Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Acheni masihara tuombe tu Mungu tusiingie kwenye huu mtego maana uchumi utarudi nyuma kwa speed ya light,, na kuja kuwa stable itatuchukua mda sana.

Mungu atuepushe tu na huu mtego wa hawa mabeberu,,
Unalaumu Mabeberu tu. Unajua sababu we mpiga kinubi wa jiwe?
 
Dah
kama alivyosema mdau mmoja hapo juu kuwa Wananchi walikuwa wavumilivu sana kipindi hicho
Maisha yalikuwa mabaya sana lakini tuliambiwa hakuna namna ni lazima tuishi kama ilivyokuwa. Mwalimu alikataa kugeuka nyuma ili asije kugeuka jiwe. Mwinyi ndiye alikuja kuruhusu biashara huria na vitu toka Kenya kuingia Tanzania.
 
Maisha yalikuwa mabaya sana lakini tuliambiwa hakuna namna ni lazima tuishi kama ilivyokuwa. Mwalimu alikataa kugeuka nyuma ili asije kugeuka jiwe. Mwinyi ndiye alikuja kuruhusu biashara huria na kurushu vitu toka Kenya kuingia Tanzania.

Aisee

Ngoja na sisi Ujamaa urudi kupitia mheshimiwa wetu hahahah
 
Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.

Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.

CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Kuna kitu kikubwa ambacho wengi hawajaona ktk kauli ya IMF (kama ikithibitishwa ni kweli wametoa hio kauli):

Miradi mingi ya Maendeleo inayotekelezwa na GoT inafadhiliwa/inakopeshwa na washirika wa maendlzeo kama WB, AFDB, JICA ama Scandnavian countries, na hilo hufanyika baada ya wao kuridhika na mapendekezo na mpango wa utekeleza wa GoT.

Ni muda mrefu sasa tangu IMF itoe mkopo/msaada wa aina yeyote ile kufadhili miradi ya Maendeleo ktk TZ. Hali ni tofauti kwa WB, AFDB, JICA ama Scandnavian countries ambao wako bega kwa bega na GoT na hata zikitokea tofauti hua zinamalizwa and life goes on bila kushinikizana kwa kutumia magazeti au waandishi wa habari wa Kenya.

Haingilii akilini kuona IMF ianatoa matamko yanayo pingana na washirika wengine ndani ya siku 2 tu tokea washirika hao (WB, AFDB, JICA) waingie makubaliana ya mikataba ya kukopesha TZ zaidi ya Tsh Trillion 2 za utelelezaji wa miradi ya maendeleo.

Eti IMF wanaita miradi hio kuwa haina maaana kwa Maendeleo ya TZ, swali la kujiuliza, je hivi washirika hao wengine wa maendeleo hawajaliona hilo wakati wanafanya due diligence kabla ya kukubali kutoa hizo fedha za miradi (i.e, BRT, SGR, Elimu, Steglers, Afya)?

Kwa hali ilivyo inawezekana kabisa:

  1. Kuwa IMF wanafanya maksudi ili kutengeneza hali ya hofu na kuchafua investment climate ya TZ duniani ili wabia wetu wa maendleo na wawekezaji waogope kushirikiana na GoT. Then tuwapigie magoti wao waje na bail-outs kutuokoa at their own terms; ama
  2. kuwa kuna watu walioko ndani ya TZ na nje wanashirikiana kwa kupeleka habari hasi IMF ili kuishinikiza GoT ibadili misimamo yake kwenye mambo kama sera za madini, energy (umeme), etc, ili GoT ikubali kuweka sera za kunufaisha makampuni yao.
Ikumbukwe kuwa IMF ni chombo amabacho kimekuwa kikutumiwa kuharibu uchumi wa nchi nyingi duniani kuanzia Latin Amerika (Brasil, Argentina) , Ulaya (Greece, etc), Asia na hata Afrika (Kama OP ulivyoeleza enzi za Mwl. Nyerere au hata Kenya miaka ya hivi karibuni). Huwa wanashinikiza nchi husika kufuata maelekezo yao kama vile kuuza viwanda vya ndani, kubinafsisha SOEs etc na baada ya hapo hali huwa inabadlika kuwa mbaya zaidi nya awali na huleta uasi na machafuko ya kijamii.

