Umaskini wa watu wengi hapa nchini umesababishwa na ujinga au upumbavu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!
Samahani kama haya maneno "ujinga na upumbavu " vitakukwaza.

UJINGA ni hali ya mtu kukosa ujuzi, elimu au taarifa fulani muhimu ambayo ingemsaidia kutatua changamoto za kwake au za jamii yake.

Huku UPUMBAVU ni hali ya mtu kushindwa kutumia elimu, maarifa au ujuzi aliona ili kutatua changamoto za kwake au za jamii yake.

Sasa kijana mwenye degree anapokuja mjini kutafuta ajira ambayo angeweza kuitafuta kwa njia ya simu yake akiwa kijijini ambako halipii kodi ya nyumba, halipii kodi ya maji na maeneo ya kufanyia ujasiriamali halipii, hapo tunasema huyo kijana ni mpumbavu.

Hivi mnajua kuwa laki moja kijijini unapata kuku matetea 8 na jogoo 2 jumla kumi.
Miti ipo kichakani.
Kijana anaweza kusubiri ajira huku akianza na ufugaji wa kuku kumi.

Hapo ananunua chanjo ya elfu 8 anawachanja anasubiri kuvuna kuku mia moja baada ya miezi michache.

Kijijini kuku wa kienyeji wanajitafutia chakula, siku ukipata elfu 2 -5 unaweza kuwanunulia pumba imetoka.

Kuku kumi ndani ya mwaka mmoja kijana una kuku wengi.

Ukiuza kuku 50 unapata pesa ambayo utajenga zizi la kisasa na kununua mahitaji yako muhimu.

Baada ya miaka 3 kama utazingatia chanjo, dawa muhimu na vyakula muhimu umetoka kimaisha.

Dili sio kuku tu, kuku nimechukulia mfano kwakuwa ninafuga, naongea kitu ninachokifahamu.
 
Mkuu, hii nchi bado inapambana na wale maadui watatu toka uhuru:

1. Ujinga
2. Umasikini
3. Maradhi.

Wewe kama umeshafanikiwa kuwashinda hao maadui 3 (ambao naamini utakuwa umeushinda Umasikini tuu ila ujinga na maradhi bado) basi wasaidie na wengine kuwashinda hao maadui pia.

Kama ushindi wako dhidi ya hao maadui 3 bado haujakusaidia kulijua hili basi nawe bado umo humohumo kwenye kundi ambalo bado linashindana na hao maadui.

Be Humble.
 
Chukua hii itakusaidia maana una safari ndefu pia

Habari!
Samahani kama haya maneno "ujinga na upumbavu " vitakukwaza.
UJINGA ni hali ya mtu kukosa ujuzi, elimu au taarifa fulani muhimu ambayo ingemsaidia kutatua changamoto za kwake au za jamii yake. Huku
UPUMBAVU ni hali ya mtu kushindwa kutumia elimu, maarifa au ujuzi aliona ili kutatua changamoto za kwake au za jamii yake.
Sasa kijana mwenye degree anapokuja mjini kutafuta ajira ambayo angeweza kuitafuta kwa njia ya simu yake akiwa kijijini ambako halipii kodi ya nyumba, halipii kodi ya maji na maeneo ya kufanyia ujasiriamali halipii, hapo tunasema huyo kijana ni mpumbavu.
Hivi mnajua kuwa laki moja kijijini unapata kuku matetea 8 na jogoo 2 jumla kumi.
Miti ipo kichakani.
Kijana anaweza kusubiri ajira huku akianza na ufugaji wa kuku kumi.
Hapo ananunua chanjo ya elfu 8 anawachanja anasubiri kuvuna kuku mia moja baada ya miezi michache.
Kijijini kuku wa kienyeji wanajitafutia chakula, siku ukipata elfu 2 -5 unaweza kuwanunulia pumba imetoka.
Kuku kumi ndani ya mwaka mmoja kijana una kuku wengi.
Ukiuza kuku 50 unapata pesa ambayo utajenga zizi la kisasa na kununua mahitaji yako muhimu.
Baada ya miaka 3 kama utazingatia chanjo, dawa muhimu na vyakula muhimu umetoka kimaisha.
Dili sio kuku tu, kuku nimechukulia mfano kwakuwa ninafuga, naongea kitu ninachokifahamu.
Bila shaka degree yako ni ya mchongo.

Nimekuja mbio kufuata madini, cha ajabu nakutana na pumba.

Futa uzi, yani hapa umetapika.
 
Back
Top Bottom