Mkuu Siku zote maisha huwa hayana formula, unaweza ukamuiga muhindi nawewe ukaacha kujenga,, hako ka hela ukakasukumia kwenye biashara kakafia hukohuko ukakosa vyote,, mwisho wa siku mwenye pango lake akakutimua. Fanya kile unachoona kinafaa kwenye maisha yako, Acha kuiga. Unaweza ukakuta huyo huyo muhindi wako amepanga kumbe Kule kwao ameacha mijengo yake na yeye amepangisha, kila mwezi anatumiwa kodi ndio maana unamuona hateteleki. Au Kule kwao ana miradi na mingine huwa wanamtumia pesa, ndio maana hateteleki. Sasa wewe iga tu kama haujajipanga au hauna hata plan b, utacheza segere pale biashara yako itakapokuwa mochwari na mwenye nyumba anataka chake, wakati huo watoto wanataka ada.