Umagufuli bila Magufuli utaendelea?

Umagufuli bila Magufuli utaendelea?

Hapana, binafsi sitegemei ingawa kuna Magufuli effects zitakuwepo kwa muda kidogo. Binadamu tumetofautiana na hili huwezi kuigiza! Na ukiigiza ni muda mfupi tu utarudi kwenye nafasi yako.

Mama ata set her good legacy iwapo atasimama kwa miguu yake mwenyewe.
Umeelewa kweli maana ya Magufulism without Magufuli?

Mbona nimeeleza kiurahisi sana..?

Tatizo ni nini? Lugha?
 
Hatutaki huo Unanii. Tunataka Usamializatiom, yani kufuata taratibu na katiba na kutowaonea watu huku watenda maovu wakiwajibishwa. Na sio uonevu, mabavu, roho mbaya, kukosa hekima na busara, kushambulia wapinzani hadi kwa risasi, kuvunja katiba n.k

Amka
 
Umagufuli is synonymous na
1. watu wasiojuliana
2. Kutoheshimu katiba
3. Kunyima wananchi haki ya kuchagua viongozi wao kwa haki
3. Kubambikizia watu kesi
4. Kutangaza hadharani kutowapelekea wananchi maji wasiomchagua
5. Kukataa kutoa msaada wa chakula kwa waliofikwa na majanga ya asili
6. Kufukuza shule watoto wenye mimba
7. Kudownplay science kwenye kupambana na Covid
8. Kufanya miradi miubwa bila kufuata sheria za manunuzi
9 Kuligeuza bunge kikaragosi
10. Kauli chafu zisizo na staha
11. Kunyima watumishi haki yao ya nyongeza za mishahara et c

Sasa sijui huo ndo umagufuli tunaotaka mama Samia aendelee nao?
 
Unaelewa maana ya Magufulism without Magufuli au wewe ukiona jina Magufuli tu unadhani ni yule mtu aliyekuwa anaitwa John Pombe Magufuli?
Ndio wizi wenyewe huo na jamaa zake umesikia huko TPA wameanza kuchunguzwa
 
Umagufuli is synonymous na
1. watu wasiojuliana
2. Kutoheshimu katiba
3. Kunyima wananchi haki ya kuchagua viongozi wao kwa haki
3. Kubambikizia watu kesi
4. Kutangaza hadharani kutowapelekea wananchi maji wasiomchagua
5. Kukataa kutoa msaada wa chakula kwa waliofikwa na majanga ya asili
6. Kufukuza shule watoto wenye mimba
7. Kudownplay science kwenye kupambana na Covid
8. Kufanya miradi miubwa bila kufuata sheria za manunuzi
9 Kuligeuza bunge kikaragosi
10. Kauli chafu zisizo na staha
11. Kunyima watumishi haki yao ya nyongeza za mishahara et c

Sasa sijui huo ndo umagufuli tunaotaka mama Samia aendelee nao?
Huku sijui sisi anatuchukuliaje, kwamba anadhani tumesahau. Hakuna chochote chamaa aliyetuachia zaidi ya mradi unaokula hasara tu
 
Umagufuli bila Magufuli unahitajika nchi hii ili iweze kupiga hatua mbele za maendeleo.
Hivi ni nini kizuri cha pekee ambacho amefanya Hayati Magufuli ambacho watangulizi wake hawakufanya?

Katika kuipeleka nchi mbele, hakika Mwalimu ni wa kwanza. Wa pili ni Mkapa, ndiye aliyeweka mifumo mingi inayoendesha mambo mengi sasa. Na wa tatu ni Kikwete, huyu alijenga miundombinu mingi kwa kiasi ambacho utawala wa marehemu Magufuli haujafikia hata 25%.

Kipya kabisa alichokifanya Magufuli ni kujenga hofu, kuonea watu, kufuta demokrasia, kufuta haki za kikatiba za uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari. Chini ya utawala wake, zilitungwa sheria nyingi za kidikteta, kwa lengo la kuzuia Serikali yake kuhojiwa na yeyote.

Waisrael, walipomkosea Mungu, aliwaacha wakatiwa utumwani ambako waliteseka na kujuta. Baada ya toba na majuto yao, Mungu aliwaokoa tena kwa kuwapa viongpzi wa kuwaongoza kwenye njia ya haki.

Watanzania, kwa miaka karibia 6, watu wameishi kwenye majonzi makubwa, isipokuwa wateule wachache waliopewa uhuru wa kujifanyia chochote wanachotaka. Najua kuna watu, walikesha kila siku wakiomba Mungu awaletee utawala wa haki. Sasa tuna Samia, hata kama atakuwa na mapungufu, lakini hayatakuwa ya uonevu mkubwa kama utawala uliotangulia. Yakumbukeni:
1) Utekaji wa watu wanaohoji
2) Mauaji ya watu wanaohoji
3) Upotezwaji wa watu wanaohoji
4) Mashambulizi dhidi ya wanaohoji
5) Ufungiaji wa vyombo vya habari visivyotaka kumsifia mheshimiwa usiku na mchana
6) Ubambikiaji wa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kwa matajiri wasiotaka kusifu
7) Kuwekwa mahabusu muda mrefu kisha kulazimishwa kukiri kosa na hela yako kukombwa
8) Uteuzi kwenye nafasi za uongozi kwa kuzingatia ukanda, ukabila na undugu
9) Watumishi wa umma kufukuzwa kazi kwa visingizio vya vyeti fake huku akina Bashite, Bagalile na Madelu wakitamba kwa kutumia majina yasiyo yao
10) Sera mbovu za uchumi na uwekezaji zilizofukuza wawekezaji wengi, na kusababisha maelfu ya watanzania kukosa ajira
11) Kuwambikizia viongozi wa upinzani kesi za madawa ya kulevya, mauaji na uchochezi

Samia anaonekana kuguswa na haya yote. Hatayatatua yote mara moja lakini atajitahidi, maana kuharibu ni rahisi kuliko kujenga, kwa vyovyote itachukua muda.

Na wenye kuomba waendelee kuomba ili daima tuwe na uongozi mzuri.

Ndugu zangu, kwa katiba ya sasa ya Tanzania, cha muhimu siyo chama, bali ni aina ya kiongozi mkuu mliye naye.

Mh. Rais Samia, wakati ukirekebisha makorongo mengi yaliyotengenezwa na mtangulizi wako, hakikisha unaondoka madarakani ukiwa umewaachia Watanzania Katiba mpya, katiba ya wananchi.
 
Sawa.

Hajafanya lolote la maana.
 
Walamba makalio wa ibilisi Jiwe Naona wote mmegeuza gia angani mpaka Heri James , Ole Sabaya aiisee mmeshikwa pabaya sana .
Screenshot_20210329-122110.png
 
Back
Top Bottom