Uliza swali lolote juu ya afya ya ngozi

Uliza swali lolote juu ya afya ya ngozi

Mimi nimejikita kutibu ngozi kwa njia za Asili tu kuanzia dawa, sabuni,scrub, ukuzaji nywele, kutibu ngozi ilobabuka kwa dawa kama metakelfin au vipodozi. Hivyo tiba kama waxing sina ufahamu nazo
 
Ngozi ya uume kuwa na mabaka baka kama mmba nini tatizo na dawa yake ni nini??
Hahahaaaa
Watanzania bhana
Jamaa Amezugumzia ngozi ya Uso na siyo ngozi ya Mboro/Uume wenye Mabaka Mabaka kama Kenge au Mamba
 
Mkuu zaganza ..nina tatizo la kuwashwa mwili ..hasa wakati wa jua, mwili unakuwa kama una sisimka alafu na hali flani kama ya kuchoma choma hutokea.

Au nikinywa chai au kitu chochote cha moto au mwili ukipata joto tu mf nikiwa natembea haraka na mwili kupata joto basi hiyo hali hunipata.

Kama ni allergy mkuu plizi nisaidie namna ya kuisha.
 
Moja ya matatizo ya kiafya yanayowasumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha baada ya kuoga.

Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu za mwili. Pia, hali hii inaweza kuendelea kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu hili linaweza kuwa tatizo sugu.

Ingawa tatizo hili la kiafya ni kama matatizo mengine, lakini baadhi ya watu kwa kukosa taarifa sahihi hulihusisha na imani potofu. Ukweli wa mambo ni kwamba kuna sababu nyingi zinazochochea kutokea kwa tatizo hili na baadhi hazina madhara makubwa lakini sababu zingine zinaweza kuwa hatarishi kwa maisha.

Miongoni mwa sababu za kutokea kwa muwasho wa mwili baada ya kuoga ni za kimazingira na sababu zingine zinahusiana na hitilafu za urithi wa vinasaba vya kijenetiki katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika.

Wakati mwingine tatizo hili linaweza kuwa dalili muhimu inayoonyesha baadhi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kama vile matatizo ya figo, ini, tezishingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani ya mitoki na msongo wa mawazo.

Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu za kimazingira ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku na mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuuwa wadudu waharibifu, mabaki ya wadudu, mavumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini.

Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho, pindi mwili unapopata msisimko, hali ambayo hujulikana kama mzio.
MUHIMU: Kapime vipimo hivyo kisha tuwasiliane
 
Mimi nimejikita kutibu ngozi kwa njia za Asili tu kuanzia dawa, sabuni,scrub, ukuzaji nywele, kutibu ngozi ilobabuka kwa dawa kama metakelfin au vipodozi. Hivyo tiba kama waxing sina ufahamu nazo
Nina ngozi yenye mafuta sana sana usoni. Nina miaka zaidi ya 10 sijapaka mafuta usoni. Lakini jua likiwaka ni kama nimejipaka Vaseline. Ushauri wako ni upi kwa sabuni na vipodozi vya ngozi ya aina hii? Angalizo ni kuwa visiwe vileeee vinavyochubua uso. Sijichubui. Asante
 
Mkuu tatizo la ngozi ya lips ya mdomo kubanduka inasababishwa na nn
 
Wakuu nisaidieni huu ni ugonjwa gani hii alama ina zaidi ya miezi mitano sasa nilienda hospitali nikapewa betamethasone though haijaleta mabadiliko yoyote
Screenshot_20180510-160243.jpg
 
Nasumbuliwa na vidonda kichwan kwenye shina la nywele nimetumia dawa nyingi sana vinapotea na kurudi sometime vinatoa had damu nakuta damu kwenye mto...ni kama vile vipele vidogo vidogo baadae vinaiva vinatoa damu au usaha..!... Vimenisumbua kwa miaka mingi..dawa yake ipo?
 
Nimetokwa na itangotango usoni ila sijikuni je,nitumie dawagani nipone haraka wakati mimi usowangu una mafuta sana
 
Salaam mtaalam wa ngozi. Shida niliyonayo mm huwasha nikioga maji yakaukapo mwilini. Hasa nikijifuta maji ndo nakaribisha muwasho sana ila yakikauka bila kujifuta huwasha kidogo
 
Natokwa na mapele kila baada ya kunyoa ndevu saloon yanayopelekea kuvia usaha. Kuna kinyoz m1 angalau ananiwezea stokagi sana mapele. Shida ni nin hasa kwa tatizo hili?
 
Kibarango hakiponi kipo katikati ya kichwa ni muda dawa nimejaribu antibiotics zote zimegoma
 
Nasumbuliwa na vidonda kichwan kwenye shina la nywele nimetumia dawa nyingi sana vinapotea na kurudi sometime vinatoa had damu nakuta damu kwenye mto...ni kama vile vipele vidogo vidogo baadae vinaiva vinatoa damu au usaha..!... Vimenisumbua kwa miaka mingi..dawa yake ipo?
Una tatizo kama la kwangu ukipata dawa pia njoo pm
 
IMG_20180516_160633.jpg
nitumie dawa gani na je hili linaweza kuwa ni tatizo gani.
 
View attachment 765967 Msaada tafadhari, hvi huuni ugonjwa gani ametembea kila baadhi ya hospitali lakini hapewi majibu ya kueleweka.
Pole kaka.Mi nimejikita kwenye matatizo ya ngozi.Hapo pichani naona kama kidonda, kama hospitali za kawaida ushapitia,nenda Muhimbili, wahi usihatarishe mguu wake ,kwani hauna spea
 
Back
Top Bottom