Mtoa mada umeongea ukweli 100% lakini sikubaliani na solutions namba moja uliyotoa, hiyo ya kuchanganya damu, nadhani tunatakiwa tutafute suluhisho lingine lenye uhalisia kuliko hili, ni ngumu sana kuwa applicable, unless ndio uwe wale uliowaita exeptional. Nasema hivi kwa sababu kuchanganya damu na watu wenye asili ya utajiri sio kitu kirahisi, sababu hata wao hawataki kuchanganya damu zao na watu wenye asili za umasikini, tena hasa kwa sasa,angalau kwa zamani kulikuwa na zile cinderella stories, kwamba mwana masikini kaolewa na mwana mfalme. Kwa sasa ni almost impossible ... Sasa kuliko kuendelea kuikumbatia hii suluhisho yafaa watu watafute suluhisho ambalo ni applicable kama hiyo namba mbili uliyoitoa na zingine na zingine.
Huu ni mjadala mkubwa sana among people of colour, na inaaminika kuwa mtu mweusi akifanikiwa anatakiwa afanikiwe kwa asilimia kubwa sana ili aweze kumaintain, akifanikiwa kidogo ni rahisi kuvutwa chini kwa kile wanachokiita "Black tax", kwamba wewe umetokea ukoo masikini, ukifanikiwa kidogo inabidi uanze kuhangaika na masikini wenzako ili nao angalau wanyanyuke, mwishowe mnajikuta mmeanguka wote.
Mimi naunga mkono suluhisho namba mbili uliyoitoa, kwasababu naamini mtu mweusi kufanikiwa inatakiwa juhudi collectively, sio suala la individuals, hivyo kwa kubadili "Imani na mitazamo labda tunaweza kupiga hatua". Nimelipenda swali la aliyeuliza je kuhusu umasikini wa nchi, tunafanyeje? au nchi hizi ndio zitaendelea kubaki hivyo hivyo?
Otherwise, Mimi nimezaliwa na exceptional naamini hadi nifike sehemu fulani nitajikuta exceptional. Tuendelee kukaza wandugu.