Umasikini hurithiwa; masikini huzaa masikini

Kuna culture poverty ambayo kama umezaliwa ndani yake ni vigumu kutoboa.

1. Hakukuna kitu kitakachokupa ushawishi kwakua utaiona ile ni hali ya kawaida.
2. Kama baba alikua anacheza bao mchana kutwa na mama ndiye anaelima, inategemewa na wewe utaishi maisha hayo hayo.
 
Daaah umeandika kinoma, nakupa 5 stars aisee. Ahsante
 
Naam
 


Hii sentence yako ya mwisho huwa sielewi, nadhani huwa Ni mawazo ya watu flani hasa maskini katika kitetea umaskini.
Siko kuutetea umaskini kwa sababu hakuna kitu kibaya Kama umaskini! Hakana kitu kibaya Kama umaskini.

Lakini umaskini wa namna gani ndio mbaya? Hapo inategemeana na tafsiri ya mtu juu ya umaskini.

Lakini pia ikumbukwe hii Ni dunia na dunia inaongozwa na kanuni na moja wapo ya kanuni Ni hakuna usawa, hakuna usawa. Sio nyakati hizi tu bali nyuma ya nyakati, tulizopo leo na zijazo, hakutakuja kuwa na usawa. hivyo umaskini na utajiri kwa namna yake lazima viwepo na kuwepo.

Ila hakuna aliefungwa kubaki maskini daima.
 
Kuna ka ukweli.
Mtoto aliyezaliwa kwenye familia ya wazazi wafanyabiashara ni rahisi sana na yeye kuja kuwa mfanyabiashara kwa sababu kuna wakati huwa anawasaidia wazazi zile kazi kisha anajifunza kitu

Hivyo hivyo wazazi wako kama ni waajiriwa, hata wewe mtoto ukimaliza shule utabweteka tu kitaa kusubiri ajira.

Ni kweli maisha ya wanaokuzunguka yanaweza kukufanya na wewe uje kuwa kama wao.
 
Umasikini ni mada pana sana na inahitaji mjadala mpana sana.....andiko la mtoa mada ni dokezo tu la huo mjadala mpana wa umasikini.......lakini kujikwamua kunategemea vitu vingi sana na mojawapo ni
(1) Fikra
( 2) Nidhamu
(3) Bidii

1) Fikra
-Unahitaji uchanganuzi yakinifu ya fikra na tafakuri juu ya mazingira yanayokuzunguka na changamoto zake ili uweze kutambua namna ya kujikwamua.....

2) Bidii
-Baada ya uchanganuzi wa fikra na kujua njia za kukabiliana na hizo changamoto zinazokuzunguka....unahitaji kuwa na bidii kwenye kuzitatua au kuziendea changamoto hizo......

3) Nidhamu
-Nidhamu ni sehemu muhimu sana kuelekea kwenye kujikwamua kutoka katika umaskini.....unatakiwa kuwa na Nidhamu ya muda na kipato ili uweze kufikia malengo yako.........

Bado huu mjadala ni mpana sana na unahitaji mawazo yakinifu.......karibuni wadau.....
 
Hakika wewe ndiye uliye-summarize vizuri. Umaskini uko zaidi kwenye culture za jamii. Jamii inaishije? Nini kinasemwa kama mafanikio kwenye jamii? kuna vitu vidogo vidogo ndani ya jamii ambavyo ndiyo huamua bidii za mtu. Kama mtu alizaliwa kwenye jamii na akaona wanaokwenda mjini kuomba ndiyo husemwa wana mafanikio basi ni rahisi na yeye kuishia kuomba. Kwa maoni yangu kuondoka na hii visual circle ni kupata elimu sahihi na exposure kwenye jamii nyingine. Nasema elimu sahihi kwa sababu unaweza kuwapa watu elimu isiyo sahihiu na isisaidie chochote au ikazidisha tatizo.
 
Utajiri hauta kua na maana yoyote iwapo hautakupelekea katika mafanikio.
Utajiri ndio mafanikio =mafanikio ndio utajiri.

Mafanikio gani tena unayoyaleta hapa wacha blaa blaa siziso na maana.
Na Kama ni maskini lakini una utukivu wa moyo huo Ni zaidi ya utajiri.
Sipendi sentensi za namna hii.
 
Utajiri ndio mafanikio =mafanikio ndio utajiri.

Mafanikio gani tena unayoyaleta hapa wacha blaa blaa siziso na maana.

Sipendi sentensi za namna hii.
Zamani kabla ya kutembelea duniani na kuona ya walimwengu nilikuwa nadhani mtu akishakuwa na sehemu ya kulala, chakula na vinywaji na pengine gari na fedha za akiba, basi huyo atakuwa ni mtu mwenye mafanikio na furaha tele. Kila niliposikia wazungu wakisema ''important thing is to be happy'' nilikuwa nadhani ukishakuwa na hayo niliyosema ni lazima uwe ''happy''. Sasa hivi nina mawazo tofauti kabisa baada ya kuona kumbe unaweza kuwa na yote hayo lakini usiwe ''happy'' na mtu anaweza kuwa anaishi kwa shida lakini akawa ''happy''
 
Nimesisimka balaa, maana tayari nishatia mimba binti wa kimasikini mtaani wakati na mimi ni masikini niliyepata vijisenti kidogo.
 
Hata mimi sikufahamu kuwa kuna watu wanaweka hela ili zije ziwasaidie wajukuu wakienda chuo kikuu. Maana yake hapa babu amewekeza kwenye elimu ya mjukuu, mjukuu ana uhakika wa kuelimika.
 
Nakubaliana na makala hii lakini kutoka kwenye umasikini haitegemei tu kuchanganya damu,bali hata kubadilisha mtazamo wako.

Kuacha mtazamo wa kimasikini na kuwa na mtazamo wa kupigana zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…