Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.
Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.
Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.
Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.
Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..
Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.
Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.
CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Sidhani kuwa yote hayo yalitokana na ugomvi wa mwalimu na IMF, siyo kweli...Hayo yote yalitokana vita kati ya Tanzania na Uganda...kumbuka kabla ya vita maisha yalikuwa mazuri kabisa...Dola moja ya marekani ilkuwa kati ya sh. 5 hadi sh. 7 kama sijakosea...lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya vita...uchumi ukawa mbaya ...ikabidi tujitumbukize baadaye kusaini mkataba na IMF wakati wa Mwinyi..Nyerere aligoma kusaini mkataba huo...Lakini kilichochangia pia uchumi kuwa mbaya siyo IMF bali ni mis-management kwenye mashirika ya umma...uzalishaji ulikuwa wa ovyo kabisa kwenye mashirika ya umma ..wanyakazi wengi kwenye mashirika lakini hawazalishi...inefficiency ilikithiri kwenye mashirika na serikalini na kadhalika na kadhalika....Nchi karibu zote za Afrika zikalazimika kuingia mkataba na IMF...lakini mikataba hiyo na IMF ilileta balaa...huko Nigeria watu karibu 200 walikufa katika maandamano kupinga mabadiliko ya kiuchumi kutokana na masharti ya IMF..Zambia pia kulikuwa na maandamano pia Uganda, Algeria na kadhalika...