Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Uko sawa kabisa, ulifanya vizuri sana, Nyumba ya kupanga ni asset,
Uko sahihi kabisa nyumba ya kupangisha ni Asset sababu ina generate income lakini nyumba ya kuishi ya kulala tu na kuamka ni liability sababu hai generate income pia gari ya kukodisha kama taxi ni Asset lakini ya kutembelea tu ni Liability hata iwe benzi au prado
 

Una hoja. Changamoto ni ya mfumo/utamaduni mzima wa maisha yetu. Wakati unasoma, kijiji kizima kinasubiri umalize, umchukue mtoto/watoto wa kijijini uwasomeshe/uishi nao.
Kila mwezi utume pesa..
Kiasi kinachobaki ni kidogo, inakuchukua muda mrefu kukusanya mtaji.. BTW, mtaji wenyewe haukusanyiki.
Kuna mengi ya kuandika but All in all, hoja yako ina mashiko sana.
Tukiweza kufikia huko, itatusaidia mno.
 
hajakamilika MWANAUME bila kuwa na hivi vitu
Familia
Nyumba
Usafiri
Hapo penye usafiri pia panachangia kuongeza umaskini mtu aweza kuwa mtumishi wa umma au sekta binafsi kazi yake ni ndani ya jiji au mjini tu anaishi hapo hapo mjini toka nyumbani hadi kazini hazifiki hata Kilomita 20 ananunua iwe kwa mkopo au cash gari Vx Landruser la milioni 240 !! Kuwa nini asinunue gari ya kawaida ya milioni 40 halafu milioni Mia 210 akawekeza?
 
Kuanza biashara badala ya nyumba kunahitaji uwe na mkataba na Mungu. Maisha yenyewe haya leo upo kesho haupo, familia unaiacha kwenye chumba cha kupanga unaona simple eeh!!??
 
Umejenga wewe?
 
Nyumba inakupa utambulishi yaani hata watoto wanakuwa na mahali pa kujivunia wakiwa wakubwa.
 
Umasikini wa watanzania sababu kubwa ni CCM
 
Umasikini wa Watanzania chanzo chake kinajulikana, ni CCM.
 
Kujenga sio tatizo , tatizo linakuja ni kujenga Kwa hela ya Kula , ...hiii kitu inakera Sana , unakuta mtu watoto wanakula michicha na ugali kisa Baba anadunduliza hela ya kujenga , huu ni upopoma wa Hali ya juu Sana , hela ya kujenga inakujaga Tuu unajenga Kwa step zinazoeleweka , kiwanja+ Msingi+ boma + kupaua+ madirisha na milango + rangi n.k lakn hii ya kujenga tofali mistari miwili rangi fulan mistar miwili rangi nyingine , nyumba ishabadilishiwa mafundi Zaid ya kumi kisa delay of money , mi hapana kabisa
 
Kuanza biashara badala ya nyumba kunahitaji uwe na mkataba na Mungu. Maisha yenyewe haya leo upo kesho haupo, familia unaiacha kwenye chumba cha kupanga unaona simple eeh!!??
Unaposema utawaacha kwenye chumba cha kupanga ?una maana gani wewe waxazi unaishi kwa wazazi wako? Wazazi wako kama walipojenga walisema kuwa Watoto tudijrlewaacha chumba cha kupanga imekula kwao wewe kuishi kwao ina maana hiyo pesa wamechexea mlengwa haupo

Kumbuka Watoto wanakua migorofa kibao watu walijenga hata kwa kuiba kwa mentality hiyo mfano Dar es salaam sasa hivi Watoto wao wakubwa wako mikoa mbalimbali na maisha yao majengo vimebaki vizee mtu na mkewe tu vyumba vingine wanalala panya na ghorofa halipangishiki!!!

