Umagufuli bila Magufuli unahitajika nchi hii ili iweze kupiga hatua mbele za maendeleo.
Hivi ni nini kizuri cha pekee ambacho amefanya Hayati Magufuli ambacho watangulizi wake hawakufanya?
Katika kuipeleka nchi mbele, hakika Mwalimu ni wa kwanza. Wa pili ni Mkapa, ndiye aliyeweka mifumo mingi inayoendesha mambo mengi sasa. Na wa tatu ni Kikwete, huyu alijenga miundombinu mingi kwa kiasi ambacho utawala wa marehemu Magufuli haujafikia hata 25%.
Kipya kabisa alichokifanya Magufuli ni kujenga hofu, kuonea watu, kufuta demokrasia, kufuta haki za kikatiba za uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari. Chini ya utawala wake, zilitungwa sheria nyingi za kidikteta, kwa lengo la kuzuia Serikali yake kuhojiwa na yeyote.
Waisrael, walipomkosea Mungu, aliwaacha wakatiwa utumwani ambako waliteseka na kujuta. Baada ya toba na majuto yao, Mungu aliwaokoa tena kwa kuwapa viongpzi wa kuwaongoza kwenye njia ya haki.
Watanzania, kwa miaka karibia 6, watu wameishi kwenye majonzi makubwa, isipokuwa wateule wachache waliopewa uhuru wa kujifanyia chochote wanachotaka. Najua kuna watu, walikesha kila siku wakiomba Mungu awaletee utawala wa haki. Sasa tuna Samia, hata kama atakuwa na mapungufu, lakini hayatakuwa ya uonevu mkubwa kama utawala uliotangulia. Yakumbukeni:
1) Utekaji wa watu wanaohoji
2) Mauaji ya watu wanaohoji
3) Upotezwaji wa watu wanaohoji
4) Mashambulizi dhidi ya wanaohoji
5) Ufungiaji wa vyombo vya habari visivyotaka kumsifia mheshimiwa usiku na mchana
6) Ubambikiaji wa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kwa matajiri wasiotaka kusifu
7) Kuwekwa mahabusu muda mrefu kisha kulazimishwa kukiri kosa na hela yako kukombwa
8) Uteuzi kwenye nafasi za uongozi kwa kuzingatia ukanda, ukabila na undugu
9) Watumishi wa umma kufukuzwa kazi kwa visingizio vya vyeti fake huku akina Bashite, Bagalile na Madelu wakitamba kwa kutumia majina yasiyo yao
10) Sera mbovu za uchumi na uwekezaji zilizofukuza wawekezaji wengi, na kusababisha maelfu ya watanzania kukosa ajira
11) Kuwambikizia viongozi wa upinzani kesi za madawa ya kulevya, mauaji na uchochezi
Samia anaonekana kuguswa na haya yote. Hatayatatua yote mara moja lakini atajitahidi, maana kuharibu ni rahisi kuliko kujenga, kwa vyovyote itachukua muda.
Na wenye kuomba waendelee kuomba ili daima tuwe na uongozi mzuri.
Ndugu zangu, kwa katiba ya sasa ya Tanzania, cha muhimu siyo chama, bali ni aina ya kiongozi mkuu mliye naye.
Mh. Rais Samia, wakati ukirekebisha makorongo mengi yaliyotengenezwa na mtangulizi wako, hakikisha unaondoka madarakani ukiwa umewaachia Watanzania Katiba mpya, katiba ya wananchi.