Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,414
- 2,181
- Thread starter
- #41
Punye ni ugonjwa wa ngozi au n nin!?
Mapunye au Tinea Capitis ni nini?
Aina hii ya maradhi ya fangasi hushambulia eneo la kichwa pekee ukiacha eneo la uso. Kwa maneno mengine, aina hii ya fangasi haishambulii uso bali hushambulia eneo lililobaki la kichwa.
Huwashambulia kina nani?
Haya hushambulia watu wote wa jinsia na umri wote, ingawa huonekana zaidi kwa watoto wadogo. Fangasi hawa hushambulia watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe na mara nyingi huacha kushambulia pale mtoto anapofikia umri huo wa balehe.
Mwonekano wake
Mapunye huweza kushambulia eneo lote la kichwa au sehemu tu ya kichwa. Eneo la ngozi ambalo lina mashambulizi ya mapunye huwa na umbo linalofanana na sarafu.
Eneo hili la ngozi lililoathirika kama lina nywele, basi hunyonyoka na hivyo mwonekano wa mfano wa sarafu huonekana vizuri tu hata bila kutumia jicho la kitaalam.
Dalili zake
Ukiachilia mbali mwonekano wa mapunye kama nilivyoeleza hapo juu kuna dalili nyingine za maradhi haya. Hizo ni:
-Eneo la ngozi lililoshambuliwa kuwasha (ingawa si mara zote)
-Kubadilika kwa rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi
-Ukitazama kwa makini eneo ambalo lina mashambulizi ya maradhi haya utagundua kuna vidoti vyeusi ambavyo vinaonyesha eneo ambalo nywele imeng`oka kutokana na maradhi.
-Ngozi kubanduka kwenye eneo lenye maambukizi
-Ngozi kukauka kwenye eneo lenye maambukizi
-Mara nyingine usaha pia huweza kuonekana kwenye eneo la ngozi lililoshambuliwa na fangasi hawa (hii kwa kitaalam huitwa kerions)
-Kama maradhi haya yakikaa bila kutibiwa kwa muda mrefu husababisha dalili nyingine kuonekana kama kutoka kwa maji maji kwenye eneo la ngozi lililoathirika pamoja na kutoka kwa harufu mbaya kwenye eneo la ngozi lililoathiriwa na vimelea hivi vya fangasi.
Jaribu hizi dawa moja kati ya hizo Dawa tatu hapo chini:
(1) Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga Msuguwe limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.
(2) (Fenugreek) kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu. Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.
(3) Mshubiri Mwitu au Aloe Vera kwa jina lingine. Ponda paka kichwani kila siku mara mbili asubuhi na usiku.
(4) Pia kuna udongo tuliouvumbua hivi karibuni wa Natural clay.
Tumia Dawa mojawapo sio zote tafadhali kisha utpe feedback.