Umati wa usaili UDOM: Tunahitaji mjadala wa Kitaifa kuhusu tatizo la ajira nchini

Izo conference ndio janga lingine mnawapotezea mda zaidi vijana mkisubiri posho baada ya vikao vyenu yani hii nchi watu wabinafsi sana.
Tunayajenga mkuu
Kumbuka if you fail absolutely you planned for failing
 
Tunayajenga mkuu
Kumbuka if you fail absolutely you planned for failing
Failing has never been an option to anyone, lakini system zetu zinawatu wabinafsi sana na kupotezeana mda unataka kunipanga kuhusu kujiajiri wakati unasubiri posho ata sijui nitakulaje huo mchana ni kitu gani kitazungumzwa kisichowezwa kufika kwa njia ya maandishi!? Gaddamit!
 
Sasa mtu umeitwa kwenye udail wew unajijua hal ngunu hata naul hauna wala pesa yakwenda kujitunza uko ukiwa unasubir hauna, alafu unaenda kufanya nn? Sometime elimu nayo inahitajika ktk kufikil kwenye mambo madg kama hayo, unajua kabs nafas n chache, alaf wanaohitaji n wengi, wew kujituliza home waona nini?? unakuta nafasi imetangazwa wanahoitajika ni kama hao 20, walioenda kugombania nafas ndy kama hao zaid ya 300.

Hapo kuna ambao wana connection, kuna ambao watatoa rushwa, kuna ambao wana vijidawa vyakishirikina , na kuna wew hapo ambaye hauna chochote chakukusaidia, then unataka utoboe kwenye nafas?? hiyo kitu haipo asee tukazane kulima na kudunduliza vijikaz huku huku mitaan kulko kupoteza muda na naul ambapo ungeitumia iyo pesa ya naul kununua maji na sigara kuuza stend, ungefaidika na vimia3 hivi, wasomi ni mzgo, kuna shauri nging sana niliwai toa ktk mitandao ya kijamii,.kama serkali.itafanyia ,kazi basi tatizo la ajira litakwisha kabisa
 
Website ya Ajira ni tatizo sana kwenye suala la kuajiri watu.

Kama taarifa inasema mtu awe amesomea Bachelor of Account wewe ukiwa na B.com yako au B.A yako hawakuchukui hats kama kwenye bachelor yako ulistick na Account.
Hyo website ina shida mfano wa course unakuta ni social science zina relate Bado wanakatilia watu naona hawajitambui aisee. Mfano computer science, IT software engineering naona zina relate ila mtu akifanya application Ina mugomea
 
Wajaribu kuwashirikisha na taasisi zinazohitaji hao wafanyakazi wanaotaka kuajiriwa, hivyo kuongeza hivyo vigezo ili visaidie kupunguza idadi ya interviewees.

Mfano mimi nimewahi kushiriki katika kuhoji waajiriwa watarajiwa wa taasisi niliyokuwa nafanyia kazi. Mchujo wa kwanza ulishirikisha vilevile maafisa wataalamu kutoka taasisi ili kuhakikisha kwamba walioteuliwa kwa mahojiano wanafaa kwenye zile post. Kwenye kila post moja walikuwepo wahojiwa sita baada ya mchujo na kwa asilimia kubwa walikuwa hawatafautiani sana kwa majibu.
 
Naombea siku moja vijana walipuke, ili wagawa keki ya taifa wapate akili.
 
Na hiyo inakwenda kwa hata baadhi ya taasisi za kimataifa, huwa tayari wanae mtu wao nyinyi munaitwa kukamilisha mchakato tu.
 
Hafu hzo oral kwanini zisiwe zinafanyika online via zoom au micro softteams kuliko kusumbua watu na kuepusha gharama maana dunia ya Sasa ni digital zaidi
 
Mtu wa BA kuitwa kwenye Auditing ni kichekesho, arudi tu tuuze mitumba hapa Kimara mwisho.
 
Nakwambia hii kutokana na experience.
Well, inategemea shirika na shirika.
Ila mimi nimefanya interviews nyingi sana mashirika ya aina hiyo na mimi pia experience yangu ni kwamba ni merit-based kiukweli. Na sasa hivi mimi kwenyewe nashiriki kwenye interview panels, kwa kweli hakuna vimemo mwendo ni merit based, na ikigundulika tu kuwa mchakato ulikua na shida sehemu, mchakato inaanzishwa upya (nimeshuhudia hii ikifanyika mara mbili baada ya kuonekana kulikua na irregularities).
 
Tatizo la ajira limeanza siku nyingi sana, ila linazidi kuongezeka/kukua kadri muda unavyokwenda.
Ndio maana hata waheshimiwa nao "wanakijifichia" kwenye siasa kama utumishi ila wanajilipa maslahi makubwa ya mishahara na gratuity kila baada ya miaka 5.
Kama tutakumbuka kuna wakati Rais Mkapa akiwa madarakani, wakubwa wengi walitengeneza fursa za ajira BoT na watoto wao wakapata ajira kwa vyeti vya form 4 tu.
Wakati wa JK kuna scandal ya uhamiaji kuingiza watoto wao/ndugu zao kwenye ajira, yote haya yana-symbolize ajira ni issue.
Wakati wa JPM kuna wakati Hamad Masauni akiwa N/Waziri mambo ya Ndani aliwachomeka nduguze 6 kwenye mfumo wa ajira polisi, nadhani mzee akashtukia.
Wakati wa JK kuna ajira TRA vijana waliokuwa wanataka ajira walikutana national stadium.

Surprisingly bajeti ya kila mwaka ikiwamo hii ambayo imepitishwa juzi hai-address kwa kina nini kifanyike ili kuongeza wigo wa kazi Tanzania.

Nitoe mfano, kuna tozo kikodi kuchangia mfuko wa barabara (road fund), kuna tozo kuchangia REA, kuna tozo kuchangia mfuko wa maji, kuna tozo kuchangia ujenzi wa barabara zilizo chini ya LGA (TARURA).
Pengine tujiulize, what are the returns on investment kwenye mabilioni ya kujenga barabara (assuming km 1 ya lami inatumia wastani wa 1.2bn).
Mind you kwenye uwekezaji wowote uwe wa private sector, public sector au parastatal organizations hichi ndicho kinatokea
18% ya manunuzi ya bidhaa nia huduma zinaingia serikalini
30% ya corporate tax inaingia serikalini
3% ya manunuzi ya umeme zinaenda REA na EWURA
10% muajiri anatoa kwenda pension funds
Imports of goods kuna % inaingia kwenye kuboresha
the list goes on
Ukifanya simple analysis ni kama uwepo wa organized systems kama ajira unapelekea maendeleo ya watu kuwa makubwa ikiwamo kukua kwa huduma za kibiashara kama banks, insurance, legal, logistics, real estate, entertainment, marketing the list goes on

Sasa tujiulize, (sina ugomvi na Waziri wa fedha wa sasa au yule wa zamani ambae kwa sasa ni Mhe. Makamu wa Rais au yule wa enzi ya Mkapa waliotitaka tule nyasi ili ndege ya Rais inunuliwe) ila nina hoja ya kujiuliza.

Ni namna gani serikali inaweka juhudi za makusudi za sera, sheria na mikakati ambayo ina-address ku-cut down imports za basics supplies kama nguo na vitambaa, viatu, sox, chupi, sidiria, toothpick, mifagio ya ndani, mafuta ya kula, samaki, nyama (products za nyama kama sausage), maziwa, sabuni za kufulia na kuogea, mbegu za mahindi, mbegu za matunda na mbogamboga, madawa ya kilimo na mifugo, madawa ya binadamu the list goes on
Ukifuatilia hizo items utajua ni ukekaji ambao wenzetu kule nje wamefanya na wamezalisha ajira kwa vijana wao (mind you mishahara ya wafantakazi iko taxable)
Sasa kwa kujua ajira sekta rasmi ni taxable entity kwenye company operations kama VAT, taxable kwenye profit kwa 25% kama kampuni imesajiliwa Dar stock exchange na 30% kama haijasajiliwa kwenye soko la hisa; hii itupe kujua lazima kuwa na collaborations efforts ili tuzalishe ajira kwa wingi kwenye kuzalisha (basics supplies kama nguo na vitambaa, viatu, sox, chupi, sidiria, toothpick, mifagio ya ndani, mafuta ya kula, samaki, nyama (products za nyama kama sausage), maziwa, sabuni za kufulia na kuogea, mbegu za mahindi, mbegu za matunda na mbogamboga, madawa ya kilimo na mifugo, madawa ya binadamu the list goes on)

Ila kama serikali itakaa ikisubiri akina "Dangote" waje, sio kila Don atakuja. Lazima kuwatengeneza hao ma-Don.

Moja ya namna ya kuwatengeneza ni kuweka mfumo huria kwenye namna ya kupata mitaji ya uwekezaji.

Rejea mchango wa mwana JF mwenzetu japo chini akidadavua namna ya kuweka uhuria kwenye soko la mitaji kama tool ya kukuza uchumi wetu.

What will it take for Tanzania to become a successful Middle-Income Country?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…