Umasikini wa mtu unaanzia kichwani pake. Kama utani nilivyopoteza mtaji wangu wote kizembe

Umasikini wa mtu unaanzia kichwani pake. Kama utani nilivyopoteza mtaji wangu wote kizembe

Huyu jamaa kama umemkumbuka kwenye ile story yeye na rafiki yake Agustino walivyoenda kwa mganga kutafuta utajiri utagundua kuwa huyu chalii ni mwandishi tu wa story na sio yaliyowahi kumkuta yeye.
Ata Kama Ni mwandishi tu Ila ili Jambo Lina ukwel kabsa wengi wapo hvyo
 
Hii hatua ya kupigika mpk unawaona boda boda na mama ntilie wanadhaman kuliko mimi imeshawahi kunipitia aisee, nilipigika hasa na degree yangu ya ualimu toka pale UDSM, Mungu hamtupi mja wake now ujasiriamali umeninyanyua toka nilipokuwa, now najihisi nina dhamani kuliko
Big up mkuu ,i wish tufahamiane tubadilishane madini
 
Mkuu kuna jamaa yangu mwaka 2018 aliingia kwenye ufugaji wa kuku wa mayai kichwa kichwa, akanunua kuku 3000, akakodi eneo akajenga mabanda ya kisasa na nyumba ndogo ya mlinzi, akaita taneso akawalipapesa nyingi wamvutie umeme fasta.
Mkuu jamaa alipoteza pesa ndefu sana na walekuku wote walikufa, yani alikula shoti ya zaidi ya milion 40, uwa nikimuuliza vipi ile project ananijibu acha usen** kwani wewe hujawahi fanya uwekezaji ukapoteza ela.
Hakupata mafunzo Interchick.
 
Hakupata mafunzo Interchick.
Alikuwa na jamaa flani ndiye kama mentor wake, alijitahidi kuleta wataalam wa kujenga mabanda ya kisasa, chanzo aliwapa kwa muda, yani alikuwa analeta wataalam na bado wakafa
 
Ndugu zanguni ni kosa kukopa ili ujenge nyumba yako ?
Mfano ulikuwa na pesa yako umepambana kwenye kujenga lakini pesa ikapelea ukaamua kukopa kama laki mbili ili ufanyie ujenzi wako . Umekopa na lengo lako nikulipa hiyo pesa kwa muda kadhaa na ukalipa hivi kunakuwa na shida ..
 
Ila wanawake watamu jamani...mie nilishajiamulia wacha tuu nizike hela yangu kwenye papuchi maana ndio raha ya dunia na hizo hela zenye nukifa nktaziacha tuu so bora nifurahie maisha kwa kugegeda papuchi
[SUP]😂😂😂😂😂😂[/SUP]
 
Ndugu zanguni ni kosa kukopa ili ujenge nyumba yako ?
Mfano ulikuwa na pesa yako umepambana kwenye kujenga lakini pesa ikapelea ukaamua kukopa kama laki mbili ili ufanyie ujenzi wako . Umekopa na lengo lako nikulipa hiyo pesa kwa muda kadhaa na ukalipa hivi kunakuwa na shida ..
Hapana mkuu, labda kama unaishi kwa kuwaangalia wao
 
Hii hatua ya kupigika mpk unawaona boda boda na mama ntilie wanadhaman kuliko mimi imeshawahi kunipitia aisee, nilipigika hasa na degree yangu ya ualimu toka pale UDSM, Mungu hamtupi mja wake now ujasiriamali umeninyanyua toka nilipokuwa, now najihisi nina dhamani kuliko
Una degeree ya ualimu na hujui kuandika
 
Natumai wote mnaendelea poa na miangaiko ya hapa na pale.

Wataalam wa mambo wanasema umri wa kufanya makosa na kujifunza vitu mbali mbali ni ule ambao bado mtu yupo kijana maana ni umri ambao unaweza kusahihisha makosa na kurudi kwenye mstari

Kwakweli mimi kama kijana kuna makosa mengi sana ambayo nimesha yafanya ambayo kuna muda nikikaa huwa nawaza nasema pengine nisinge fanya ule ujinga pengine ningekuwa mbali sana kiuchumi lakini ndio unakuta opportunity imeshapita.

Kwa kweli huwa muda mwingine nakaa nafikiria wale wazee ambao umri umeenda na wako bado kwenye umasikini wa kutupwa sipatii picha maumivu ya majuto walionayo maana unakuta umri umeenda hawawezi tena kupindua meza

Sasa kuna kisa ambacho kimenisukuma kuandika huu uzi , kama mnavyo fahamu maisha ya jiji la dar es salaam kwa wale ambao hawana ajira rasmi na pia hawana mitaji mikubwa ya kufanya biashara maisha yao yanavyokuwa, unakuta ni kuangaika sana kama kuku wa kienyeji na kazi ndogo ndogo ili mkono uende kinywani na ulipe bili kama maji na umeme.