Cha muhimu ni kwa GoT kuhakikisha Kuwa haichukui mkopo wa aina yeyote toka IMF period. Kama tayari mikopo hio ilikuwepo toka zamani basi wendelee kuilipa lakini kamwe wasikuckue mikopo yao mipya.
 
Aisee

Ngoja na sisi Ujamaa urudi kupitia mheshimiwa wetu hahahah
Tusiombe ile hali ijirudie. Watu walikuwa wanakwenda kazini kwa kupakizwa kwenye Pick Up baada ya Magari ya UDA kutotosheleza. Jumapili Magari kutembea mwisho saa 8 mchana isipokuwa yale tu yaliyoruhusiwa kwa maana hakukuwa na mafuta ya kutosha.

Dala dala zilianzia hapo baada ya UDA kuzidiwa na idadi ya Abiria. Magari binafsi yalikuwa yanatoza shilingi tano kwa nauli wakati UDA walitoza shilingi moja kwa mtu mzima na senti hamsini kwa watoto na wanafunzi.

Dola moja ilikuwa sawa na shilingi tano (Gwala) ya kitanzania kwa ivo magari yaliyotoza shilingi tano yakawa yanaitwa "Dala dala".
 
Tusiombe ile hali ijirudie. Watu walikuwa wanakwenda kazini kwa kupakizwa kwenye Pick Up baada ya Magari ya UDA kutotosheleza. Jumapili Magari kutembea mwisho saa 8 mchana isipokuwa yale tu yaliyoruhusiwa kwa maana hakukuwa na mafuta ya kutosha.

Dala dala zilianzia hapo baada ya UDA kuzidiwa na idadi ya Abiria. Magari binafsi yalikuwa yanatoza shilingi tano kwa nauli wakati UDA walitoza shilingi moja kwa mtu mzima na senti hamsini kwa watoto na wanafunzi.

Dola moja ilikuwa sawa na shilingi tano (Gwala) ya kitanzania kwa ivo magari yaliyotoza shilingi tano yakawa yaitwa "Dala dala".


Hhahahah

Kwa kipindi hiki watafeli aisee maana watu watajitoa muhanga kutokubali hali kama hiyo. Kuna watu watakubali kwenda jela kuliko kuvumilia upuuzi wa hivyo
 
natamani sana kungetengenezwa documentary/ makala ya watu walioishu enzi hizi wakielezea hali ilivyo huku ikiwa na video zilizochukuliwa enzi hizo huku wataalamu wa historia na wachumu wakisimulia chanzo cha ushu hiyo.

it is very intersting story.
Chanzo ni sera za mwenye heri mtakatifu Nyerere, hata vita na Uganda ulikuwa ni ugomvi binafsi wa mtakatifu na Idd Amin kwa sababu Milton Obotte alikuwa Tanzania na mipango yote ya kumpinduwa Idd Amin ilifanyikia Tanzania kwa baraka zote za Mtakatifu. Huu ndio ukweli.

Bado leo kuna kundi la matapeli linaamini wanaweza kushindana na wakubwa, waangalie tu sikukuu ya pasaka hii ilivyodorora, tunarudi kulekule ila safari hii madukani kuna vitu lakini watu hatuna kitu.
 
Kinacho nishangaza watu badala ya kuleta historia halisi na hoja mezani kulingana na mtoa mada waliowengi mnatoa matusi alafu mnajiita ma Great Thinkers!!!!!! Kweli mnachofanya siyo sahihi
 
Enzi za chama kushika hatamu,
Tatizo una changanya Mambo,
1.Nyakayi i.e. kipindi cha kutupa hela na kumiliki Mali e.g. TV

2.UJAMAA na MASHARTI YA MABEBERU, hata sasa wanataka USE SHOGA, je utakubali??? wana gawa kondomu, ili hali, nyenzo za umiliki Mali wana zishikiria, UNAPEWA ELIMU YA MATUMIZI na sio MATENGENEZO, e.g. simu, laptop n.k

n.b. JAMBO USILO LIJUA NI SAWA NA USIKU WA GIZA, usimlaumu mwl, sema tu ALI SAILTIWA.....

