Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.

Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.

Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.

Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.

Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..

Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.

Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.

CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
 
I still remember those days, katambuga, midabwada(viraka), duka la kaya zilikuwa ni common terms. Kwenda kununua vitu National milling(in bulk) ilikuwa mpaka uwe na ka'note ka kutoka wizarani.
Kwa senior officers wa serikali na wa kwenye mashirika ya umma kulikuwa na unafuu lakini kwingineko ilikuwa ni mshikemshike.
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu.
Wakati ule tulikuwa wavumilivu sana. Siwezi kusema kuwa kulikuwa na uzalendo, ila uvumilivu tu. Je uvumilivu ulileta faida kwa nchi au hasara? Je wakati huu wa sayansi na teknolojia iliokomaa uvumilivu utatamalaki bado? Nchi inahitaji kwenda na dunia ki maendeleo. Enzi za foleni ya shirika la Ugawaji halina nafasi. Badala ya kufanya kazi wananchi including watoto walishinda kusubiri unga, sukari, mafuta nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni masihara tuombe tu Mungu tusiingie kwenye huu mtego maana uchumi utarudi nyuma kwa speed ya light,, na kuja kuwa stable itatuchukua mda sana.

Mungu atuepushe tu na huu mtego wa hawa mabeberu,,
 
Lissu kwa ujuzi wake washeria ulivyo sidhani kama hataru na kurasa mpya ambao ni mwanzo Tanzania mpya kwani mazingira ameshayaona yalivyo ndio maana tunatakiwa kumwombea sana kwa Mungu apone vizuri kwani kululu inalindwa kama mboni ya jicho Lissu yule sio Lissu wa leo ambaye Dunia inamulika na kumwangalia ni nani atakayemgusa kwa lipi
 
Back
Top Bottom