Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Hapana sijapotea wala sitegemei kupotea, ukweli ninasimamia yale ninayoyaamini ni ya ukweli kwa HOJA. Hapa usinielewe vibaya, hoja ya MUKAMASIMBA ni kuwa M23 walikuwa wanawalinda Watusi hapa DRC (GOMA). Nikamweleza kuwa hata hao watusi waliporwa na kunyanyaswa na M23 mwaka jana. Tena hawataki kusikia kitu kinachoitwa M23 hapa GOMA. Juzi wamechanga karibu dola 16,000 kusaidia jeshi kupambana na M23. Wangechanga vipi kusaidia kuuawa kwa walinzi wao? Ndiyo maana nimeweka angalizo kuwa tuone sasa nani atawalinda hao Watusi wa GOMA baada ya M23?. Sijabadirika kaka.

Mkuu naona ulianza vizuri ukionekana kama hujaegamia upande wowote ila kadri muda unavyoenda unaonekana kuwa umeagamia upande mmoja. Umepotelea wapi?
 
Hawa watusi wanapokea msaada kutoka Rwanda na Uganda, eti sasa mazungumzo ya kuleta amani hufanyika Kampala chini ya usimamizi wa Kaguta Museveni! Ni kichekesho.
 
Mkuu ni kweli huwa mnanunua madini kinyemela kutoka kwa majeshi ya MONUSCO?
 
Baada ya kutokea mgawanyiko ndani ya M23 mwezi May mwaka huu, ilitokea vita kubwa baina ya wafuasi wa Makenga na Ntaganda (chanzo cha ugomvi nitakielza baadae). Upande wa Ntaganda walipigwa katika vita hiyo. Ntaganda na wafuasi wake (pamoja na rais wa M23 wa wakati huo Mchungaji Runiga) walimbilia Rwanda. Huko Ntaganda alijisamilisha Ubalozi wa Marekani nchin Rwanda na sasa anasubiri kesi Mahakama ya ICC. Hao wengine wanaishi kama wakimbizi kwenye kambi moja hapo Rwanda.

Mkuu hawa watu wapo wapi Generali Nkundabatware na Askofu Jean-Marie Runiga Lugero, Generali Makenga
 
Baada ya kutokea mgawanyiko ndani ya M23 mwezi May mwaka huu, ilitokea vita kubwa baina ya wafuasi wa Makenga na Ntaganda (chanzo cha ugomvi nitakielza baadae). Upande wa Ntaganda walipigwa katika vita hiyo. Ntaganda na wafuasi wake (pamoja na rais wa M23 wa wakati huo Mchungaji Runiga) walimbilia Rwanda. Huko Ntaganda alijisamilisha Ubalozi wa Marekani nchin Rwanda na sasa anasubiri kesi Mahakama ya ICC. Hao wengine wanaishi kama wakimbizi kwenye kambi moja hapo Rwanda. Nilisahu, Nkunda alikamatwa mwaka 2009 na sasa yupo under house arrest huko RWANDA. Makenga mpaka sasa hajulikani alipoila inadaiwa amevuka mpka kuingia Rwanda au Uganda.[/QUOTE]
 
Kama nia yao haikuwa M23, kumbe bado wanasababu mkononi ya kuendelezea nia yao. Maana, kama kweli nia yao sio m23 wata demand serikali ziwakamate hao m23, kama hawakamati basi watafuatwa. Kama marekani alivyomfuata Osama afghan. Kama UN wanasababu nyingine bado wana option nyingi mkononi.## #HIZO SERIKALI WALIZOKIMBILIA HAZINA BUDI KUTOA MAELEZO YA KINA NA KWANINI ZISICHUKULIWE HATU KIMATAIFA,WALITAKIWA WAWAKAMATE NA SHERIA ICHUKUWE MKONDO WAKE KWANI WAMESABABISHA UMWAGAJI MKUBWA WA DAMU ZA WAKONGOMANI +MASS GRAVES ZILiZOKUTWA KIWADJA
 
MONUSCO hawachimbi madini. Nimekaa GOMA kwa miaka zaidi ya 12, sijaliona hili.
Mkuu sijakuambia MONUSCO wanachimba madini.

Kuna habari kila siku tunasoma kuwa MONUSCO kazi yao ni kupora madini na kuuza ughaibuni na wala siyo kuwalinda raia Congo.
 
