Uliza swali lolote juu ya afya ya ngozi

Uliza swali lolote juu ya afya ya ngozi

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
AINA ZA NGOZI.
Kuna aina nne za ngozi ya binadamu:

1.Ngozi ya kawaida (normal skin)
Hii ni ngozi ambayo ina mafuta na unyevu wa kawaida kwa ajili ya ustawi mzuri wa ngozi,hivyo huwa ni ngozi isiyo na mikunjo ya aina yeyote na huonekana vizuri. Pia ni ngozi ambayo ni vigumu kuwa na chunusi na matatizo mengine ambayo yanapatikana katika aina nyingine za ngozi. Kwa hiyo ni ngozi inayohitaji matunzo ya kawaida kama vile, kuisafisha na kuipatia unyevu wa kawaida kabisa(moisture).

2. Ngozi kavu(dry skin)
Ni ngozi ambayo ni rahisi kujikunja(wrinkles) na hivyo kuzeeka haraka na hii hutokana na kiasi kidogo cha mafuta kinachotengenezwa katika mwili. Hii ni ngozi ambayo haiendani na mazingira ya baridi kwani huwa kavu sana. Hii ni ngozi ambayo inahitaji unyevu(moisture) kwa wingi,kwa hiyo ni vyema kutumia vipodozi ambavyo vina unyevu mwingi mchana na usiku unapolala ili kuzuia mikunjo(wrinkles) na muonekano wa kuzeka kwa ngozi.

3. Ngozi yenye mafuta(oil skin)
Hii ni aina ya ngozi yenye mafuta mengi na hivyo kupelekea mtu kung’aa na hivyo kukosa mvuto. Pia ni ngozi ambayo ina uwezo wa kushika uchafu kama vumbi kutoka kwenye mazingira na hivyo kuonekana ni chafu.
Pia ni ngozi ambayo ni rahisi kuwa na chunusi kutokana na hayo mafuta pamoja na sababu zingine,hivyo inahitaji matunzo mazuri na ya kila siku ili kupunguza au kuondoa matatizo yanayoambatana na aina hii ya ngozi. Watu wenye ngozi ya aina hii wanatakiwa wawe na mtindo mzuri wa kimaisha ikiwa ni pamoja na vyakula wanavyokula,hali ya usafi na kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yao, ambapo vitu vyote vikifanyika kwa usahihi vitafanya ngozi iwe ni nzuri na yenye mvuto.
Kitu kizuri kwa watu wenye ngozi yenye mafuta ni kwamba ngozi zao hazipati mikunjo(wrinkles) na hivyo ngozi zao hazizeeki mapema.

4. Ngozi ya mchanganyiko(combination skin)
Hii ni ngozi ambayo ina sehemu ambazo zina mafuta na sehemu nyingine ambazo ni kavu, hivyo ni mchanganyiko wa ngozi yenye mafuta na ngozi kavu au ngozi ya kawaida.

Mara nyingi sehemu za uso kama vile paji la uso,kwenye pua na kwenye kidevu kunakuwa na mafuta mengi, wakati sehemu za shavuni na maeneo yote kuzunguka mdomo na macho huwa ni kavu.

Hapa unatakiwa utunze hizo sehemu za ngozi kutokana na aina yake,kama hiyo sehemu ina mafuta, tunza kama ngozi yenye mafuta,pia tumia njia za kutunza ngozi kavu sehemu ambapo kuna ngozi kavu.

JINSI YA KUWEZA KUITAMBUA NGOZI YAKO NI YA AINA GANI

Ni vizuri sana kwako kuweza kujua aina ya ngozi yako maana itasidia wewe uweze kuitunza ngozi yako vizuri.Vile vile itakusaidi katika kujua ni vipozi vya aina gani utumie kutokana na ngozi yako. Hakuna ngozi mbili ambazo zinafanana exactly ila zinatofautiana ambapo inawezekana ngozi yako ikawa ni Ngozi Kavu, Ngozi ya Kawaida, Ngozi ya mafuta na ngozi mchanganyiko yaani combine skin.

uso 1.JPG

Ili kujua ngozi yako ni ya aina gani osha uso wako kwa kutumia sabuni ya kusafishia uso then baada ya dakika 30 chukua tishu na futa sehemu ya paji lako la uso, kwenye pua, kidevu na mashavu.

