Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Enzi hizo nafikiri 1984 Dr. Salim akiwa waziri mkuu alifanya ziara Lindi kama sijakosea na kukuta watu wakiwa wamevaa nguo chakavu ajabu ndio ikawa chanzo cha mitumba kuruhusiwa kuingia nchini.

Ulikuwa ukipatikana na Colgate, Imperial, Rexona au Lux Soaps au hata Lady gay Lotion toka Kenya ilikuwa kama umepatikana tu na meno ya tembo.

Hawa IMF/WB ukishakosana nao na kama hauna pengine pa kukopa ni lazima uwake tu, wanaobisha ni watoto wadogo wasiojua wapi tulikotoka, hawakupanga mawe mbele ya milango ya maduka ya RTC kushikia nafasi ya foleni ya kesho.
 
ugh!
 
Mitumba ilianza kuingia Bongo kabla ya 1984; Kutokana na hali ilivyokuwa mbaya, White Fathers wa enzi zile walikuwa wakileta viroba vya nguzo za mitumba toka kwao Ulaya na kumwaga ktk Parish zao, at least bei ya mitumba hiyo ilikuwa tahafifu.
 
Kabla ya hapo ni mashirika ya kidini tu ndio walioruhusiwa kuingiza mitumba tena enzi hizo ikiitwa "Kafa Ulaya" na walikuwa wakigawa bure kwa waumini wao wenye uwezo mdogo kiuchumi.

Mitumba iliruhusiwa kuingizwa rasmi kibiashara 1984 baada ya Dr. Salim kumshauri Nyerere (Rip) ndio serikali ikaridhia kwani hali ilikuwa ni mbaya mno na viwanda vya nguo nchini viliishaanza kufa na hata kabla vilikuwa vikitengeneza nguo za kiwango cha chini mno mostly polyester.
 
Asante mkuu Nyanjomigire!
 
Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.
Bahati nzuri hukusombwa kwenda Gezaulole enzi hizo, au sio?

Ni 'context' mkuu, ya wakati huo na wakati huu. Wakati huo palikuwepo na "Principle' iliyokuwa inasimamiwi na ilieleweka.

Wakati huu sijui tunachosimamia hasa, au wewe unakijua? Mimi sijaelezwa kinagaubaga nikaelewa, mbali ya kusikia tu kuwa kuna watu "wanyonge".

Ndio, mambo yalikuwa magumu kweli, na yakachagizwa na hao watendaji, hao akina mgambo na wao kuweka ya kwao kama ulivyoyaeleza. Hilo halikuwa lengo, na nashukuru kwamba hukuhusisha yaliyosimamiwa na hayo machafu yaliyojitokeza.

Sasa, siku baada ya siku tulitoka huko na hao jamaa IMF na WB wakaja na ya kwao aliyoyakataa Mwalimu kwa 'principle.'
Wakaleta "Structural Adjustment Programme", unaikumbuka?

Huenda siku moja utakuwa na mda wa kuielezea vizuri ili na wengine tujue ilikotupeleka.

Mambo mengi sana yalikuwa yanatokea wakati ule duniani kote, hata ndugu zetu waliokuwa na nafuu kidogo na wao
wanakumbuka hali hiyo ya mtikisiko. Kenya hadi leo wanamlaani Moi kuwalisha "Yanga" kama farasi! Ethiopia, miaka michache baadae wakaimbiwa "Do They Know It's Chistmas?"

Tushukuru mkuu, tulipita, hata kama ilikuwa ni kwa mbinde; lakini 'Principle' zetu zilibaki 'intact'. Sasa sijui kama katika hili tutakubaliana.

Kwa bahati nzuri, mada zako ni za kufikirisha sana bila la maudhi Allen Kilewella.
 
Acheni masihara tuombe tu Mungu tusiingie kwenye huu mtego maana uchumi utarudi nyuma kwa speed ya light,, na kuja kuwa stable itatuchukua mda sana.

Mungu atuepushe tu na huu mtego wa hawa mabeberu,,
Hakuna mtego wowote tunaowekewa sisi, bali mtego tunajiwekea wenyewe kwa sababu zisizoelezwa. Mbona juzi tu waliwekeana saini na WB kupewa zaidi ya dola bilioni (ndio, bilioni na sio milioni)?

Watu mnapenda sana kuchanganya mambo yenu kwa sababu zisizojulikana!
 
Ndiyo maana watoto wakiwa wanaropoka kwamba maisha enzi za mwalimu yalikuwa mazuri, huwa nawasikiliza tuu kisha nakaa kimya tuu.

Enzi za mwalimu nyerere, mtu akitoka Kinshasa au Bujumbura mnamuona kama ambavyo leo vijana mnavyomuona mtu aliyetoka New York. Mtaa mzima mnamzungumzia yeye.
 
Kwahiyo IMF na World Bank wakisema kitu inabidi tukubali na kufuata hata kama sio kweli au hatukubaliani nacho.
 
Sidhani kuwa yote hayo yalitokana na ugomvi wa mwalimu na IMF, siyo kweli...Hayo yote yalitokana vita kati ya Tanzania na Uganda...kumbuka kabla ya vita maisha yalikuwa mazuri kabisa...Dola moja ya marekani ilkuwa kati ya sh. 5 hadi sh. 7 kama sijakosea...lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya vita...uchumi ukawa mbaya ...ikabidi tujitumbukize baadaye kusaini mkataba na IMF wakati wa Mwinyi..Nyerere alioma kusaini mkataba huo...Lakini kilichochangia pia uchumi kuwa mbaya siyo IMF bali ni mis-management kwenye mashirika ya umma...uzalishaji ulikuwa wa ovyo kabisa kwenye mashirika ya umma ..wanyakazi wengi kwenye mashirika lakini hawazalishi...inefficiency na kadhalika na kadhalika....Nchi karibu zote za Afrika zikalazimikakuinia mkataba na IMF...lakini mikataba hiyo na IMF ilileta balaa...huko Nigeria watu karibu 200 walikufa katika maandamano kupinga mabadiliko ya kiuchumi kutokana na masharti ya IMF..Zambia pia kulikuwa na maandamano pia Uganda, Algeria na kadhalika...
 
Watu hawali principle mzee, watu wanahitaji mahitaji muhimu!
Hayo mambo ya Nyerere kujifanya mwanafalsafa, mwenye misimamo, eti isiyoyumba ilitusaidia nini sisi wakati wa njaa kali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…