Kuanzia terehe 25 Oktoba mapigano mapya yameanza ambapo mpaka mchana huu taarifa zilizopo ni kuwa M23 wamekimbia maeneo yote na sasa wanaelekea BUNAGANA jirani kabisa na mpaka wa Uganda. Wananchi wanashangilia sana. Ujue hapa GOMA wananchi wamechoshwa sana na M23 kila siku tunafunga maduka na kukimbia huku na huku. Saa hizi ni shangwe tupu, waendesha pikipiki wote wapo barabarani. Jana walifanya kitu ambacho hata mimi kilinigusa. Kila mwenye pikipiki (Boda boda) alinunua maji chupa moja (lita moja) na wote kwa pamoja walienda mpaka eneo la Kanyaruchina ambako majeshi ya Serikali yalikuwepo na kuwapatia maji hayo kama ishara ya kuwaunga mkono.

ni jambo jema unapogundua kuwa kuna majirani wanaokuhitaji na kuthamini mchango wako, wakati wengine wakitaka kukufanya ujidharau na kujiona si chochote si lolote. Serikari iharakishe kuundwa kwa umoja mpya wa Tz, Burundi na DRC
 
[h=1]Kabila anyoosha mkono wa diplomasia[/h] Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewataka wapiganaji wa makundi yote ya waasi mashariki mwa nchi yake kuweka silaha zao chini, baada ya kile kinachoaminika kuwa ni kusambaratika kwa kundi la M23.

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.



Akihutibia taifa hapo jana (tarehe 30 Oktoba) kwa njia ya redio na televisheni, mara tu baada ya jeshi la serikali kuuteka mji wa Bunagana, Rais Kabila alilipongeza jeshi hilo na wale Umoja wa Mataifa kwa kulirejesha eneo la Rutshuru mikononi mwa serikali.


Hata hivyo, Rais Kabila akasema pamoja na ushindi huo wa kijeshi, diplomasia na mazungumzo baina ya Wakongomani yataendelea.


"Ninasisitiza wito wangu kwa wapiganaji wa kundi lililofurushwa kwenye mitaa ya Nyiragongo na Rutshuru kutua silaha zao chini kwa ikhari yao wenyewe kulingana na pendekezo la Nchi za Maziwa Makuu. Kinyume cha kufanya hivyo tutalazimika kuwapokonya silaha kwa nguvu. Wito wa aina hiyo hiyo unatolewa pia kwa makundi mengine ya wapiganaji ya kitaifa, kusitisha hatua zote za kijeshi kutasababisha wao na wengine kufaidika na mpango wa kuingizwa katika maisha ya kawaida." Amesema Rais Kabila.


Kabila azionya nchi jirani, makundi ya kigeni
Wanajeshi wa Kongo wakipumzika baada ya vita vya kuwafurusha M23 mashariki mwa nchi hiyo.


Katika hotuba hiyo ya kwanza tangu taarifa za kusambaratika kwa kundi la waasi wa M23 mashariki kwa nchi hiyo, Rais Kabila aliyatahadharisha pia makundi ya wapiganaji ya kigeni yalioko nchini huko Kivu.


"Kuhusu makundi yaliosalia ya kigeni yakiwemo FDLR, LRA, ADF/Nalu na FNL yanayoendelea kutaabisha wakaazi wa Kivu ya Kusini na Kivu ya Kaskazini, ninayatahadharisha kutua chini silaha haraka sana. Vyenginevyo, makundi hayo yatapokonywa silaha kwa nguvu na yatachukuliwa hatua kama tunayoendesha hivi sasa."


Katika hatua nyengine, Rais Kabila ametumia hotuba hiyo kuzionya nchi jirani,ambayo hakuzitaja jina, kwamba amani ya kudumu ya Kanda la Maziwa Makuu itatokana na utekelezwaji wa Mkataba wa amani wa Addis Ababa.


"Kwan nchi jirani, ninaziambia mara nyingine kwamba njia muafaka ya kuleta amani na ustawi wa ukanda huu, ni utekelezwaji wa dhati na kwa nia nzuri kwa Mkataba wa Amani wa Addis Ababa na vile vile Azimio Namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ninawahimiza kutekeleza wajibu wao kulingana na mkataba huo."


Anyoosha mkono wa diplomasia
Wanajeshi wa Kongo wakifurahia ushindi dhidi ya M23.
Rais Kabila amesema ijapokuwa ushindi wa kijeshi umepatikana, lakini juhudi za kidiplomasia na kisiasa zitaendelea.
"Mtizamo wetu ni ule wa kutafuta suluhisho la mzozo wa Kongo kwa njia tatu: ya kijeshi, ya kisiasa na kidiplomasia. Na ndilo tunalofanya sasa. Ushindi wa kijeshi huko Kivu hauwezi kuvunja juhudi zingine za kisiasa na kidiplomasia."
Kufuatia ushindi wa jeshi la Kongo dhidi ya waasi wa M23, Rais Kabila aliwapongeza wanajeshi na kusema wameungwa mkono na taifa nzima.


