Kwanza Binti anataka kusoma kitu gani? Au anatamani kufanya nini baadae?
Lakini, kama akitaka kusoma field ya science au engineering, basi inabidi aanzie Certificate maana naona Maths ana F, sijajua kama utaratibu umebadilika.
kwa sasa, ni vizuri kumuuliza anachotaka kusoma ili iwe rahisi kujua hatua zinazofuata, maana kuna fields za kusoma zaidi ya 100 na zinatofautiana vigezo.
Mwambie asijisikie vibaya kwakuwa amepata Four ya 28, kuna njia nyingi sana kupitia NACTE ili kufikia malengo aliyojiwekea, kuna watu wengi makazini walipiga Four za mwisho, ila kupitia certificate na diploma sasa wapo kwenye nafasi za juu serikalini na sehemu binafsi.