Kuna siku rafiki yangu mmoja alinipigia simu akaniambia njoo makumbusho karibia na stand kuna dili la maana litanifaa niachane na mambo ya uchinga niliokuwa nafanya ilala boma .

Kweli nilienda nikakutananae akanipeleka kwa jamaa yake flani akaniambia huyu rafiki yangu amabahatika kupata kazi sasa anauza hii sehemu yake ya biashara kama nitakuwa na pesa aniuzie maana mzunguko wa biashara pale ulikuwa mzuri.

Jamaa alikuwa amechongesha banda kubwa sana la kisasa alikuwa anauza juisi za matunda pamoja na kupaki matunda ndani ya hilo banda alikuwa na freezer kubwa, friji moja ndefu, blender za kisasa na vitu vingine vidogo vidogo,mbele kaweka banda la chips na mishikaki pia mpesa kazi alikuwa anapiga hadi saa 6 usiku .

Vitu vyote alikuwa anataka million 2 kuanzia banda hadi vifaa hapo mfukoni nilikuwa na shillingi laki mbili tu, ikabidi niongee na yule jamaa yangu kama anaweza kunikopesha kiasi kadhaa kweli alikubali kuniongezea laki 4 nije nimrudishie laki 4.5

Baada ya mazungumzo tulielewana baada ya wiki nitampelekea ile pesa maana ilibidi nitafute kama millioni 1.4 ili itimie 2 million. Wakati narudi nimepanda kwenye daladala nikaanza kujilaumu na kumlaumu mungu nitapata wapi mtaji nikachukue ile sehemu kiukweli mawazo yalikuwa mengi sana lakini sikupata jibu wapi nitatoa 1.4m

Baada ya siku kama 3 nikapiga dili kwenye maswala haya ya upatu kwa bahati nikapata kama million 5 hapo ndio akili ikapotea kichwani .kumbuka hapo jamaa yangu yule alikuwa kakubali kunipa laki 4, mm nilikuwa tayari na laki 2 ilikuwa kwenye ile pesa nilioipata nilikuwa natakiwa kutoa 1.4 million ili nikamilishe kuchukua lile eneo.

Kiukweli akili yangu ilibadilika nikaona nikitoa ile pesa kuchukua ile sehemu nikama pesa yote itaisha, yaani nikawa naona kama naenda kudhulumiwa. Wazo nililolipata niakona nitoe pesa yote niitunze getto. Kisha nikampigia yule rafiki yangu nikamwabia amwabie yule mwenye eneo atafute mtu mwingine mimi jamaa niliokuwa natarajia anipe pesa amegoma.

Kiukweli baada ya kushika ile pesa mkononi niliiona ni nyingi mno zaidi ya millioni 5 mabunda manne ya elfu kumi kumi na mawilli ya elfu tano tano.

Uone sisi masikini tulivyowajinga kwanza shughuli nilizokuwa nafanya ilala boma pale nikasitisha nilikuwa mvivu balaa maana ile kazi nilikuwa nawahi saa 9 hadi saa kumi asubuhi nikaona kama nauchosha mwili bure.

Nikaacha kabisa kwenda kufanya kazi kule ilala , kaziniliokuwa nafanya nikula kucheki gemu za mpira mixer, mieleka tamthilia, nilikuwa sitoki njee nikitoka asubuhi naenda kuchukua tray nzima ya mayai kila siku nakaanga mayai 10, maziwa yale fresh ya asas kila siku nachukua mifuko miwili. Matunda yalikuwa hayakauki getto, mikate, juice zile za Ceres ndio yalikuwa maji yangu ya kunywa.

Pale riverside kuna mama mchaga anafuga kuku wa kisasa kila siku nilikuwa nimeweka order kuku mzima ananitengenezea kabisa kisha ananiletea nakaanga vyakula vilijaa getto ikabidi ninunue kale ka friji kadogo kabisa used boss laki na hamsini nikawa natunza mazaga zaga humo.

Pale riverside sehemu ya starehe iliozoeleka ni mikasa kila siku nilikuwa naenda kula raha pale usiku kisha naondoka na demu napeleka getto .

Akili yangu ilikuwa kama imeruka kuna siku nilikuwa nalala naamka hata saa 7 usiku kutoka usingizini najiandaa naingia bar kunywa pale mikasa yaani kwa muda mfupi wahudumu wa pale wakanizoea maana mm kila siku kuanzia J3 hadi jpili sijui usiku wa kareoke vyote nilikuwa nahudhuria kisha nikiona demu mkali lazima nijikoshe na vipesa kisha niondeke nae.

Ikifika asubuhi kabla demu hajaondoka namwambia atoe kuku kwenye kale ka freezer akaange mixer mayai, maziwa kisha nampatia na pesa kisha ndio anaondoka.

