Umati wa usaili UDOM: Tunahitaji mjadala wa Kitaifa kuhusu tatizo la ajira nchini

Ndugu zangu nalisema hili kwa uchungu sana.

Kama huna Godfather kwenye hizo Taasisi za Serikali, wewe kupata kazi ni kizungumkuti. Watu wanahonga mpaka milioni 5 ili apate kazi Tanesco au TRA au TAWA na anapata, hizo kitu mnaita Usaili kwa kiasi kikubwa ni kuwaridhisha tu wananzengo ili msipige sana kelele. Kuna nafasi ziliwahi kutangazwa na Mamlaka ya Anga walikuwa wanataka watu, kabla hata usaili kufanyika tayari kuna watu wakawa wameshazikava zile nafasi na kazi wameanza.

Kuna kitu nilikuwa nakiona binafsi, mama angeamua sasa tuanze kupunguza idadi ya milima tuliyonayo, vijana tupewe nyenzo na Serikali kwa kukopeshwa, nchi yetu ijengwe kwa barabara za kokoto na Mawe na sio lami tena. Tuanzie Morogoro na Dodoma, tukeleze hiyo milima mpaka ipatikane kokoto na mchanga wa kokoto ndio utumike, eneo litakalopatikana tuanze kulima, mitaji tutakuwa tumeshaipata.

Pia, Mama aruhusu kilimo cha bangi. Amin nakwambia, uvutaji wa bangi mitaani utapungua kwa kasi ya ajabu mno maana kila atafocus kwenye kuiivisha ili apige mpunga wa maana.
 
Hata Mimi ndo ninavojua hivo na labda incase ka wanataka kumchukua internal candidate wao aliyejitolea.
 
Of course siyo mashirika yote, lakini angalia yale ya kimataifa ambayo jamaa zetu Watz wametamalaki katika baadhi ya idara au vitengo (sitaki kutaja majina). Na sizungumzii ambao hawana qualifications kabisa, hapana.
 
Hili tatizo acha liwe kubwa kwakuwa tunachagua wasio na mission wala vision kutuongoza
 
Hizo interview nyingi ni geresha tu, uhalisia ni kwamba hizo nafasi zilizotangazwa zote zina watu wake tayari.
 
Tupo hapa ukumbi wa Jakaya Kikwete Conference Centre

Tunajadili mabadiliko ya mtaala unaoweza kuandaa wahitimu kujiajili, kuajiliwa katika kukuza uchumi wa kati

Karibu tujadili

Let's be A Job creator rather than being the Job seeker
Acheni kuumiza vichwa,hata ulaya vijana wanatafuta ajira,uzuri ni kwamba serikali za nchi zao,zilijenga viwanda vya kutosha kwahiyo Swala la kuajiliwa sio tatizo.
Sasa hapa unasomesha wahandisi 4000,wakati nchi haina hata uwezo wa kuajili wahandisi 200!
Twendeni tukafuge,tuendeshe boda boda,tufungue saluni za kike,vibanda vya chipsi.
 
Website ya Ajira ni tatizo sana kwenye suala la kuajiri watu.

Kama taarifa inasema mtu awe amesomea Bachelor of Account wewe ukiwa na B.com yako au B.A yako hawakuchukui hats kama kwenye bachelor yako ulistick na Account.
Mkuu sidhani kama upo sahihi,mimi nimesomea BBA kwenye mwelekeo wa uhasibu tena chuo cha private,sijawahi kuomba nafasi ya kada yenye sifa nilizosomea wakaniacha,mara zote nimeitwa, juzi nimeomba za TRA,tax management officer,najua lazima kwenye usaili nitaitwa.

Cha umuhimu uweke taarifa zako za kielimu vizuri tu utaitwa hadi zingine utakuwa unachagua kwenda kwenye usaili au kutokwenda.
 
Tupo hapa ukumbi wa Jakaya Kikwete Conference Centre

Tunajadili mabadiliko ya mtaala unaoweza kuandaa wahitimu kujiajili, kuajiliwa katika kukuza uchumi wa kati

Karibu tujadili

Let's be A Job creator rather than being the Job seeker
But you are employed too...
 
Ninachosema ni kutokana na experience ya watu waliokataliwa kwa sababu hiyo, uzuri ni kwamba ajira portal kama umeomba kazi wanatoa mrejesho kama hawakuchukui kwa ajiri ya interview.
Ntamuomba mmoja ya watu waliokataliwa kwenye kazi hizi za National Audit anitumie screenshot ya walichojibu watu wa ajira portal uamini.
 
Tupo hapa ukumbi wa Jakaya Kikwete Conference Centre

Tunajadili mabadiliko ya mtaala unaoweza kuandaa wahitimu kujiajili, kuajiliwa katika kukuza uchumi wa kati

Karibu tujadili

Let's be A Job creator rather than being the Job seeker
Ndio maana mmeona mjikusanye hapo kupata per diem zenu! ndio mme-create job hapo.
 
Kuna kipindi walikuwa wanasisitiza sana waombaji waupdate details za accounta zao kutokana na maboresho waliyoyafanya,inawezekana ni kipindi hicho
 
Wanaepuka lawama, mfano SUA ,juzi kuna jamaa wa Kilombero walikuwa wanataka kupata vijana wa Field Kwa njia ya interwiew,sasa kuna wanafunzi waliomba nafasi hiyo hawakuitwa hata kwenye interwiew, unajua lawama zake??. Vijana wale walilaumu Sana kuwa Kwanini hawajawaita?, kwamba si wangewaita tu wakashindwe wenyewe?. Umeona eenhh?, Kwa hiyo walichokifanya utumishi ni sahihi kabisa.
 
Kuna kipindi walikuwa wanasisitiza sana waombaji waupdate details za accounta zao kutokana na maboresho waliyoyafanya,inawezekana ni kipindi hicho
Mimi naongelea sasa hv kwa mtu aliye update tayari taarifa zake na ameapply kazi hizi za juzi tu
 
Wanatafuta siku za usaili ziwe ndefu na nyingi ili wapongezane kwa posho kubwa kubwa...
 
Mpe pole Sana mkeo kwa kukutana na swali la khs mambo ya GDP kwny mtihani wa Auditing.

Ndio Tz ya Viwanda hio.
 
ni wakati wakuanza kutumia teknolojia kuinterview watu baada ya kuwaita maelfu ya watu kama tuko zama za ujima.....hivi hao utumishi hawajui kama kuna zoom na tools nyinginezo kama skype nk...
 
Wakiandaa vigezo vizuri wakati wa shortlisting, hawana haja ya kuita watu wote wale. Sometimes ukijaa hofu ya kuwa challenged unaweza fanya mambo yasiyo na maana
 
ni wakati wakuanza kutumia teknolojia kuinterview watu baada ya kuwaita maelfu ya watu kama tuko zama za ujima.....hivi hao utumishi hawajui kama kuna zoom na tools nyinginezo kama skype nk...
tanzania ina mambo mengi sn kila mtu analake wakisema watumie technologies kuna watu watalalamika hawana vifaa vyakufanya hvy wengine wengine location na networks problem kuna watu wanasoma chuo hadi wanamaliza computer hawajue kutumia
kipindi cha corona watu wameambiwa wajaribu kufundisha kwa technology imeshindikan kila mtu anasema lake

mm naona ni muda wakubadilika tufanye reform kweny mifumo yetu tuendane na technology bila kusubir kwan itasaidia sn itafanya watu wajifunze matumizi kwakua itakua muhimu na sio option tena
tusave cost na time kwa jobseekers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…