Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Aaaah vijana wana mambo, hiv wote tukiamua tusijenge nyumba za kuishi itakuwaje? Usiogope kujenga!
 
Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha.

Haya ni mawazo ya kishamba sana. Kwamba kununua huduma fulani ni kumtajirisha muuza huduma?

Mbona hutibu wanao nyumbani? Kama hutaki kumtajirisha mwenye hospital? Somesha wanao, usimtajirishe mwenye shule.

Usinunue vitu dukani au gengeni manake unawatajirisha wamiliki.

Hizi 'mentality' za kishamba mnatoa wapi?
 
Hata hao wahindi kwao wana nyumba wamejenga. Huwezi kuwa unaishi say Afrika Kusini ukafikiria kujenga huko. Utapanga na kufanya biashara au shughuli yoyote halali. Hii dhana ndio ipo kwa wahindi, hapa wahindi sio kwao. Kwa baadhi wenye fedha nyingi sana uwa wanajenga maeneo kama masaki, upanga n.k na wengi uwa wananunua apartment.

Halafu kujenga sio umasikini, kumiliki nyumba ni jambo bora sana katika maisha maana nyumba ni kitu ambacho kinakupa mengi sana ikiwepo kukupunguzia gharama za kodi, kukuondolea stress za kutokuwa na kwako na pia hata ukipata tatizo la kiuchumi unakuwa na pa kuanzia.

Nyumba ni kitu ambacho hata ukiondoka duniani ghafla familia yako inakuwa na sehemu ya kuanzia kuliko ukiwa huna nyumba.

Nyumba ni muhimu katika ukuaji wa miji na Taifa kwa ujumla. Unavyoona nje yale majengo ni kwamba watu wamewekeza ndio maana kunapendeza. Na sisi tujenge majengo kukuza nchi yetu. Tuachane na wahindi wale hapa sio kwao ndio maana hawajengi. Tena si wahindi tu hata wazungu hawajengi hapa kwa kuwa si kwao hapa watachuma tu ila kujenga wataenda jenga kwao
Unaweza waachia wanao biashara zilizosimama. Wakazidi kuingiza kipato.

Ukiwaachia nyumba wanaweza kuiuza, wakapata mtaji, wakaenda zao kupanga.
 
Hii ni tofauti sana mzee. National housing nyumba bei nafuu(bora kupanga kuliko kujenga) mfano nchi zilizoendelea hakuna viwanja vya bei powa.

Hata hivyo sheria za ujenzi ni kali kuliko za Tanzania, yani huwezi kujenga bila kibali,bila ramani, bila mpango yan ukipiga hesabu ya ujenzi unaona bora ukapange. Tanzania kujenga ni nafuu kuliko kupanga, kupanga kero nyingi kuliko kuishi kwako. Bora kujenga kuliko kukuza biashara sababu pesa inaweza kufia huko na pesa ya pango ukakosa vile vile.
Watu wa mbele wapo flexible and mobile.

Hataki akiondoka huo mji aache mzigo nyuma, ndo maana hata matajiri nao wanapanga.
 
Kodi ya nyumba ni kati ya vitu vinavyotafuna mtaji wa biashara kuliko maelezo..umepanga nyumba ya wastani ya laki nne kila mwezi. Kutoa kiasi hiki kama kodi ya nyumba toka kwenye pato la biashara ni pesa nyingi sana. Usipokuwa makini unaweza ukayumba hata kibiashara. Kumbuka bado biashara ina gharama zake za uendeshaji ikiwemo kodi ya ofisi, mishahara, etc.

Usipo kuwa makini utajikuta milioni inachomoka kila mwezi kwaajili ya kodi pekee.....haina afya kibiashara.

Kingine ni swala la kukopesheka na taasisi za fedha. Biashara haiwezi kusimama bila mikopo, na hakuna mkopo bila dhamana. Siku hizi hawapokei tena eneo lisiloendelezwa kama dhamana ya mkopo. Wanahitaji nyumba. Huna nyumba utatumia muda mwingi sana kusimama kibiashara.

