Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umenikumbusha mbali sana mkuu.
Wakati ule tulikuwa wavumilivu sana. Siwezi kusema kuwa kulikuwa na uzalendo, ila uvumilivu tu. Je uvumilivu ulileta faida kwa nchi au hasara? Je wakati huu wa sayansi na teknolojia iliokomaa uvumilivu utatamalaki bado? Nchi inahitaji kwenda na dunia ki maendeleo. Enzi za foleni ya shirika la Ugawaji halina nafasi. Badala ya kufanya kazi wananchi including watoto walishinda kusubiri unga, sukari, mafuta nk.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani mpaka khanga zilishonwa viraka, tena sometimes kiraka cha khaki material hadi ukaja ubunifu kuyapika mavitambaa(sikumbuki ni madurufu yale au materials gani) kwa marangirangi na kuyakausha(tie and dye if I'm not mistaken) na ikawa ni biashara hasa.
Raha ilikuwa ni mtu akitoka overseas upate jeans, T-shirts, 'raba mtoni' na music system na audiotapes zenye ngoma latest dunia yote unaiona yako. Nchi ilikuwa imejaa dhiki na ushamba kiasi kwamba hata mtu aliyekuja kutoka Burundi alikuwa anaonekana 'sopsop' kuliko m'Tz.
Umenikumbusha mbali!!!! Nilipojifungua mtoto wangu wa kwanza 84 nilichukua hizo marekani nikazinunulia jick toka Kenya ili ziwe nyeupe. Shuleni tulikuwa tunafundishwa kutalizi hivyo nilizipamba nepi za mwanangu ikawa fasheni. Raba mtoni ilikuwa hatari na isilogwe ukaanika nje inatoka kabla haijakauka! Khanga za kenya zilikuwa na maneno siyo mazuri ila tulipenda ugumu wake na rangi zake? Hivi bado zipo??? Tumetoka mbali na tumesota sana. Hivi wanataka kuturudisha huko tugeuke mawe?Yaani mpaka khanga zilishonwa viraka, tena sometimes kiraka cha khaki material hadi ukaja ubunifu kuyapika mavitambaa(sikumbuki ni madurufu yale au materials gani) kwa marangirangi na kuyakausha(tie and dye if I'm not mistaken) na ikawa ni biashara hasa.
Raha ilikuwa ni mtu akitoka overseas upate jeans, T-shirts, 'raba mtoni' na music system na audiotapes zenye ngoma latest dunia yote unaiona yako. Nchi ilikuwa imejaa dhiki na ushamba kiasi kwamba hata mtu aliyekuja kutoka Burundi alikuwa anaonekana 'sopsop' kuliko m'Tz.
Kama mbinguni kuna matabaka why Tanzania ujamaa ni mfumo wa kijinga yaani umaskini ni fahari
Umenikumbusha mbali!!!! Nilipojifungua mtoto wangu wa kwanza 84 nilichukua hizo marekani nikazinunulia jick toka Kenya ili ziwe nyeupe. Shuleni tulikuwa tunafundishwa kutalizi hivyo nilizipamba nepi za mwanangu ikawa fasheni. Raba mtoni ilikuwa hatari na isilogwe ukaanika nje inatoka kabla haijakauka! Khanga za kenya zilikuwa na maneno siyo mazuri ila tulipenda ugumu wake na rangi zake? Hivi bado zipo??? Tumetoka mbali na tumesota sana. Hivi wanataka kuturudisha huko tugeuke mawe?
Waache washangiiliaji labda wawe na ndugu ughaibuni na hivi hawaruhusiwi kutoka, watajiju. Watakumbuka enzi za sabuni za mchina za MEI YU, Samsang, mu na zingine ambazo ukiogea unapata vipere. Mikopo ya wachina itatufikisha kule tulikotoka.
Sudan Rais aliongeza bei ya mkate tu Duuh! wakamuondoa Rais Bashiri madarakani!!! Unajifunza nini hapa kwa Watanzania kuvumilia hayo yote? Lack of knowledge! Ingalikuwa ni ile miaka ya 1470 A.D. wote wangaliishia kuwa watumwa Uarabuni na India! Haya ni mawazo yangu tu isipokuwa Wamaasai![emoji38]
Saa hivi kupata hata pass wanahaha. Tunapowaambia watashaa wanadhani uongo. We were together in the rain but some of us managed to get the shelter somewhere.Mpaka wajionee kwa macho ndiyo wataamini, watatafuta pa kukimbilia.
