Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Aaaah vijana wana mambo, hiv wote tukiamua tusijenge nyumba za kuishi itakuwaje? Usiogope kujenga!
 
Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha.

Haya ni mawazo ya kishamba sana. Kwamba kununua huduma fulani ni kumtajirisha muuza huduma?

Mbona hutibu wanao nyumbani? Kama hutaki kumtajirisha mwenye hospital? Somesha wanao, usimtajirishe mwenye shule.

Usinunue vitu dukani au gengeni manake unawatajirisha wamiliki.

Hizi 'mentality' za kishamba mnatoa wapi?
 
Unaweza waachia wanao biashara zilizosimama. Wakazidi kuingiza kipato.

Ukiwaachia nyumba wanaweza kuiuza, wakapata mtaji, wakaenda zao kupanga.
 
Watu wa mbele wapo flexible and mobile.

Hataki akiondoka huo mji aache mzigo nyuma, ndo maana hata matajiri nao wanapanga.
 
Kama unajifahamu una biashara ambayo ukitoa 400K kwa mwezi kwa ajili ya kodi inayumba, katafute nyumba ya 150K.
 
Wale mawizara waliohamia Dodoma toka Dar wakajenge nyingine Dodoma?
Mkuu hizo wizara zimehamishiwa huko moja kwa moja na wao mikataba yao ni permanent and pensionable terms hivyo watafanya kazi huko mpaka kustafu kwao hapo kwanini wasijenge tena huko kama uwezo unaruhusu?

Alafu mtu aliyezoea kukaa kwenye nyumba yake binafsi huwa anaona shida sana kukaa kwenye nyumba ambayo siyo yake hata kama ni serikali, navyokwambia hivi kuna watumishi kibao tayari wameshajenga huko Dom!
 
Lakini umesoma alichoandika mtoa mada soma tena umekurupuka vibaya.
 
Assets: kitu kinachoingiza pesa mfukoni mwako mfano ardhi, shamba
liability:kitu kinachutoa pesa mfukoni kwako mfano nyumba ya kuishi gari la kutembelea ni liability


source: financial IQ kutoka kwa robert kiyosaki
According tu Kiyosaki sio? hiyo inabaki kuwa ni falsafa yake na wafuasi wake akiwemo mm ila kamwe haiwezi kuwa maana halisi ya asset au liability
 
Wachache sana wana elim hio, angalia wanavyobisha kwenye huu uzi,
 
Nauliza hivii ukipanga utaweza kulima tu matuta tutatu twa tembele na tukibanda twa kuku 40?

Tuachee!!.
 
Wewe unadhani ni sababu ipi inayosababisha wajenge nyumba kwanza kabla ya kuwekeza?
 
Ni mimi tu nadhani ndo sielewagi na sitoweza.
Yaani nipate pesa... niwekeze kwa biashara...biashara ichanganye vizuri inilipe...niwe na pesa nzuri....halafu nikajibanze kwenye national housing maisha yangu yote?Loh!
 
Maisha hayana formula, na kila mmoja anatafuta ile furaha halisi katika maisha yake. Kile kinachokuletea wewe furaha siyo sawa na kile kinachomletea mwingine furaha.

Kila mmoja Mungu alimuumba kwa namna yake. Lakini pia njia ya kuifikia furaha kamwe usitegemee kuwa sawasawa kwa asilimia mia na ya mwingine.

Maisha ni kama kurasa za vitabu, tatizo wengi wanaamini kuwa kurasa zake ni sawa na kurasa za watu wengine kwasababu wote wapo katika tabaka fulani au wote ni wanadamu na ni kama utofauti hawauoni.

Tuongee ukwel, huwezi fanikiwa kama hujijui wewe mwenyewe kuanzia ndani, madhaifu yako huyajui, uimara wako hauutambui na wewe mwenyewe unaishi kwa kuangalia akina nani wanafanya nini.

Wengi tunaishi maisha ya mkumbo na wachache wanaoishi maisha yao wao kama wao.

Suala la kujenga na kuazisha biashara yote ni ya msingi lakini kutokana na utofauti uliopo siyo lazima wote tuamini kuwa ni lazima kujenga kisha ndo biashara , au ni lazima biashara kisha baadae huko ndo kujenga. Tuelewe malengo ya watu hutofautiana na mitazamo pia hutofautiana.

Umasikini unaanziaga kwenye fikra za mtu na ndiyo maana lazima uwe na uelewa wa wewe mwenyewe kujua uko vipi, vipao mbele vyako ni vipi, wapi uko vizuri, wapi haupo vizuri.

Kujifunza ni muhimu maana huwa inakuamsha kuanza kujihoji juu ya nini ufanye, ila fanya kile ambacho wewe utaweza wajibika kama likitokea lolote, yaani ukianzisha biashara na kuikuza huku unaishi nyumba za kupanga kubaliana n hali yoyote itakyojitokeza kwenye biashara na hata mazingira unayoishi pia.

Lakini kama ukiamua kujenga kisha ndo biashara pia kubaliana na hali.

Pokea ushauri wowote ule ila kuwa muamuzi wa mwisho bila kujali kipi wengi au wachache wanakiamini.
 
Je, ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako.
Kujenga pia ni kutajirisha mafundi na watu wa hardware... Jenga ila kama tayari umeridhishwa na kipato chako na tayari umri umeenda kidogo. Ninavyoona kama una chini ya miaka 35 hamna haja ya kutumia rasilimali kujenga na badala yake lenga kuwa na kipato kikubwa zaidi
 
Umejenga kwa kutumia milioni 30 hiyo ni milioni 30 imetoka kwenye mtaji wa biashara. Na huo mstari wa nyumba unayoishi ni asset umeoitwa na wakati. Tujifunze kuwa asset ni kitu kinachokuongezea thamani kila mwezi. Hiyo ndio maana halisi. Kama umejenga kwa pesa yako cash, bado nyumba unayoishi ina gharama za umeme, maji na maintainance. Ni liability na sio asset. Wale wenye mikopo ndio zaidi wana marejesho. Angalau aliejenga kwa ajili ya kupanfisha anaweza kusema nyumba yake ni asset
 
Kwahiyo wewe mbuzi, sisi tuache kuishi maisha yetu kama watu weusi "tuanze kukopi kila kitu, kila lifestyle ya Mhindi???
Kizuri kichukue kibaya achana nacho. Wahindi ni katika watu wenye mafanikio makubwa katika kurithisha watoto wao mali zao tena na tena. Ni kwa sababu wanajua jinsi ya kuitumia pesa kuongeza ziwe zaidi bila anasa. Somo hilo litakufaa wewe na hata wanaokuja baada yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…