Vijana jengeni....nyumba ni asset.
Kama unajifahamu una biashara ambayo ukitoa 400K kwa mwezi kwa ajili ya kodi inayumba, katafute nyumba ya 150K.
 
Wale mawizara waliohamia Dodoma toka Dar wakajenge nyingine Dodoma?
Mkuu hizo wizara zimehamishiwa huko moja kwa moja na wao mikataba yao ni permanent and pensionable terms hivyo watafanya kazi huko mpaka kustafu kwao hapo kwanini wasijenge tena huko kama uwezo unaruhusu?

Alafu mtu aliyezoea kukaa kwenye nyumba yake binafsi huwa anaona shida sana kukaa kwenye nyumba ambayo siyo yake hata kama ni serikali, navyokwambia hivi kuna watumishi kibao tayari wameshajenga huko Dom!
 
[emoji16][emoji16][emoji16]acha kupotosha watu sisi dar tuna nyumba zaidi ya 4 lakin upiga kwa mwaka hela tunayo chukua si chini ya milion 16 na nikufumbue katika biashara ambayo haina hasara ni nyumba ni bonge la biashara watu kila siku wanakuwa wanahitaji kuishi maisha yao hapo kwenye nyumba bado ujaja kwenye hustle zetu wenywe huku tumetulia tunajua nyumba zipo miezi ikifika hela zinaingia ila upate mpangaji mzuri anae lipa kodi kwa wakati siyo kichefu chefu wa kupiga calenda
Lakini umesoma alichoandika mtoa mada soma tena umekurupuka vibaya.
 
Assets: kitu kinachoingiza pesa mfukoni mwako mfano ardhi, shamba
liability:kitu kinachutoa pesa mfukoni kwako mfano nyumba ya kuishi gari la kutembelea ni liability


source: financial IQ kutoka kwa robert kiyosaki
According tu Kiyosaki sio? hiyo inabaki kuwa ni falsafa yake na wafuasi wake akiwemo mm ila kamwe haiwezi kuwa maana halisi ya asset au liability
 
Babu zetu walijenga nyumba za kulala, baba zetu wamejenga nyumba za kulala na sisi tunaendelea kurithi akili ile ile, japo pamoja na kuona hali ngumu ya hao wazazi waliokuwa wanamiliki hizo nyumba bado tunakosa ubunifu. Huwezi sikia mtu anawaza kuanzisha kampuni au investment endelevu.

Yaani mtanzania akiugua mwaka Kwisha habari yake kwa sababu anategemea active income badala ya passive income. Ukiugua au ukafukuzwa kazi nyumba ya kulala itakulisha? Au utakuwa ombaomba.
Wachache sana wana elim hio, angalia wanavyobisha kwenye huu uzi,
 
Nauliza hivii ukipanga utaweza kulima tu matuta tutatu twa tembele na tukibanda twa kuku 40?

Tuachee!!.
 
Wewe unadhani ni sababu ipi inayosababisha wajenge nyumba kwanza kabla ya kuwekeza?
 
Ni mimi tu nadhani ndo sielewagi na sitoweza.
Yaani nipate pesa... niwekeze kwa biashara...biashara ichanganye vizuri inilipe...niwe na pesa nzuri....halafu nikajibanze kwenye national housing maisha yangu yote?Loh!
 
Maisha hayana formula, na kila mmoja anatafuta ile furaha halisi katika maisha yake. Kile kinachokuletea wewe furaha siyo sawa na kile kinachomletea mwingine furaha.

Kila mmoja Mungu alimuumba kwa namna yake. Lakini pia njia ya kuifikia furaha kamwe usitegemee kuwa sawasawa kwa asilimia mia na ya mwingine.

Maisha ni kama kurasa za vitabu, tatizo wengi wanaamini kuwa kurasa zake ni sawa na kurasa za watu wengine kwasababu wote wapo katika tabaka fulani au wote ni wanadamu na ni kama utofauti hawauoni.