Hivi mfano aliyefariki akiwa na nyumba yake akaachia familia nyumba na mwingine aliyefariki akawa mpangaji akaachia familia biashara iliyosimama vizuri huoni huyo aliyewaamchia biashara kufanya jambo la maana kuliko huyi aliyewaachia nyumba ya kulala na kuamka? Kama hawana maisha watakula na kuvaa hiyo nyumba ya kulala na kuamka? Mtu kufariji unatakiwa kuacha asset zinazoingiza kipato sio tu ohh nimewaachia familia mali swali hiyo mali ina nini cha maana hata liwe ghorofa ujidai kuwa umewaachia urithi? Njaa ikiwabana hilo ghorofa wataliotroka na kukulaani kwa hukuwekeza kwenye biashara ukamwaga pesa zote kwenye ghorofa ukawaacha wanahangaika maisha hata bili za maji na umeme wanashindwa kulipa
 
Ndio nyumba za kutosha na ninaendelea kuzijenga
Kama uyasemayo ni kweli, elewa kuwa mahesabu yanakupiga chenga Mkuu. Huwezi kujenga nyumba ukapangisha ukapata utajiri. Nitakupa mfano. Nyumba za NHC huko Dodoma zinauzwa Million 78. Hizo nyumba zinapangishwa kwa 350,000/=.

Kwa mantiki hiyo mmiliki atasubiri miezi 223 kurejesha hela yake! Ambayo ni miaka 19. Wakati huo huo lazima kila baada ya miaka 5 ifanyike repair na akisubiri ifike miaka 10 itakuwa imekula kwake.

Kimahesabu Chumba na sebule Dar ni gharama ya million 10 kukijenga hadi mtu kuingia ndani kimekamilika. Kodo yake ni laki moja. Hivyo ni kama miaka 9 kikiwa na wapangaji utarudisha hela yako. Je, hii ni biashara kweli au biashara kichaa. Jioni njema
 
Nyumba inakupa utambulishi yaani hata watoto wanakuwa na mahali pa kujivunia wakiwa wakubwa.
Hivi Watoto wakiwa wakubwa watajivunia lkipi Kati ya nyumba ya mzazi wao au biashara ya mzazi ?

Ulishasikia Watoto wa Reginald Mengi wanajivunia nyumba ya mzazi wao? Wanajivunia biashara sio nyumba

ulishasikia Watoto wa Bakheresa wanajivunia nyumba ya mzazi wao ? Wanajivunia biashara

Wewe unajivunia nyumba ya mzazi wako?
 
Halafu ukiwa nyumbani kwako hata mwendo unabadilika,,

Sijuwi kwann?
Hahaaaa ukiwa kwako unapata usingizi mzuri huko kupanga wenye nyumba wengi wachawi full kuota mauza uza. Kibongo bongo nyumba ni muhimu hata ukikosa msosi utakunywa uji kuliko usiwe na Kodi utalala nje, tusijifanye kuiga wahindi kwao ni india aisee
 
Sihitaji kuwa tajiri mimi ni mtumishi wa Serikali. Nina biashara kubwa Kariakoo na Mlimani City pia nina nyumba za kupangisha pamoja na mashamba na mifugo. Kwa upande wangu naona nimefanikiwa kwani nina uhakika ni watanzania wachache wenye maisha kama yangu.

Ninaijua biashara nina uhakika zaidi yako. Kabla awamu hii nimeenda China mara 17 kibiashara. Na kwangu mimi biashara ya nyumba ndio ina uhakika mkubwa wa mapato kuliko zote kwani haina supervision kubwa na haikuathirika na corona wala Kodi za TRA
 
Unaangalia mambo juu juu sana na huu mfano wa Mengi ndio ovyo kabisa. Kwenye biashara wale wamerithishwa share na hata me nikifa wanangu watarithi mali zangu ziwe nyumba au biashara na mashamba
 
Hahaaaa ukiwa kwako unapata usingizi mzuri huko kupanga wenye nyumba wengi wachawi full kuota mauza uza. Kibongo bongo nyumba ni muhimu hata ukikosa msosi utakunywa uji kuliko usiwe na Kodi utalala nje, tusijifanye kuiga wahindi kwao ni india aisee
Hakika kabisa mkuu.
 
Correct ✓ 100%
 
Unaangalia mambo juu juu sana na huu mfano wa Mengi ndio ovyo kabisa. Kwenye biashara wale wamerithishwa share na hata me nikifa wanangu watarithi mali zangu ziwe nyumba au biashara na mashamba
Biashara ziko za juu za Kati na za chini kutegemea uwezo mtoto atajivunia hiyo biashara inayoendana na uwezo wa mzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…