Ujamaa ni nadharia na ni ngumu kuwa katika halisi, sababu hulka ya mwanadamu ni u binafsi.Nyerere alitufanyia mengi sana Mazuri mfano kuunganisha watu umoja wa kitaifa,undugu wa kitz,ardhi kuwa si Mali binafsi ila alifanya makosa kuleta ujamaa na azimio la Arusha.Mi naukubali sana ubepari kwani unachochea kukua kwa uchumi na kumfanya masikini apate nafuu. Hulka ya tajiri ni kutaka zaidi kutaka zaidi umfanya azidi kufungua miradi mingi zaidi ambapo masikini watapata ajira na serikali itapata kodi zaidi kupitia Tozo mbali mbali.
 
Ujamaa ni nadharia na ni ngumu kuwa katika halisi, sababu hulka ya mwanadamu ni u binafsi.Nyerere alitufanyia mengi sana Mazuri mfano kuunganisha watu umoja wa kitaifa,undugu wa kitz,ardhi kuwa si Mali binafsi ila alifanya makosa kuleta ujamaa na azimio la Arusha.Mi naukubali sana ubepari kwani unachochea kukua kwa uchumi na kumfanya masikini apate nafuu. Hulka ya tajiri ni kutaka zaidi kutaka zaidi umfanya azidi kufungua miradi mingi zaidi ambapo masikini watapata ajira na serikali itapata kodi zaidi kupitia Tozo mbali mbali.
Sawa bwana!
 
Nae

Nakumbuka vizuri kipindi hiki Nyerere alituahidi miezi 18 ya njaa lakini badala yake ikawa ni ufukara wa kudumu, mbaya zaidi akamteuwa waziri mkuu kichaa ndio ikawa mshike mshike hasa.

Ila mimi mtaani kwetu tulipata bahati tulikuwa na brother ni mtundu wa kuiga signature gari la ugawaji likija foneni ya kuweka sign kwenye vitabu tulikuwa hatukai jamaa akiangalia tu zile saini za makarani wa siku hiyo mchezo umeisha anazipiga vilevile

Ila Zimbabwe inasikisha zaidi mwaka 1997 nilipita Zimbabwe transit nakumbuka nilitoa noti ya Zim dola 5 kununuwa hot dog na cicacola can lakini bado nilirudishiwa chenji ya kwacha kadhaa by that time Zimbabwe walikuwa wanatumia sarafu mbili kwa wakati mmoja ila Zim dola ilukuwa powerfull zaidi ilikuwa ikichuana na Rand ya Sourh Africa na Pula ya Botswana.

By the way jana Pasaka jana mji umepowa utadhani ni karume day, nadhani wenzetu wanaccm walikuwa sehemu yao maalum wanafurahia sikukuu.

Siku zote nawaambia watu viongozi wa kiafrica kwenye uchumi wanafeli.Hawajafikia hata nusu na robo speed ya mkoloni kutuletea maendeleo. Hali ya kimaendeleo ya Africa ailingani kabisa na umri tulionao baada ya Uhuru,tungekuwa dunia ya PILI zaidi ya Latin America.
 
Sina maana HIYO, na sija isifia.
But, TAFUTA taarifa sahihi....
Taarifa sahihi iko wapi mkuu zaidi ya maisha magumu waliyonayo watanzania,?Uchumi ni kama mimba huwezi kuficha,mwambieni jamaa yenu 2020 astaafu kwa heshima na Dunia itamkumbuka kwa hekima endapo ataondoka kwa kustaafu mwenyewe.
2020 hatashinda,ni kichaa pekee anayeweza kumpigia kura huyu mtu,hivi unamchagua huyu kwa lipi hasa!???
Nchi nzima imejaa vilio vya ugumu wa maisha,na kwa sababu huyu ni mpumbavu akila yeye akashiba,anakula chochote anachotaka,anaona wanaoteseka na maisha magumu hawana akili timamu na ni wavivu wa kutafuta.
Nyie endeleeni kumpigia makofi tu ila muda utaongea,si umeona kilichomkuta Bashir? Naye alijua anapendwa sana na hakuna wa kumtoa.
 
Miaka hiyo ya 83-84 kule vijijini hali ilikuwa mbaya mno bora ya DAR kidogo nakumbuka mwaka 88 sukari ilikuwa hadimu kwelikweli ambapo wazazi wetu walikuwa wananunua zile pipi za rangi zinasagwa na zinatumiwa kama sukari kwenye chai....
Mimi nakumbuka tulikuwa tunatengeneza kahawa bila sukari tunakula na viazi vitamu Au linatengenezwa togwa la ndizi linawekwa kwenye uji. Maisha hayo yalikuwa magumu sana.
 
Back
Top Bottom