Vile vile, aliwapongeza wanajeshi wa Tanzania katika kazi wanayoifanya kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa na kutoa heshima zake na rambirambi za pole kwa familia ya wanajeshi wa Kongo na wale wa Tanzania waliopoteza maisha yao kwenye uwanja wa mapambano.
Rais Kabila alitoa wito wa kutokueko na ulipizaji kisasi baina ya Wakongomani.


Mwandishi: Saleh Mwanamilongo/DW Kinshasa
Mhariri: Mohammed Khelef


[h=4]DW.DE[/h]
 
Wewe kaa kimya hujui historia ya Congo, udini upo wapi?

Rais wa kundi la CNDP alikuwa akiitwa Askofu Jean-Marie Runiga Lugerero.

Wewe jamaa usijifanye kujua sana hapa...kuna watu wanajua kukuzidi wewe....Mbona FLASH HIDER anajua mengi na hajigambi...Usituletee mambo ya Ki CCM hapa
 
Last edited by a moderator:
MONUSCO hawachimbi madini. Nimekaa GOMA kwa miaka zaidi ya 12, sijaliona hili.

KINSHASA, Oct 30, 2013 (BERNAMA-NNN-SA NEWS) --

South Africa and the Democratic Republic of Congo (DRC) have signed a treaty for the construction of the 40,000-MW Grand Inga Hydro-electric Power Project on the Congo River, which is expected to become the biggest in the world, generating enough electricity to power half of Africa's needs.

The treaty also included provisions paving the way for South African utility Eskom and DRC utility Societe Nationale d'Electricite to enter into an agreement to facilitate execution of the project.
President Jacob Zuma, who made the announcement while addressing the Parliament of the DRC in Kinshasa Tuesday Oct 29, 2013, said the treaty was a major step towards the realisation of the long cherished dream of the people of the DRC.

"It is with great pleasure that an important treaty on the Grand Inga Hydro-power Project has been signed this morning. This long talked about project has got the potential to change the economic prospects of the DRC, the region and the continent," said Zuma, who is on an official visit to the DRC.



Ayaa sasa FLASH HIDER upo apooo!

Hii ni break newz! imetoka jana tuu kwenye vyombo mbali mbali vya habari,

Project hii ya Grand Inga Hydro-electric ina ya thamani ya $120 billion, Kimsingi wa South Africa hawatatoa cash ila walipeleka scope yao ya hii project World Bank kwa ajili ya mkopo, WB ika kubali kutoa mkopo kwa South Africa ili iweze kuendesha mradi huu kwa masharti ya kusimamia ulinzi na ?political stability kwa DRC ktk mpango mzima wa kutengeneza faida na kunusuru mihela ya WB na ndani ya miaka 20 wanatakiwa wawe wamerudisha mkopo na riba, hii project inatakiwa kuanza rasmi mwaka 2015!

Sasa ukiangalia vizuri hii si biashara bali ni 'wizi' wa mchana mchana yaani wa South Africa wamsaidie na kumlinda kabila ili aendelee kukaa madarakani huku wao wakijilipa sehemu kubwa ya returns & profits za Grand Inga Hydro-electric Power Project. All in all WB inasema project hii itanyanyua uchumi na maisha ya wacongoman kwa kiasi kikubwa!
Na sisi wa TZ sijui tumepata nini zaidi ya vi allowance vidogo vidogo vya MONUSCO kutoka UN, huku wajanja wakimsainisha kabila mikata ya kilaghai na kuchukua chao mapema wakati vijana wetu wa JWTZ wakitandikwa risasi kila siku wakirudishwa kwenye masunduku.
 
FLASH HIDER
Unazungumnziaje hili?
"[h=5] bali tulie kwenda sisi wote katika milima, bila kufanya vita, kwa sasa tuna patikana, Katika sehemu za Virunga, huko Cyanzu, Jomba, Runyoni, Bweza, kasebeya, na Ntamugenga. Kule tuliko anziya tukiwa 300. leo tuko maelfu na silaha kali kali."[/h]
 
Last edited by a moderator:
maajabu, wauaji m 23 wakitwangwa watu wanakana asili yao, tukiingia rwanda si watakubali kuolewa bila shuruti? viva JWTZ

Acha upuuzi wewe,hunakifua cha kuingia rwanda,huwezi hata kuingi 1cm kama huja toweka duniani.
 
Wewe jamaa usijifanye kujua sana hapa...kuna watu wanajua kukuzidi wewe....Mbona FLASH HIDER anajua mengi na hajigambi...Usituletee mambo ya Ki CCM hapa
Mimi sijui chochote nipo hapa kujifunza, hayo mengine ni yako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom