Leo asubuhi nimemleta mtu hapa UDOM kuhudhuria Usaili wa kazi za Utumishi, hakika watu ni wengi. Binafsi nliyemleta ameitwa kwenye Usaili wa nafasi za National Audit, only 10 kama sio 20 nafasi lkn wameitwa watu sio chini ya 3400, yaani watu hao ndio wapatikane only 20 people. Kibaya zaidi wameitwa watu waliosoma Business Administration lkn wamefika wakaaambiwa hawana sifa.
Sasa unajiuliza kama hawakua na sifa waliwaita vipi? Hizo garama alizotumia kuja hapa Dodoma atalipwa na nani? Kuna dada kwa Mfano katokea Ifakara, anasema kaja kwa malori na kaingia Dodoma saa 8 za usiku then amekataliwa kufanya usaili eti kasoma Business Administration, kwakweli Inauma na inakera mnoo.
Kingine nnaomba kufaham ikiwa watu wa Utumishi wananufaika vip na hizi Interview maana haiingii akilini wanaohitajika kua 10 au 20 unaita watu 3600 kwenye usaili. Yaan hawana njia ya kuwachuja japo basi waitwe 100 ama 200 badala ya kuwapotezea muda hawa vijana tena ambao wengine nauli wamekopa?
Hili swala ni nyeti sana kwa mustakabali wa Taifa, hawa watu waiichoka nchi haiwez kua salama maana ukiangalia idadi ya wanaosaka ajira na nafasi zilizopo kuna shida mahala.
Mwisho niwaombee wanaosumbuka na hizi Interview Mungu Awape Subra
Tatizo la ajira limeanza siku nyingi sana, ila linazidi kuongezeka/kukua kadri muda unavyokwenda.
Ndio maana hata waheshimiwa nao "wanakijifichia" kwenye siasa kama utumishi ila wanajilipa maslahi makubwa ya mishahara na gratuity kila baada ya miaka 5.
Kama tutakumbuka kuna wakati Rais Mkapa akiwa madarakani, wakubwa wengi walitengeneza fursa za ajira BoT na watoto wao wakapata ajira kwa vyeti vya form 4 tu.
Wakati wa JK kuna scandal ya uhamiaji kuingiza watoto wao/ndugu zao kwenye ajira, yote haya yana-symbolize ajira ni issue.
Wakati wa JPM kuna wakati Hamad Masauni akiwa N/Waziri mambo ya Ndani aliwachomeka nduguze 6 kwenye mfumo wa ajira polisi, nadhani mzee akashtukia.
Wakati wa JK kuna ajira TRA vijana waliokuwa wanataka ajira walikutana national stadium.
Surprisingly bajeti ya kila mwaka ikiwamo hii ambayo imepitishwa juzi hai-address kwa kina nini kifanyike ili kuongeza wigo wa kazi Tanzania.
Nitoe mfano, kuna tozo kikodi kuchangia mfuko wa barabara (road fund), kuna tozo kuchangia REA, kuna tozo kuchangia mfuko wa maji, kuna tozo kuchangia ujenzi wa barabara zilizo chini ya LGA (TARURA).
Pengine tujiulize, what are the returns on investment kwenye mabilioni ya kujenga barabara (assuming km 1 ya lami inatumia wastani wa 1.2bn).
Mind you kwenye uwekezaji wowote uwe wa private sector, public sector au parastatal organizations hichi ndicho kinatokea
18% ya manunuzi ya bidhaa nia huduma zinaingia serikalini
30% ya corporate tax inaingia serikalini
3% ya manunuzi ya umeme zinaenda REA na EWURA
10% muajiri anatoa kwenda pension funds
Imports of goods kuna % inaingia kwenye kuboresha
the list goes on
Ukifanya simple analysis ni kama uwepo wa organized systems kama ajira unapelekea maendeleo ya watu kuwa makubwa ikiwamo kukua kwa huduma za kibiashara kama banks, insurance, legal, logistics, real estate, entertainment, marketing the list goes on
Sasa tujiulize, (sina ugomvi na Waziri wa fedha wa sasa au yule wa zamani ambae kwa sasa ni Mhe. Makamu wa Rais au yule wa enzi ya Mkapa waliotitaka tule nyasi ili ndege ya Rais inunuliwe) ila nina hoja ya kujiuliza.
Ni namna gani serikali inaweka juhudi za makusudi za sera, sheria na mikakati ambayo ina-address ku-cut down imports za basics supplies kama nguo na vitambaa, viatu, sox, chupi, sidiria, toothpick, mifagio ya ndani, mafuta ya kula, samaki, nyama (products za nyama kama sausage), maziwa, sabuni za kufulia na kuogea, mbegu za mahindi, mbegu za matunda na mbogamboga, madawa ya kilimo na mifugo, madawa ya binadamu the list goes on
Ukifuatilia hizo items utajua ni ukekaji ambao wenzetu kule nje wamefanya na wamezalisha ajira kwa vijana wao (mind you mishahara ya wafantakazi iko taxable)
Sasa kwa kujua ajira sekta rasmi ni taxable entity kwenye company operations kama VAT, taxable kwenye profit kwa 25% kama kampuni imesajiliwa Dar stock exchange na 30% kama haijasajiliwa kwenye soko la hisa; hii itupe kujua lazima kuwa na collaborations efforts ili tuzalishe ajira kwa wingi kwenye kuzalisha (basics supplies kama nguo na vitambaa, viatu, sox, chupi, sidiria, toothpick, mifagio ya ndani, mafuta ya kula, samaki, nyama (products za nyama kama sausage), maziwa, sabuni za kufulia na kuogea, mbegu za mahindi, mbegu za matunda na mbogamboga, madawa ya kilimo na mifugo, madawa ya binadamu the list goes on)
Ila kama serikali itakaa ikisubiri akina "Dangote" waje, sio kila Don atakuja. Lazima kuwatengeneza hao ma-Don.
Moja ya namna ya kuwatengeneza ni kuweka mfumo huria kwenye namna ya kupata mitaji ya uwekezaji.
Rejea mchango wa mwana JF mwenzetu japo chini akidadavua namna ya kuweka uhuria kwenye soko la mitaji kama tool ya kukuza uchumi wetu.
What will it take for Tanzania to become a successful Middle-Income Country?