarisha.

Naomba kujua historia ya mgogoro wa DRC, kuna uhusiano gani uliopo kati ya mgogoro huo na nchi za Rwanda, Uganda na Tanzania?
 
You are a good man. Tunaitaji watu kama wewe JF sio hao......kazi kubwa kulinda matumbo yao. 2015 tutawafundisha adabu na kuirudisha heshima ya Tanzania yetu.
 
Ukweli hapa GOMA ni mchanganyiko. Unajua hapa ni bussiness center. Kuna wa Congo, Wazambia, Warundi, watusi waliokimbia vita ya mwaka 60 (wanyamulenge) na wale Wahutu waliokimba hii ya mwaka 94. Uhusiano wetu na wao sio mbaya ingawa kwenye suala la kuvuka mpaka hivi karibuni hasa kwa Watanzania lilitaka kuonekana gumu. Ila kwa ujumla ni shwari.
Karibuni


Hapo Goma,kuna mahusiano mazuri kati yenu wabongo na wanyarwanda hivi sasa?ukiwa mji wa mashariki mwa Congo,idadi ya raia wenye asili ya Rwanda ikoje hapo?Kuna kabila lolote la hapo lenye uhusiano wa damu na wanyarwanda au wote walioko hapo ni wahamiaji?
 
Nashukuru kama ume assess na kugundua ninachozungumza kinakaribiana na ukweli. Naomba tusaidiane hiyo 10 % ambayo si sahihi ili niwe records zangu vizuri. Upande wa pili, Sijajua kwanini Malawi walichelewa kuwasili GOMA. Na kuhusu fursa za madini hata kama hupendi kusikia nitakueleza tu. Hapa biashara kubwa ni madini, karibu tuwe wengi kaka.

huku mashariki mwa nchi tupo na Wacongo wote wana mtazamano chanya juu ya Jwtz ila wanashaka na sisi watz kuwa maneno mengi sana kwenye biashara,

hali ya usalama kiujumla ikoje?usafiri na malazi yakoje?
 
Sina uhakika na hilo kwa sasa. Ila wale waliofundishwa mwaka 1997 ndiyo wanafanya kweli sasa.

asante kwa taarifa na uniwie radhi kwa kukudhiki hapo mwanzo, kwa taarifa nina fununu kuwa kjeshi letu pia kwa sasa linawafundisha wanajeshi wa congo kule arusha..... kulingana na taarifa ni kwamba ndo hao baadhi wanaonyesha uhai wa jeshi la congo kwenye uwanja wa mapigano
 
Leo asubuhi tumesikia kuwa mpaka sasa askari 7 wa Tanzania wamekufa huku kwetu tunajua mmoja tu, hebu tueleze ukweli.

Kwa nini nchi kubwa km kongo ishindwe vita na nchi ndogo km Rwanda unasemaje kuhusu hili.


Unafikiri vita ikiisha Tanzania ina fursa gani kiuchumi, ukizingatia kuwa bidhaa kutoka Tanzania kwenda Goma lazima zipite Rwanda iliyopandisha ushuru pia hakuna maelewano na Tz.

Je kuna njia nyingine kupitia Burundi kutokea Kigoma kwenda Kongo DRC na km ipo unashuri nini serikali yetu.

Mkuu kuna Bara bara inajengwa kwa kiwango cha lami kutoka Sumbawanga Mpaka Kasanga, about 120 Km, Kasanga kuna Bandari kubwa sana ambayo bado inajengwa kwenye Ziwa Tanganyika kueleka Congo, Ujenzi wa Bara Bara Kabila Mwenye anasimamia Shoo, Nadhani hataki huu sumbufu wa Kupitia Rwanda ama Zambia
 
Umenena vyema kuwa wewe ni mtanzania ambaye umelowea Goma. Inaonekana huna habari na amri ya JWTZ kuwa sisi wananchi haturuhusiwi kuongelea masuala ya vita ya huko Congo mpaka kwa kibali chao. Angalia usije ukaingia matatizoni na jeshi letu kwa kuongelea vita ambayo tayari kuna katazo la chombo chetu cha ulinzi na usalama.
Iyo amri labda umepewa mwenyewe. Muache mdau aelimishe watu kuhusu mgogoro huu ili wajue umuhimu wa kuruhusu jeshi letu kusaidia huko au tunabebwa na agenda za kimataifa
 