Sisi walowezi wa mbali tutawakaribisha wakianza kukimbia though kimbia ya wengi itakuwa ni ile unplanned.
Ujamaa ulifaa Wa-Africa woote, siyo kizazi kimoja tu cha Kitanzania cha jana au leo, Ujamaa ulianzia mbinguni, haupitwi na wakati, pia Mawazo huwa hayagandi, waliosema ivo ni waongo. usiamini kila jambo..Nyie bado mmefungwa na mawazo mgando ujamaa uliwafaa nyie sio kizazi cha sasa,kila kitu kimebadilika mazingira na mifumo imebadilika.Hakuna laana yeyeto ya kumkosoa MWALIMU yule ni mwanadamu anayo mema mengi na mabaya pia japo alifanikiwa kuyadhibiti yasijulikane na aliweza sababu hakukuwa na mitandao tofauti na huyu copy na paste inavomuumbua.Ujamaa ndio ulizaa azimio la Arusha la kudhulumu Mali za watu walizozitafuta kwa jasho kizazi na kizazi.Laana ya kuitaifisha Mali za watu pasipo ridhaa zao ikapelekea zote kufa kibudu na kupelekea kuzirejesha mikononi mwa watu.Nia ya MWALIMU ilikuwa ni nzuri sema tu akuzijua tabia za watz.Swala LA watu kuchagua aliyewaambia mtaisoma no ( kuwafanyeni nyote muwe masikini) na watu kuchagua huo ni uelewa Mdogo wa watu sababu ya ukosefu wa utambuzi tofauti na wenzetu wa Kenya walivoambiwa hivo awakukosea kuchagua Leo Wangekuwa wakilia tu wakaona heri ya mkate kamili.
Amina ndugu yangu weee! kalamu1Eeenh, smaki, una njia yako ya kufikisha ujumbe; ni njia isiyokuwa rahisi sana kwa wengi watakaokusoma, lakini ni ujumbe mzito uliotoa hapa..
Kuna mtu humu anasema eti Kenya tupo nao sawa kimaendeleo D
Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.
Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.
Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.
Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.
Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..
Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.
Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.
CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Aisee!!Kwa bahati mbaya ndiko magufuli anakotupeleka.
Hawa kanda ya ziwa si wazuri sana kwenye uchumi ni wazuri kwenye kusomesha namba watu na si kuinua watu Nyerere aliuwa uchumi kama ilivo awamu nayo imekuja kuuwa uchumiNakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.
Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.
Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.
Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.
Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..
Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.
Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.
CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Sidhani kama kuna tatizo linalohusiana na watokako. Tatizo mmoja anataka kumuiga mwingine. Kama alikosea na yeye pia atakosea.Hawa kanda ya ziwa si wazuri sana kwenye uchumi ni wazuri kwenye kusomesha namba watu na si kuinua watu Nyerere aliuwa uchumi kama ilivo awamu nayo imekuja kuuwa uchumi
Kabisa. Kama biashara za watu binafsi zinauawa kwa makusudi (kutokana na sheria mbovu na uonevu wa dhahiri) tutegemee nini?Aisee!!
Ndio kulimia meno kwenyewe huko,mlidhani wanaambiwa matajiri. Hali itakuwa ngumu kuliko hata kipindi cha nyerere mnapoambiwa sio kila jamii ni za kuwapa leseni ya udereva muwe mnaelewaKabisa. Kama biashara za watu binafsi zinauawa kwa makusudi (kutokana na sheria mbovu na uonevu wa dhahiri) tutegemee nini?
Soma history ya mkoloni kwann jamii zingine aliona ni hasara kuzipa elimu,jamii inayoamini matumizi ya nguvu kuliko akili aliitumia kwenye Kazi za mashambani na ukuli bandarini sasa usipojua history ukachanganya vitu hivi ni lzm yaharibike mambo.We uoni hio jamii si wazuri kwenye reasoning Bali kwenye nguvu.Uongozi ni hekima na busara ukitumia mechanical ni lzm GARI litafail tu.Sidhani kama kuna tatizo linalohusiana na watokako. Tatizo mmoja anataka kumuiga mwingine. Kama alikosea na yeye pia atakosea.