Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Yale maumivu ya miaka ile yalileta tija gani na haya ya sasa unadhani tija yake itakuwa ipi?
Ya wakati ule yalifanya tukawa na akili hata kidogo za kibepali tulizonazo leo, vinginevyo ingekuwa tatizo zaidi.

Sasa kuna maumivu gani ya kulinganisha na wakati huo!!!
 
Credibility kidogo mliyokuwa nayo mshaipoteza, you better shut up.
Hueleweki unapofanya jambo la nchi kama ni masuala ya kivyama. Nyie wenye "Credility" ndiyo kila siku mnakiri hadharani waliowatangulia walikosea kuongoza nchi.

Hii nchi haijawahi kuongozwa na chama kingine zaidi ya CCM kwa ivo madudu yote yanatokana na CCM kuwa madarakani. Chama kisicho na "Credibility" ndiyo mnalazimisha washushe bendera zao kwa lazima?
 
Acheni masihara tuombe tu Mungu tusiingie kwenye huu mtego maana uchumi utarudi nyuma kwa speed ya light,, na kuja kuwa stable itatuchukua mda sana.

Mungu atuepushe tu na huu mtego wa hawa mabeberu,,
Mimi sielewi eti hivi tunategwa na mabeberu au tunajitega wenyewe kwa uroho wetu wa madaraka?
 
Mkuu umesahau,watu walitembea matako wazi kwa kukosa nguo hata za mtumba.Ndala zilikuwa za tairi za gari.
 
Hivi Tundu lisu ndo ametunga Sheria ya takwimu? Mkuu Kama huna nauli ya kwenda Dodoma mie ntakuchangia please
Dodoma kuna mambo matatu:

  1. Kupigwa risasi
  2. Kuchapwa bakora kichwani mpaka uzimie
  3. Au uingie ukumbini pekupeku
Sijui kati ya hayo matatu ukimpa nauli litamkuta lipi?
 
Wananchi wanatumiaje nguvu kazi zao bila ya kuwa na sera za kifedha nzuri za nchi za kimataifa. Hivi Zimbabwe waliingia kwenye ufukara kwa kuwa tu walikuwa hawana nguvu kazi ya wananchi?
Sera za kimataifa ni kwa ajiri ya manufaa yao waliozitunga,haziwezi kukufaa wewe wakati wote, una factor tofauti.

Kule urusi, china na kolea waliamua tu na ikawezekana. Sasa hivi kila mtu anamheshimu mwenzake.
 
Mamaee,nimecheka vibaya mno,kwamba akili zimedumaa kwa kula chakula cha ng'ombe?!!
 
Nina mashaka na UMRI wako, na jinsi ulivyo hadithiwa,
HISTORIA MASHULENI HAWA WAALIMU WANA POTOSHA WATOTO WETU,

ndio maana naanza kuona sasa VIJANA wanakosa UZALENDO.
Nahisi wewe ndiye Mtoto na hujui unaloliongea, unajua azimio LA arusha? Hujui utaifishaji wa majumba, mabenki, mashule, mahospitali, makampuni nk? Au wewe unajua nn?
 
Afadhali mabalozi wa nyumba kumi, Mgambo walifanya kufuru sana. Kwetu kulikuwa na mmoja anaitwa "Mikonyezo" huyu alikuwa hatari ukichanganya alikuwa anamiliki Vespa "Batavuzi".
Bwana "Mikonyezo",sio kwa kuwapelekea moto wake za watu hapo kijijini,naamini lazima alikufa kwa ngoma baadae.
 
Sera za kimataifa ni kwa ajiri ya manufaa yao waliozitunga,haziwezi kukufaa wewe wakati wote, una factor tofauti.

Kule urusi, china na kolea waliamua tu na ikawezekana. Sasa hivi kila mtu anamheshimu mwenzake.
Hii hoja inaupotoshaji wa hali ya juu sana. Urusi na Uchina walitoka kwenye Ubepari kwenda kwenye ushoshalisti na Ukomunist na wamerudi kwenye Ubepari unaodhibitiwa na dola,

Hao wote unaowataja kwa wakati mmoja ama mwingine wameshirikisha mabepari wanaofadhiliwa na hayo Mashirika kujenga uchumi wa nchi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…