Msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop Golden Mbunda maarufu Godzilla baada ya kufariki ndipo wengi watamfahamu na kutaja sifa zake.
Ni tabia ya 'kipuuzi' iliyozoeleka Mara mtu anapofariki ndipo tunakumbuka umuhimu na mchango wake katika nyanja inayomuhusu na wengine wana kwenda mbali na kuthubutu kupokea michango ya rambirambi kwa ajili ya manufaa yao binafsi, hii ni aibu isiyo na kifani!
Nimeona katika mitandao mbalimbali watu wame-publish video clip za interview na michano ya Godzilla wakiwa na maana ya kukumbuka, kutambua na kuthamini kazi na mchango wake katika muziki, na hii imetokea baada ya Kifo chake!
Hoja yangu ni kuwa kwa nini mambo Haya yasifanyike angali mtu akiwa hai, kwani kwa jinsi inavyofanyika sasa haiwezi kumnufaisha kwa jinsi yoyote,,,,,Tunaweza kujifunza!!!!
Sent using
Jamii Forums mobile app