Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...


Sidhani kuwa yote hayo yalitokana na ugomvi wa mwalimu na IMF, siyo kweli...Hayo yote yalitokana vita kati ya Tanzania na Uganda...kumbuka kabla ya vita maisha yalikuwa mazuri kabisa...Dola moja ya marekani ilkuwa kati ya sh. 5 hadi sh. 7 kama sijakosea...lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya vita...uchumi ukawa mbaya ...ikabidi tujitumbukize baadaye kusaini mkataba na IMF wakati wa Mwinyi..Nyerere aligoma kusaini mkataba huo...Lakini kilichochangia pia uchumi kuwa mbaya siyo IMF bali ni mis-management kwenye mashirika ya umma...uzalishaji ulikuwa wa ovyo kabisa kwenye mashirika ya umma ..wanyakazi wengi kwenye mashirika lakini hawazalishi...inefficiency ilikithiri kwenye mashirika na serikalini na kadhalika na kadhalika....Nchi karibu zote za Afrika zikalazimika kuingia mkataba na IMF...lakini mikataba hiyo na IMF ilileta balaa...huko Nigeria watu karibu 200 walikufa katika maandamano kupinga mabadiliko ya kiuchumi kutokana na masharti ya IMF..Zambia pia kulikuwa na maandamano pia Uganda, Algeria na kadhalika...
 
1$= 2340.
 
Yaani mkuu story za humu, ndio maana wengine huwa hatuko serious nazo, tunajibu kwa mzaha tu.

Mtu unamuuliza kivipi ugomvi wa serikali na tasisi ya tathmini ya uchumi, ivuruge uchumi wa tz hana jibu!!!.

Report ya zitto imetoka, IMF wanaonyesha msimamo wao jinsi ulivyo hauna mchango wa moja kwa moja isipokuwa ni kama mshauri, watu tunaendelea kuhoji. Haya yote ni kwa maslahi ya taifa au maumivu ya mmoj mmoja!!!
 
Mtu unamuuliza kivipi ugomvi wa serikali na tasisi ya tathmini ya uchumi, ivuruge uchumi wa tz hana jibu!!!.
IMF ni taasisi ya kufanya tathimini ya Uchumi peke yake? Ndiyo maana swali lako halina majibu kwa maana halina msingi unaofanana na mada husika.
 
Kalamu1 umeandika vizuri sana kuhusu "Principle" na wengi wa kizazi hiki hawatakuelewa unamaanisha nini. Kuna wakati nawaza kama kwa jamii hii ya sasa ya watanzania kingetokea nini kama ile vita yetu na Uganda ingetokea zama hizi.

Kanuni maana yake ni lazima uwe na sababu za msingi za kukubali ama kukataa jambo. Kwa mfano Mwalimu alikuwa ni Mjamaa sasa baadhi ya masharti ya WB/IMF yalikuwa ni kinyume kabisa na falsafa yake ya Ujamaa. Leo tunagombana na IMF kwa kigezo gani cha kikanuni?

Lakini programu nyingi sana zilizoletwa na hao mabwana wakubwa zilikuwa haziendani na akili za sisi tulioletewa hizo programu ila zilikubaliwa ili mradi tu tukopeshwe ama tupewe misaada kwa miradi yetu wenyewe tuliyokuwa tunataka kuitekeleza.

Akiulizwa ni kwa nini anataka aliyekuwa Rais wa DRC wakati ule Laurent Kabila asilipe fedha zilizokopwa na Mobutu, lakini anaona sawa aliyekuwa Rais wakati hule Ally Hassani mwinyi alipe mikopo iliyokopwa na yeye, Mwalimu alijibu kwamba Mobutu alikopa kwa kuwatumia wakongo lakini fedha akatumia yeye binafsi wakati yeye Mwalimu alikopa kwa niaba ya watanzania na fedha akazitumia kwa watanzania. Hiyo ndiyo Kanuni.

