Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.
Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.
CC:
Mshana Jr Pascal Mayalla
Kuna kitu kikubwa ambacho wengi hawajaona ktk kauli ya
IMF (kama ikithibitishwa ni kweli wametoa hio kauli):
Miradi mingi ya Maendeleo inayotekelezwa na GoT inafadhiliwa/inakopeshwa na washirika wa maendlzeo kama WB, AFDB, JICA ama Scandnavian countries, na hilo hufanyika baada ya wao kuridhika na mapendekezo na mpango wa utekeleza wa GoT.
Ni muda mrefu sasa tangu
IMF itoe mkopo/msaada wa aina yeyote ile kufadhili miradi ya Maendeleo ktk TZ. Hali ni tofauti kwa WB, AFDB, JICA ama Scandnavian countries ambao wako bega kwa bega na GoT na hata zikitokea tofauti hua zinamalizwa and life goes on bila kushinikizana kwa kutumia magazeti au waandishi wa habari wa Kenya.
Haingilii akilini kuona
IMF ianatoa matamko yanayo pingana na washirika wengine ndani ya siku 2 tu tokea washirika hao (WB, AFDB, JICA) waingie makubaliana ya mikataba ya kukopesha TZ zaidi ya Tsh Trillion 2 za utelelezaji wa miradi ya maendeleo.
Eti IMF wanaita miradi hio kuwa haina maaana kwa Maendeleo ya TZ, swali la kujiuliza, je hivi washirika hao wengine wa maendeleo hawajaliona hilo wakati wanafanya due diligence kabla ya kukubali kutoa hizo fedha za miradi (i.e, BRT, SGR, Elimu, Steglers, Afya)?
Kwa hali ilivyo inawezekana kabisa:
- Kuwa IMF wanafanya maksudi ili kutengeneza hali ya hofu na kuchafua investment climate ya TZ duniani ili wabia wetu wa maendleo na wawekezaji waogope kushirikiana na GoT. Then tuwapigie magoti wao waje na bail-outs kutuokoa at their own terms; ama
- kuwa kuna watu walioko ndani ya TZ na nje wanashirikiana kwa kupeleka habari hasi IMF ili kuishinikiza GoT ibadili misimamo yake kwenye mambo kama sera za madini, energy (umeme), etc, ili GoT ikubali kuweka sera za kunufaisha makampuni yao.
Ikumbukwe kuwa IMF ni chombo amabacho kimekuwa kikutumiwa kuharibu uchumi wa nchi nyingi duniani kuanzia Latin Amerika (Brasil, Argentina) , Ulaya (Greece, etc), Asia na hata Afrika (Kama OP ulivyoeleza enzi za Mwl. Nyerere au hata Kenya miaka ya hivi karibuni). Huwa wanashinikiza nchi husika kufuata maelekezo yao kama vile kuuza viwanda vya ndani, kubinafsisha SOEs etc na baada ya hapo hali huwa inabadlika kuwa mbaya zaidi nya awali na huleta uasi na machafuko ya kijamii.
Cha muhimu ni kwa GoT kuhakikisha Kuwa haichukui mkopo wa aina yeyote toka IMF period. Kama tayari mikopo hio ilikuwepo toka zamani basi wendelee kuilipa lakini kamwe wasikuckue mikopo yao mipya.