Tuongee ukwel, huwezi fanikiwa kama hujijui wewe mwenyewe kuanzia ndani, madhaifu yako huyajui, uimara wako hauutambui na wewe mwenyewe unaishi kwa kuangalia akina nani wanafanya nini.

Wengi tunaishi maisha ya mkumbo na wachache wanaoishi maisha yao wao kama wao.

Suala la kujenga na kuazisha biashara yote ni ya msingi lakini kutokana na utofauti uliopo siyo lazima wote tuamini kuwa ni lazima kujenga kisha ndo biashara , au ni lazima biashara kisha baadae huko ndo kujenga. Tuelewe malengo ya watu hutofautiana na mitazamo pia hutofautiana.

Umasikini unaanziaga kwenye fikra za mtu na ndiyo maana lazima uwe na uelewa wa wewe mwenyewe kujua uko vipi, vipao mbele vyako ni vipi, wapi uko vizuri, wapi haupo vizuri.

Kujifunza ni muhimu maana huwa inakuamsha kuanza kujihoji juu ya nini ufanye, ila fanya kile ambacho wewe utaweza wajibika kama likitokea lolote, yaani ukianzisha biashara na kuikuza huku unaishi nyumba za kupanga kubaliana n hali yoyote itakyojitokeza kwenye biashara na hata mazingira unayoishi pia.

Lakini kama ukiamua kujenga kisha ndo biashara pia kubaliana na hali.

Pokea ushauri wowote ule ila kuwa muamuzi wa mwisho bila kujali kipi wengi au wachache wanakiamini.
 
Je, ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako.
Kujenga pia ni kutajirisha mafundi na watu wa hardware... Jenga ila kama tayari umeridhishwa na kipato chako na tayari umri umeenda kidogo. Ninavyoona kama una chini ya miaka 35 hamna haja ya kutumia rasilimali kujenga na badala yake lenga kuwa na kipato kikubwa zaidi
 
Kodi ya nyumba ni kati ya vitu vinavyotafuna mtaji wa biashara kuliko maelezo..umepanga nyumba ya wastani ya laki nne kila mwezi. Kutoa kiasi hiki kama kodi ya nyumba toka kwenye pato la biashara ni pesa nyingi sana. Usipokuwa makini unaweza ukayumba hata kibiashara. Kumbuka bado biashara ina gharama zake za uendeshaji ikiwemo kodi ya ofisi, mishahara, etc.

Usipo kuwa makini utajikuta milioni inachomoka kila mwezi kwaajili ya kodi pekee.....haina afya kibiashara.

Kingine ni swala la kukopesheka na taasisi za fedha. Biashara haiwezi kusimama bila mikopo, na hakuna mkopo bila dhamana. Siku hizi hawapokei tena eneo lisiloendelezwa kama dhamana ya mkopo. Wanahitaji nyumba. Huna nyumba utatumia muda mwingi sana kusimama kibiashara.

Vijana jengeni....nyumba ni asset.
Umejenga kwa kutumia milioni 30 hiyo ni milioni 30 imetoka kwenye mtaji wa biashara. Na huo mstari wa nyumba unayoishi ni asset umeoitwa na wakati. Tujifunze kuwa asset ni kitu kinachokuongezea thamani kila mwezi. Hiyo ndio maana halisi. Kama umejenga kwa pesa yako cash, bado nyumba unayoishi ina gharama za umeme, maji na maintainance. Ni liability na sio asset. Wale wenye mikopo ndio zaidi wana marejesho. Angalau aliejenga kwa ajili ya kupanfisha anaweza kusema nyumba yake ni asset
 
Kwahiyo wewe mbuzi, sisi tuache kuishi maisha yetu kama watu weusi "tuanze kukopi kila kitu, kila lifestyle ya Mhindi???
Kizuri kichukue kibaya achana nacho. Wahindi ni katika watu wenye mafanikio makubwa katika kurithisha watoto wao mali zao tena na tena. Ni kwa sababu wanajua jinsi ya kuitumia pesa kuongeza ziwe zaidi bila anasa. Somo hilo litakufaa wewe na hata wanaokuja baada yako
 
Back
Top Bottom