Kama tishu hiyo haitaonyesha kuwana mafuta baada ya kufuta basi ngozi yako itakua ni aina ya ngozi kavu.

uso 2.JPG

Ngozi kavu huwa inaonekana rough na hukabiliwana mistari na wrinkles lakini kama ngozi yako kuna sehemu nyingine inakua kavu sehemu nyingine inakua na mafuta basi ngozi yako itakua ni ngozi mchanganyiko.

uso 3.JPG

Ngozi ya kawaida au Normal skin huwa inaonekana laini na ngozi hii ya mafuta ukiigusa unayahisi mafuta na huwa inang`aa. Ngozi hii ya mafuta huwa inakabiliwa sana na blackheads na pimples/chunusi na kwa kuwa ngozi hii ni sensitive inahitaji special care na umakini na vipodozi unavyopaka kwenye uso wako.

uso 4.JPG

Kwa watu wenye ngozi sensitive kama hii ni lazima kutumia misaada ya ushauri kwa wataalamu wa ngozi ili kulinda ngozi zao kupata mzio/allergic. Ni lazima mara kwa mara uwe na utaratibu maalum wa kuihudumia ngozi yako kulingana na mahitaji ya ngozi yako na huenda ikachukua muda mrefu kwa ngozi yako kurudia hali ya kawaida kuweza kuondokana na hili tatizo.

Kwa ushauri BURE juu ya afya ya ngozi yake, wasiliana nami

0713 03 98 75
Dr. Mussa Zaganza
Mtaalamu wa Afya ya Ngozi Na Nywele
Natural Skin Solution
 
UPDATES:
Tumefanikiwa kuja na natural clay na sabuni yake kwa ajili ya tiba ya magonjwa yote ya ngozi.
Jinsi natural clay inavyofanya kazi:

Clay inapochanganywa na maji,inatengeneza mikondo midogo midogo ya umeme,ambayo ukipaka kwenye ngozi ,inaenda kumpiga shoti bacteria au fungus anayeshambulia eneo hilo la ngozi.

Hivyo unapopaka tu,utaanza hisi ubaridi ikiwa ni ishara bacteria wanaanza pungua.Ukirudia wiki hadi mwezi,tatizo lako humalizika.Kwa ushauri wa bure au mahitaji ya dawa,piga: 0713-039875
 
Ngozi ya uume kuwa na mabaka baka kama mmba nini tatizo na dawa yake ni nini??
Hizo ni fungus. Fanya yafuatayo:
1. Kunyoa muda wote
2. Kukausha vizuri kwa taulo baada ya kuoga
3.Pia hakikisha unavaa nguo safi na kavu ukibadilisha chupi kila siku pia uhakikishe kabla ya kuvaa nguo umekausha sehemu hizo nyeti. Zingatia kupasafisha vizuri, ondoa mapovu ya sabuni na kausha vizuri pia.
4.Zikiendelea tuwasiliane kwa maelekezo ya dawa
 
dawa ya kuondoa mabaka yaliyo kutokana na chunusi ni ipi?
TIPS ZA KUONDOA WEUSI WA MAKALIO, MAPAJA NA USO
3.GANDA LA CHUNGWA NA ASALI AU NATURAL CLAY

Kama mnavyojua machungwa yana vitamin C, na hivyo ukichukua ganda la chungwa pamoja na asali, mchanganyiko wake pia unaondoa weusi. Fuata step hizi::
Chukua ganda la chungwa na kijiko kimoja cha asali.
Kamua hilo ganda maji yake yangie kwenye asali.
Kausha nakusaga hilo ganda kisha poda yake ichanganye na asali
Paka mchanganyiko huo katika sehemu yenye weusi, kaa kwa muda wa dakika 15
Osha na maji ya kawaida hadi kugandaganda kupotee.
Kama huna muda wa kuandaa mchanganyiko huu tuwasiliane, nikupe natural clay
 
Shukrani,,,mafuta ya Nazi ni mazuri kwa ngozi?
faida zake ni zipi?
 
Nina shida kubwa ya kuwashwa mwili hasa mgongoni baada ya kuoga, ni tatizo la miaka mingi zaidi ya 20, hata jirudie kujipaka sabuni mara ngapi haisaidii.
 
Je ngozi kuwa na vipele vingi kama vya joto tatizo nini na natakiwa kufanya nn
Hivyo ni vipele vinatokana na joto.Jitahidi kubadilisha mazingira ya nyumbani. Hapa nina maana chumba unacholala kiwe na singboard zuri, madirisha makubwa ambayo hayana top, na ikiwezakana umuwekee na feni.