Nakumbuka kunasiku nilikuwa counter nimekunywa kweli siunajua watoto wa dar walivyo mara akaja manzi flani akakaa karibu yangu bila kuuliza nikaanza kumnunulia bia kunywa sana bia zangu na unajua mule ndani bia yenye bei ndogo kabisa 3000 . Nakambuka niliondokanae kufika getto kumbe ni malaya aliekubuu ananiambia kabla ya kila kitu naomba changu kabisa.

Asee nilikasirika sana kwa ile kauli nilifungua begi kwa hasira nikatoa burungutu moja la million moja nikahesabu elfu 30 mbele yake nikamwambia chukua kisha usepe na hapo huyo manzi alikuwa ameomba 20k.

Yaani kiukweli zile pesa zilinipa kiburi kuna demu mmoja slay queen amekula sana pesa zangu pale Mcity piza heat, nilimmnunlia hadi samsung A30

Kiukweli nilifanya mambo mengi ya kufuja pesa yaani sitaki kukumbuka maana nilikuwa sipigi hesabu nilikuwa naingiza mkono nachukua burungutu lolote sitoi hata labberband navuta tu noti kadhaa mpaka kunasiku noti kama 3 ziichanika

Siku akili yangu ilirudi kukaa sawa niliingiza mkono kwenye lile begi nikakuta kuna labberband nyingine hazina kitu kupiga hesabu nikakuta nimebaki kama na laki moja na elfu ishirini asee niliogopa, hapo ndio nikakumbuka mwezi unaokuja natakiwa kulipa kodi ya nyumba yaani nilichanganyikiwa .

Nalitawanya zile pesa zote ndani ya kama mwezi na nusu nikarudi sifuri yaani ilifika muda nikawa naongea mwenyewe barabarani wazo ndio likaniijia kwanini nisinge chukua lile eneo la biashara tena rafiki yangu alikuwa kajitolea kunisaidia .Nilikuwa nikitembea barabarani naona kila mtu kanizidi akili kuanzia boda boda, wale wanaouza maji pembeni ya barabara, sehemu za mpesa, hadi mamantilie

Nilichojifunza ukiona anapata pesa badala ya kuwekeza unaogopa unakaanayo ndani nakupa pole sana unauwezekano mkubwa wa kufa masikini. Masikini tunaogopa sana kuwekeza hapo ndio matajiri wanatuzidia.

Now mtu hanidanganyi nilivyosota hadi kukaa sawa nibora pesa yangu iteketee kwenye biashara kuliko kwenye mambo ya kijinga. Mfano bora anaewekeza kwenye jambo fulani mfano kilimo pesa ikapotea kuliko kuharibu kwenye mambo ya kihuni wote ndio watakuwa wamepoteza lakini kunautofauti mkubwa sana kati ya hao watu wawili

Ogoba sana wale jamaa wakatisha tamaa wekeza pesa yako kwenye biashara yoyote ilimradi umeona inaweza kulipa anaekukatisha tamaa anataka uharibu pesa kwenye mambo ya kujinga.

Pia nilichojifunza vitu ambavyo ni hatari kwa pesa za vijana wengi watafutaji cha kwanza upatu/gambling, wanawake, pombe, ukiangalia vizuri vyote vinaambatana na tamaa

Uzi tayari
Kinachotucost vijana wengi sisi wa kiafrika (ngozi nyeus) Ni nidhamu ya maisha.

Na Nidhamu inaanza kwny malezi,hatuzingatii vitu km afya,kutunza fedha na mengineyo.
 
Mpaka leo sijui nilikosea wapi mkuu, maana chanjo nilitumia kwa wakati tena kwa kumshirikisha doctor wa mifugo....usafi nilijitahidi,maji masafi sana muda wote na chakula kilikuwa cha kutosha maana nilikuwa nanunua hadi debe 6 na mashudu,chokaa,damu, mahindi yaliyobalazwa, mboga za majani na vitamin na vingine ila kuna kipindi magonjwa yalikuwa yanabeba kuku karibu 8 kwa siku....

nahisi kuku ilichukua muda kuja kuzoea mazingira nahisi maana niliwatoa kijijini sana wakikwa na miezi 2 hadi 3 kwa bei ya elfu 4 mmoja nikawaleta mjini tena nikawa nafungia bandani masaa 24....

Waliisha wote wakabakia kama 8 tu, ajabu sahizi muda ambao siwajali kabisa ndo wanakuja vizuri, maana hela ya pumba watage wasitage nawahudumia na dawa natumia za asili tu aloevera na nyingine, wamefika 29 sahizi na 6 wanalalia kwa mara nyingine hadi sasa....
Ndio uwekezaji mkubwa huu?
 
Back
Top Bottom