Kilemakyaaro
JF-Expert Member
- Jul 19, 2016
- 5,051
- 5,104
Leo asubuhi nimemleta mtu hapa UDOM kuhudhuria Usaili wa kazi za Utumishi, hakika watu ni wengi. Binafsi nliyemleta ameitwa kwenye Usaili wa nafasi za National Audit, only 10 kama sio 20 nafasi lkn wameitwa watu sio chini ya 3400, yaani watu hao ndio wapatikane only 20 people. Kibaya zaidi wameitwa watu waliosoma Business Administration lkn wamefika wakaaambiwa hawana sifa.
Sasa unajiuliza kama hawakua na sifa waliwaita vipi? Hizo garama alizotumia kuja hapa Dodoma atalipwa na nani? Kuna dada kwa Mfano katokea Ifakara, anasema kaja kwa malori na kaingia Dodoma saa 8 za usiku then amekataliwa kufanya usaili eti kasoma Business Administration, kwakweli Inauma na inakera mnoo.
Kingine nnaomba kufaham ikiwa watu wa Utumishi wananufaika vip na hizi Interview maana haiingii akilini wanaohitajika kua 10 au 20 unaita watu 3600 kwenye usaili. Yaan hawana njia ya kuwachuja japo basi waitwe 100 ama 200 badala ya kuwapotezea muda hawa vijana tena ambao wengine nauli wamekopa?
Hili swala ni nyeti sana kwa mustakabali wa Taifa, hawa watu waiichoka nchi haiwez kua salama maana ukiangalia idadi ya wanaosaka ajira na nafasi zilizopo kuna shida mahala.
Mwisho niwaombee wanaosumbuka na hizi Interview Mungu Awape Subra