Kwa sababu mara nyingi joto linaloumiza sana ni lile la usiku kitandani. Na tena hakikisha kama ni muhimu kujifunika shuka usiku basi ajifunike shuka nyepesi ya pamba. Na mchana avae nguo nyepesi za pamba
 
Shukrani,,,mafuta ya Nazi ni mazuri kwa ngozi?
faida zake ni zipi?
Mafuta ya nazi ni borakama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji . MUHIMU: Mafuta ya nazi huongeza joto,yanafaa zaidi mazingira ya baridi
 
Nina shida kubwa ya kuwashwa mwili hasa mgongoni baada ya kuoga, ni tatizo la miaka mingi zaidi ya 20, hata jirudie kujipaka sabuni mara ngapi haisaidii.
Moja ya matatizo ya kiafya yanayowasumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha baada ya kuoga.

Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu za mwili. Pia, hali hii inaweza kuendelea kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu hili linaweza kuwa tatizo sugu.

Ingawa tatizo hili la kiafya ni kama matatizo mengine, lakini baadhi ya watu kwa kukosa taarifa sahihi hulihusisha na imani potofu. Ukweli wa mambo ni kwamba kuna sababu nyingi zinazochochea kutokea kwa tatizo hili na baadhi hazina madhara makubwa lakini sababu zingine zinaweza kuwa hatarishi kwa maisha.

Miongoni mwa sababu za kutokea kwa muwasho wa mwili baada ya kuoga ni za kimazingira na sababu zingine zinahusiana na hitilafu za urithi wa vinasaba vya kijenetiki katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika.

Wakati mwingine tatizo hili linaweza kuwa dalili muhimu inayoonyesha baadhi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kama vile matatizo ya figo, ini, tezishingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani ya mitoki na msongo wa mawazo.

Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu za kimazingira ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku na mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuuwa wadudu waharibifu, mabaki ya wadudu, mavumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini.

Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho, pindi mwili unapopata msisimko, hali ambayo hujulikana kama mzio.
MUHIMU: Kapime vipimo hivyo kisha tuwasiliane
 
Chunusi za mgongoni husababishwa na nini?na tiba yake nini?
 
Nashukuru sana mkuu.
 
Dawa ya kuondoa michirizi na harahara kwenye uso wenye mafuta mengi
Chanzo cha tatizo

Ngozi ya binadamu ina matabaka matatu yaani tabaka la juu, tabaka la kati na tabaka la chini. Michirizi ya ngozi huanzia katika tabaka la kati ambalo kimsingi ndilo linaloipatia ngozi uimara na uwezo wa kuvutika. Sehemu hii ya ngozi inapovutika kupita kiasi ndani ya kipindi kifupi na ikaendelea kuwa katika hali hiyo, ngozi huvimba na kusababisha kuchanika kwa nyuzi za ngozi ziitwazo collagen. Hali hii pia husababisha upungufu wa elastin na fibronectin, vitu ambavyo huifanya ngozi kuwa imara na kuvutika kwa urahisi.

Hali hii kwa wanawake hujitokeza zaidi wakati wa ujauzito kiasi kwamba asilimia 90 ya wanawake wajawazito hupata tatizo hili kwa ukubwa unaotofautiana

Jinsi ya kukabiliana nalo

Njia ya kwanza ya kukabiliana na tatizo hili ni kuzingatia kanuni bora za lishe pamoja na kunywa maji ya kutosha kila siku. Ni vizuri kula chakula chenye madini ya kutosha ya zinc na aina mbalimbali za vitamini ili kuimarisha afya ya ngozi.

Njia nyingine inayosaidia kukabiliana na tatizo hili ni kuchua misuli mara kwa mara ili kuongeza kiasi cha damu. Utafiti uliofanyika nchini Uturuki mwaka 2012 unaonyesha kuwa wanawake wanaochua misuli kwa angalau dakika 15 kwa kutumia mafuta ya mlozi wanapunguza uwezekano wa kupata michirizi ya ngozi.
Tuwasiliane kama tatizo linaendelea

Utafiti mwingine uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba, Tehran huko Iran nao ulionesha kuwa kuchua misuli kwa mafuta ya mizeituni wakati wa ujauzito, hupunguza uwezekano wa kupata michirizi ya ngozi.
 
Ngozi kuwa kama inababuka sehemu za siri specually kwenye ngozi ya korodani nini tatzo na matibabu yake pia na tufanyeje ili kuepuka
 
Ngozi ya mafuta nitumie aina gani ya mafuta/lotion ili I we vizuri
 
Boss unaijua benzoyl peroxide kama dawa ya kusaidia kuondoa chunusi?? Unaiamni vp kwa ufanisis wake wa kaz?
 
Back
Top Bottom