Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Hawa MONUSCO kazi yao kupora madini na kuuza ughaibuni, na wala soyo kulinda raia wa Congo kama walivyotumwa na Umoja wa Mataifa.

Alafu wako wengi sana zaidi ya 20,000. Miaka kibao sijuhi wanafanya nini huko, Maana FBI wamekwenda hapo 3000 tu , hata mwaka haujaisha kazi kwisha.
 
Mbona wewe muoga? huwezi kamata silaha,halafu hakuna kichapo chochote kwa M23 wamehama tu,game lime change sasa huwezi kua mtu 2000 unapigana na watu 100000 kama siafu ahahahhaa,sasa ni kuchomoa siafu moja moja mpaka zitakapo isha.

wewe piga manenooo lakini ole ole ole wako tukutie mikononi, utajuta kukutana uso kwa uso nasisi. wewe bwabwaja tu lakini tusikutie mikononi mwetu.
 
Ukwaju ndugu zako FDLR or Congolese wakijaribu kufanya walichofanya 1994 Rwanda huo ndio utakuwa mwisho wa utawala wa Kabila na mwanzo wa utawala wa Banyamulenge Kinshasa.

Mauaji ya kimbari hayawezi kutokea Congo,na hata Rwanda hayawezi kutokea tena kwani mpaka sasa mataifa ya magharibi yanajuta kwanini hawakuingilia kati kijeshi kuinusuru Rwanda.Hasa Marekani wakati ule wa utawala wa Raisi Clinton-1994.

Ila kinachoweza kutokea ni kuanguka kwa serikali ya Kagame,kama hata fanya bidii ya kujenga taasisi imara za kidemokrasia inayowahusisha raia wote hata wale anaodhani wana ideology ya mauaji ya kimbari.Ikiwa reconciliation +(gachacha) ilifanyika basi hakuna haja ya kuwachukulia wengine kuwa ni kitisho ukizingatia kuwa wengi wao waliofanya mauaji hayo wengi wameishatiwa mbaroni,na wengine wameishakufa huko msituni Congo kutokana na umri wao. Hicho kizazi kilichopo huko FDLR ni kipya kwani wengi wao wakati wa mauaji 1994 walikuwa vijana wadogo sana na yamkini wengine walikuwa hawajazaliwa kabisa.

Cha msingi ni kujenga Taifa Imara lisilo na utawala wa kibaguzi kitu ambacho bado ndio kinaitafuna Rwanda kwa miaka mingi na kuwafanya watu wanao zungumza lugha moja wasiaminiane. Anyway it is a process......Lakini lazima mchakato wa unification kati ya(tus/hut/twa) ufanyike haraka iwezekanavyo.

Resources zilizokuwa zinatumika ku i finance M23 zitumike sasa kujenga umoja na mshikamano wa clans(tus/hut/twa) zote ndani ya Rwanda,achaneni na vita visivyoisha havitaleta tija yoyote kwenu ninyi jengeni Taifa lenu kwani bado liko very fragile,....wahutu wanataka nao warudi watawale nchi....!!!
 
Ndugu yangu katika hili swala la watusi watu wengi huongea uongo dhidi yao na ndio maana wahutu waliweza kuwaangamiza juu ya hayo masomo yachuki waliyo tiwa kichwani,na kinacho nishangaza nina wapa ukweli wote kuhusu hao watu lakini watu wanang'an'gania wanayotaka kusikia,ninacho jua ukweli utajulikana,watusi wanaonewa sana,hata wakichinjwa hakuna mtu wa kuwatetea lakini kinacho julikana mungu yuko pamoja nao atawalinda kama walivyo weza kuwashinda wauwaji nchini rwanda.

hivi wewe ni mtusi eti?
 
Where is Sultan Makenga?, (m 23 military chief) it was believed tha he was severely injured, was that true?
 
ninasikia mademu wa huko kongo wanahusudu sana wabpngo, eti ni kweli?
halfu nasikia vijana wa huko wanajiremba sana , unaweza kuta mtu anakaa kwenye kijinyumba cha ushenzi lakini amevalia kipapaa sana,, n hayo tu,naomba kueleweshwa

...............haa..haaa...hhaa ! huko mpaka muuza mayai anaimba ile mbaya :smile-big:
 
Madini ya Coltan yametajwa kuleta hali ya sintofahamu.Haya madini yanatumika kutengeneza CPU ya simu na lama unavyojua technology ya mawasiliano inavyokuwa ndivyo haya madini huitaji wake inavyoongezeka,coltan IPO CONGO kwa kiwango kikubwa sana zaidi kivu ya kaskazini.Mataifa kama USA na China wamekuwa wa watumia business elites wakibeligium kukusanya madini Congo, kunareport ya UN imewataja hao watu..hayo madini yanasafirishwa kwa ndege Tokay Congo hadi Mombasa then to China ambapo kunacheap labor of man power.Kampuni za simu tajwa ni Motorola na Nokia, so fedha inaenda master planners then inarudi kufadhili rebels Congo na associate just kufanya Congo isisettle ili wao wandelee kuchuma.So kama unadeal na madini Congo no blood miniral..hii deal Israel pia wamo ndo wanunuzi wakubwa humo...wachimbaji ni wacongo wenyewe..mamiddle men ndo nyiye...tafuta blood coltan' IPO YouTube.
As long as economic is concerned Congo won't settle hao kina Pk .nkunda.m7.etc wanatumika na visababu vya hapa na pale.Chezea midini.mafuta na gesi.
tchao.
 
Hawa jamaa wanahasira za bure tu,hawautaki ukweli,hizo articles zimeandikwa na wapinzani wa pk na zingine sponsored by france ili kuharibu sura ya pk,utakua hittler ukaishi dunia yaleo? hizo ninjama za watu wachache,rwanda hivi inaongozwa vizuri na wananchi wanaufurahia uongozi wake.

Don't be a fanatic for nothing. Kumbuka hata Rwanda ya kina Habyarimana iliongozwa vizuri tu kabla ya PK kuanzisha cold war, unakumbuka hii? PK baada ya kuingia Rwanda amejaribu kuzima ukweli kwa kuua watu (generals na viongozi wengine) waliomkimbia, unataka kutuambia kuwa hii wewe hujuwi na kama hujuwi sasa kwanini unabisha ama kukataa ukweli, si ni ujinga huo? PK is a blatant killer, his time is coming though because God will never let him live long enough before fate will follow him. Jiulizeni, whatever happened to Hitler, Iddi Amini, Mobutu, Sadam Hussein, Samuel Doe, Taylor, Gaddafi?
 
Mkuu FLASH HIDER tunashukuru sana kwa taarifa unazotupatia,mimi binafsi umenifungua macho.Maswali yangu ni: 1.vipi kuhusu vikundi vingine vyenye silaha kama FDLR navyo vinanyang'anywa silaha?
2.Mbali na kunyang'anywa maeneo waliyokuwa wameyakalia je kuna maafa gani mengine makubwa ambayo M23 wameyapata?
3.Je kuna askari wa Rwanda waliouawa ambao walikuwa wanapigana sanjari na M23?
4.Vipi kuhusu Sultani Makenga na viongozi wenzie kuna ambaye kakamatwa au kuuawa au wamekimbilia wapi?

Ndugu zangu kwa current affairs, ninatumia media kama TV, Magazeti nk.Kwa haya masuala mengine natumia knowledge yangu ya DRC. Kwa jinsi nilivyosikia ni kuwa:

1. Msukumo mkubwa wa Serikali ulikuwa ni dhidi ya M23 kwanza kwani wao ndiyo walikuwa tishio zaidi. Kitendo cha kuanzisha serikali ndani ya serikali kilionekana wazi kuwa ni kibaya na hakiwezi kuvumiliwa.

2. M23 wamenyang'anywa silaha, maeneo, na kuuawa wapiganaji wengi.

3. Mpaka sasa vyombo vya habari vinatangaza kuwa kuna Wanyarwanda wameuawa katika vita hiyo.

4. Mpaka sasa hakuna kiongozi kubwa wa M23 ambaye ameuawa au kukamatwa. Hao viongozi wanatajwa kukimbilia Rwanda na Uganda.
 
FLASH HIDER
Inasemamwa JE KUNA UKWELI HAPO?
"JWTZ wakongo wanasema binduki ya Tanzania iko nguvu kabisa ukiishikia unayua hii niyakutanzania iko natofauti ya Zimbabwe, masasi yake iko kabambe hongera MUNUSCO ikiongozwa na majemedali toka Tz "
 
Last edited by a moderator:
FLASH HIDER
Vipi kuhusu hili ?
"[h=5]RAIS KABILA ANALIHUTUBIA TAIFA MDA HUU KUPITIA TV YA TAIFA NA KUONYA KUWA
MAKUNDI YA WAASI YA FDLR NA ADF/NALU KUWEKA SILAHA CHINI AMA LA WATAKABILI NGUVU ZA KIJENSHI NA KUNYANG'ANYWA KWA NGUVU SIALAHA."
[/h]
 
Last edited by a moderator:
Hiyo vita vijana wa JWTZ wanaimaliza sasa.

Tafadhalini vijana wetu msije mkanogewa mkawafukuza hadi Kampala mkaleta mtafuruku wa kidiplomasia lol
 
Mkuu Babtutu,

Huyu jamaa MUKAMASIMBA niliamua kutokuendelea kubishana nae kwani niligundua hajui anasema nini. Good analysis about him, Tutsi, Hutu , and Rwanda problems.

QUOTE=babtutu;7695996]Bado nasema MUKAMASIMBA hajielewi, ukiongea uwongo unatakiwa uwe unakumbuka vizuri.
MUKAMASIMBA anamaanisha kwamba M23 wamepelekwa na Kagame kule DRC ili kupambana na FDLR ili wawazuie wasije wakarudi Rwanda(wawa-disturb FDLR).
Kwa upande mwingine MUKAMASIMBA anasema b4 mipaka haijagawanywa na wazungu watu walikuwa wana-move tu ndiyo watutsi wakawa wameenda Kivu mipaka ilivyogawanywa wakawa wako huko kivu, (wahutu hawakwendaga Kivu b4 mipaka haijagawanywa) Sasa kama watutsi wa DRC wako huko Kivu wanaleta fujo hukko nyie Rwanda (tutsi MUKAMASIMBA) inawahusu nini kama hao huko DRC (M23)wakipigwa tu kwa sababu wanaleta fujo, wanauwa watu, wanabaka watoto/wamama, uwizi wa madini, uwizi wa mali za innocent civillians??
Au unamaanisha Jaluo wa Kenya akifanya uvunjifu wa sheria/amani huko Kenya then Akapigwa TU ina maana Jaluo wa TZ na Serikali yake waende huko Kenya wakawasaidie wajaluo wenzao kwa sababu wajaluo wanapigwa huko Kenya??

Hawa watutsi waliohamia Uganda, Kenya, Kigoma/Kagera TZ, Burundi mbona hawaleti fujo/vita?? Mbona Hakuna M23 huko??
Au kwanini huwaongelei hao???

M23 ni wanyarwanda raia hai wa Rwanda tena watutsi waliovamia DRC kwa ajili ya KUIBA Diamond na rasilimali nyingine kwa manufaa ya Rwanda.
Rwanda ina Rasilimali gani mpaka sasa inayojulikana??

MUKAMASIMBA wewe ni Al Saif wa Kagame na nadhani unakesha kwenye jf kumtetea Kagame tatizo ni kwamba unachanganyikiwa hujui hata uliandika nini b4 au hii ID ya MUKAMASIMBA inatumika na more than 1 user.[/QUOTE]
 
Ni kweli kaka, tena usikiliza BBC Kiwahili leo jioni, Kabila atahojiwa na kutoa maelezo kuhusu hili.Hilo linawezekana kabisa, unajua M23 ndiyo ilikuwa hatari zaidi kutokana na support iliyokuwa inapata.

FLASH HIDER
Vipi kuhusu hili ?
"RAIS KABILA ANALIHUTUBIA TAIFA MDA HUU KUPITIA TV YA TAIFA NA KUONYA KUWA
MAKUNDI YA WAASI YA FDLR NA ADF/NALU KUWEKA SILAHA CHINI AMA LA WATAKABILI NGUVU ZA KIJENSHI NA KUNYANG'ANYWA KWA NGUVU SIALAHA."
 
Sijajua ukweli wa hili ingawa ukweli JWTZ linasifiwa sana hapa DRC. Sijui huko front mambo yakoje, maana hao JWTZ tokea waondoke hapa kwenda huko hawajarudi..

FLASH HIDER
Inasemamwa JE KUNA UKWELI HAPO?
"JWTZ wakongo wanasema binduki ya Tanzania iko nguvu kabisa ukiishikia unayua hii niyakutanzania iko natofauti ya Zimbabwe, masasi yake iko kabambe hongera MUNUSCO ikiongozwa na majemedali toka Tz "
 
JAMAA MBISHI taratibu kaka, maneno yako ni makali ingawa yana ukweli ambao huenda watu wa aina ya MUKAMASIMBA wasingependa kuyasikia.

Don't be a fanatic for nothing. Kumbuka hata Rwanda ya kina Habyarimana iliongozwa vizuri tu kabla ya PK kuanzisha cold war, unakumbuka hii? PK baada ya kuingia Rwanda amejaribu kuzima ukweli kwa kuua watu (generals na viongozi wengine) waliomkimbia, unataka kutuambia kuwa hii wewe hujuwi na kama hujuwi sasa kwanini unabisha ama kukataa ukweli, si ni ujinga huo? PK is a blatant killer, his time is coming though because God will never let him live long enough before fate will follow him. Jiulizeni, whatever happened to Hitler, Iddi Amini, Mobutu, Sadam Hussein, Samuel Doe, Taylor, Gaddafi?
 
Mkuu Cheze nakubaliana na wewe kwa 100%. Hata sisi, masoko yetu wakati mwingine ni kwa Walebanese na Waisrael ambao huwa wahawezi kwenda field kwa kuogopa risks na kubaki mijini. Wachina ndo sawa na wachinga, hawaogopi lolote, popote pale tena porini, utakutana nao. Nashukuru kwa lesson hii. You have added something to me.

Madini ya Coltan yametajwa kuleta hali ya sintofahamu.Haya madini yanatumika kutengeneza CPU ya simu na lama unavyojua technology ya mawasiliano inavyokuwa ndivyo haya madini huitaji wake inavyoongezeka,coltan IPO CONGO kwa kiwango kikubwa sana zaidi kivu ya kaskazini.Mataifa kama USA na China wamekuwa wa watumia business elites wakibeligium kukusanya madini Congo, kunareport ya UN imewataja hao watu..hayo madini yanasafirishwa kwa ndege Tokay Congo hadi Mombasa then to China ambapo kunacheap labor of man power.Kampuni za simu tajwa ni Motorola na Nokia, so fedha inaenda master planners then inarudi kufadhili rebels Congo na associate just kufanya Congo isisettle ili wao wandelee kuchuma.So kama unadeal na madini Congo no blood miniral..hii deal Israel pia wamo ndo wanunuzi wakubwa humo...wachimbaji ni wacongo wenyewe..mamiddle men ndo nyiye...tafuta blood coltan' IPO YouTube.
As long as economic is concerned Congo won't settle hao kina Pk .nkunda.m7.etc wanatumika na visababu vya hapa na pale.Chezea midini.mafuta na gesi.
tchao.
 
Mh! big lesson. Tusipoelewa hapa, basi hatutaelewa tena. Ila ninachojua mimi PK lazima ataendelea kuleta chochoko ndani ya DRC. Distabilisation ya DRC inamnufaisha yeye kwa ku-exploit mali ya ndugu zetu wa DRC.

Back
Top Bottom