Hivi mkuu unaionaje hii hali ya kila wakati m23 wakielemewa,kuna mataifa hasa haya ya figisufigisu yanashinikiza kusitishwe mapigano waongee. Na wakati wakiongea,m23 ndio wanavuta pumzi na kujipanga. Hauoni ni muhimu kuendelea kuwafurusha mpaka waombe poo!?
Kama unafuatilia vizuri jamaa walifanikiwa kuwa-push back na mapigano yakasimama kabisa. UN iliamua kuwa yafanyike mazungumzo ya kumaliza mgogoro huu. Hapo ndipo majeshi hayo yalitakiwa kurejea makwao. Kumbuka hiyo ilikuwa ni initiative ya SADC.
 
Mimi nipo huku kwa miaka 10 sasa. Nimetia timu huku katika kuhangaika na maisha baada ya mambo kuwa magumu huko Dar na Arusha. Kujua masuala ya socialogy na polotology yasikutishe, si kweli kuwa wafanyabiashara ni tabaka lisilokuwa na elimu.

Niulize kuhusu DRC kaka au yameisha?

Mbona unaonekana km mtu uliyeenda shuke na unajua mambo hasa socialogy na polotical, we unafanya biahsra kweli au ni intelenjesia wetu unafanya kazi yako? hebu tueleze una muda gani unafanya u-FBI huko< tunakuomba usiwe kama mmarekani snoden. Naamini huwezi kuwa businessma huko kwa mtutu uliopo huko siyo rahisi. una uelewa mkubwa.
 
Mdau hebu elezea ushiriki wa marekani katika mgogoro huu upoje? habari zilizopo ni kuwa kuna uhusika mkubwa wa mataifa ya kigeni hasa marekani. Interest kuu ni rasilimali zilizopo Congo (zaidi madini).Walimtumia Kagame akishirikiana na Mu7 kuharibu hali ya amani consistently ili waendelee kutimiza interest zao, lakini pia ushiriki wa tanzania katika kipindi hiki una mgongo wa Marekani.(Kwa kifupi Tanzania imetumiwa na Marekani)
Kagame hajatenda kadiri ya maelekezo ya marekani kwani naye amekuwa akichota rasilimali na kuijenga Rwanda na kufaidikia kuliko anayemtuma (hii pia inasemekana ndo chachu ya maendeleo ya haraka ya Rwanda). Hivyo Marekani anatumia JWTZ kuimaliza M23 yenye ufadhili wa Kagame na Mu7 kama njia ya kumshikisha adabu Rwanda. Inasemekana ziara ya juzi iliyowakutanisha kwa pamoja Obama na Bush hapa Tanzania ina nyayo za huu mgogoro. Hebu endelea kufunguka kuhusu hizi nilizoziita "inasemekana, inasemekana, inasemekana....."
 
nkunda kwa sasa yupo under house arrest huko rwanda. Ana uhusiano mkubwa na m23 kwani yeye andiyo mwanzilishi wa cndp(the national congress for the defence of the people (kwa kifaransa congrès national pour la défense du peuple) ambalo ndiyo chumbuko la m23. Hebu pitia uzi huu kwa ujumla nimejaribu kuelezea uhusiano wa m23 na nkunda laurent
nimepitia mkuu na nashukuru kwa majibu yako
nasikia nkunda alipandikizwa na kinamseveni na kagame kwa ajili ya kupora mali ya drc kulipia ahadi walizopeana na kabila, na kunatetesi hawa ndo walimuua huyu mzee?
 
Mkuu Flash Hider umenifurahisha sana.Ila ntakusumbua wakati mwingine kuhusu biashara ya madini huko.Nafikira kuja huko hali ikitulia.
 
Back
Top Bottom