Nisichoelewa ni kwa nini tunapanga kutekeleza miradi mikubwa sana kwa kutegemea fedha za mikopo na misaada toka kwa watu tunaowaona ni wanyonyaji wa uchumi wetu?
 
Sijuaji kwani hawa IMF wakiikataa nchi yoyotre kinachofuata ni ukame .
Mfano angalia Zimbabwa na Nchi nyingine ziliingia kwenye mtego huu
System nzima ya benk wanaimiliki wao wakikutoa tu! Kwenye system lazima ulimie meno
 
Ishu ambayo watu wengi wanashindwa kuelewa ni kuwa system nzima ya mfumo wa pesa hpa duniani inamilikiwa na wazungu kupitia world bank ndyo ukiwatibua tu! Wanakutoa kwenye system na hela yako inaporomoka thamani kwa kasi ya ajabu ndicho kilichowakuta zimbabwe na venezuela
 
Hujawahi kumuona shoga mtaani? Mpaka wabunge wapo. . Acheni propaganda.. Pogba afukuzwe magogoni.. Wengi wenu kizazi cha instagram hamjui shida
 

Unfortunately, ndiko tunakoelekea. Ila sio IMF tu watakaosababisha hali hiyo. Chanzo kikubwa ni utawala mbovu uliopo unaoamini kuwa serikali inaweza kufanya biashara na ikapata faida.
 
Unfortunately, ndiko tunakoelekea. Ila sio IMF tu watakaosababisha hali hiyo. Chanzo kikubwa ni utawala mbovu uliopo unaoamini kuwa serikali inaweza kufanya biashara na ikapata faida.
IMF watolewe kabisa kwenye hili, maana hata uchumi ukikua huwa hawahusiki.
 
Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.
Umenikumbusha mbali sana. Tumevaa sana hizo nguo shuleni. Kitambaa kilikuwa kikiitwa malekani. Na kwa sababu ya ukosefu wa vitenge na kanga, kina mama nao walivaa hizohizo malekani lakini zilizowekwa rangi za kienyeji nadhani, na wao wakaziita kamanyora. Ilikuwa patashika. Ila vijana wa dotcom hawajui haya.
 
Kilichotokea africa ndicho kilichotokea amerika ya kusini tht why today Tanzania tunamiliki only 4% ya madini asilimia zilizobaki wanamiliki mabeberu
 
Hawa wazungu vitafunwa kweli yani ugombane na mtu mmoja utese mamilioni ya watu?
Ila msimu huu tuna chakujitetea kuwa kwa bahati mbaya tunae kichaa na tulichaguliwa hatukumchagua wenyewe.
 
Hii ya kweli kabisa kwani hawa Watu sio wa kubeza kumbuka kila kitu wao wanapanga bei ss tukilima huku wao wanatupangia bei.
Sasa watu kama hawa huwezi kubishana nao kwani wao wanaamuzi yote hata ya kiutawala wakiamua kumweka Mtu wao wanamweka
 
Kweli njaa kipimo cha akili
Miaka hiyo ya 83-84 kule vijijini hali ilikuwa mbaya mno bora ya DAR kidogo nakumbuka mwaka 88 sukari ilikuwa hadimu kwelikweli ambapo wazazi wetu walikuwa wananunua zile pipi za rangi zinasagwa na zinatumiwa kama sukari kwenye chai....
 
Nadhani umejichanganya kidogo.Badaa ya Mwinyi kukubali masharti ya IMF ndipo tulipoanza kupata unafuu kama taifa. Bidhaa zilianza kufurika madukani, nguo aina ya malekani na kamanyora zikaanza kutoweka (baada ya kuingiza nguo kutoka China, Japani, India na mitumba kutoka Ulaya). Nakumbuka akina mama walianza kuvaa kanga za China, Japani na India. Kiujumla hali ilibadilika kuwa nafuu kuanzia kipindi hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…