Umasikini hurithiwa; masikini huzaa masikini

Umasikini hurithiwa; masikini huzaa masikini

Umenielewa vyema mtoa mada !?? Amesema kwamba Kama umezaliwa katika Koo masikini halafu katika ukoo wenu mliofanikiwa kuwa na uchumi mkubwa mkiwa wawili halafu wale masikini wakiwa Ni wa 5 hiyo I nakufanya uendelee kubaki kuwa unatoka katika family ya kimasikini Yaani ukwasi wako ulionao haiwezi kukusafisha na kukufanya uonekane unatoka katika family tajiri

Binafsi nimemuelewa sana mleta thread

Serikali impe ulinzi haraka Sana
Ok kama unazungumzia utajiri wa ukoo sawa.
 
Kuzaliwa katika familia maskini si dhambi kwa kuwa wewe huna uwezo wa kubadili matokeo hayo, ila katika maisha haya uliyopewa na Mungu, ukifa maskini hiyo umejitakia. Umejitakia kwa kuwa wanadamu wote tumepewa masaa 24, na uwezo wa kufanya kazi tumepewa sawa, ni namna unavyotumia muda wako ndio inaleta utofauti kati ya maskini na tajiri.

Hivyo basi kama umezaliwa familia ya kimaskini, hakikisha wewe una sacrifice maisha yako ili kizazi cha baadae waweze kuendeleza pale utakapoishia. Wewe ndio uwe wa kwanza ku break hiyo chain ya umaskini. Utavunja vipi mnyororo huo wa umaskini ndio unakuja kwenye point za mtoa mada.

Pia kujifunza namna social class za walio juu yako namna wanavyoishi na hatimaye kuendeleza utajiri walio nao, ni muhimu sana. Hii hubadili mitazamo tuliyorithi kutoka kwenye jamii tunazoishi na husaidia kuwa na mbinu tofauti za kujitafutia maendeleo. Mfano mimi napenda kufuatilia na kujifunza namna jamii ya watu wa bara Asia(wahindi, waarabu, wachina). Watu hawa miaka 100 iliyopita walikuwa kama sisi tu lakini leo hii wanachangia kwa asilimia kubwa katika uchumi wa dunia.
 
Vipi kama umezaliwa na moja kati ya watu expectional, ambayo kwenye ukoo ndio wamebahatika kuwa na vihela wakati wengine waliobaki njaa kali, sasa hapo utahesabika umetoka familia tajiri au maskini?
 
Ukiwa unatoka familia masikini, ukafanikiwa kidogo, ukitaka kuinua ndugu deal na watoto wao usideal na hao ndugu wenyewe. Watoto ndio catalyst ya mabadiliko. Ukideal na ndugu zako waliokuzidi watazidi tu kukunyonya ila watoto wakikaa poa ni rahisi kubadili maisha yao baadae.....
 
Vipi kama umezaliwa na moja kati ya watu expectional, ambayo kwenye ukoo ndio wamebahatika kuwa na vihela wakati wengine waliobaki njaa kali, sasa hapo utahesabika umetoka familia tajiri au maskini?

Exceptional kwa sehemu kubwa huzaa exceptional kutegemea na mke au mume wapoje.


Kibiblia watu Exceptional ni kama Nuhu wakati wengine wakifanya maasi yeye alikuwa mcha Mungu, akapata kibali akapewa mission ya kutengeneza Safina.

Mwingine ni Ibrahimu, Ibrahimu mwana wa Tera, wakati wengine wakiabudu miungu yeye alipata akili ya kuabudu Mungu wa Mbinguni.

Mwingine ni Mfalme Daudi, huyu ametoka familia masikini ya kifugaji lakini baadaye akawa exceptional akawa mfalme. Shida ya Daudi ipo kwenye suala la ndoa ambapo joto ya jiwe aliionja kutokana na kuzaa na wake wengi

Ukiwa Exceptional jitahidi uoe/kuolewa na exceptional mwenzako au mwenye asili ya utajiri

Exceptional jina jingine unaweza kuwaita Next level,
 
Ukiwa unatoka familia masikini, ukafanikiwa kidogo, ukitaka kuinua ndugu deal na watoto wao usideal na hao ndugu wenyewe. Watoto ndio catalyst ya mabadiliko. Ukideal na ndugu zako waliokuzidi watazidi tu kukunyonya ila watoto wakikaa poa ni rahisi kubadili maisha yao baadae.....

Umenena kweli kabisa
 
Tupo kwenye uchumi wa kati naomba tusifatiliane...

Alisikika Mlevi Mmoja hiv" akiwa Bar na nguo za kijani[emoji849]
 
Sometimes tazama tu akili na upeo wa mtu. Unaweza kwenda jimix na watu wenye pesa mambo yakawa sio mambo.

Pesa zinatafutwa ila make sure kabla haujaanza zitafuta upate mtu ambaye anachukia umasikini kuliko kitu chochote na hana tamaa za kipuuzi.
 
Ukiamua kurithi lazima uwe maskini ila ukiamua kutokuurithi utakuwa tajiri mzuri tu aliyetokea familia ya kimaskini.

Kurithi huamui, kurithi kunakuja natural mkuu.

Kama huamini endelea kuishi utakuja kunielewa, au kulewa waliotangulia waliosema huwezi chuma tini kwenye mzabibu' Yesu wa Nazareth
 
Nakujibu kwa kwa namna hiyohiyo ya falsafa yako,fanya reseach zaidi isitumie ubabe wa kusoma kitabu kimoja au viwili ukajiona mwamba Neno maskini au tajiri vinatafsiliwa vibaya kwenye jamii yetu..unaweza kuwa na utajiri wa kipumbavu au masikini mjinga haya maneno unatakiwa kuyafanyia kazi na kuyajua vizuri na ifike wakati tubadilishe mitazamo usiwasilishe hoja kwa mipasho uzi wako umejaa mipasho.
 
Back
Top Bottom