Uchaguzi 2020 Umefaidika nini na CCM -Jipime tokea 2015 tu hata leo uipe tena kura yako

Uchaguzi 2020 Umefaidika nini na CCM -Jipime tokea 2015 tu hata leo uipe tena kura yako

Ndugu yangu wa karibu amestaafu ni mwaka wa tatu huu anasubiri mafao. Hata nauli ya kurudi kwao hajapewa. Nyumba anayoishi ni ya kupanga inabidi mke wake apike mama ntilie ili waweze kuishi. Bado wanadaiwa 20,000 kitambulisho cha mjasiliamali.
Mzembe huyo, mtu Hadi unastaafu hukuweza kuwaza utaishije baada ya kustaafu? Hicho kutambulisho si angekata kabla ya kustaafu? Acheni kutetea wazembe.
 
Mzembe huyo, mtu Hadi unastaafu hukuweza kuwaza utaishije baada ya kustaafu? Hicho kutambulisho si angekata kabla ya kustaafu? Acheni kutetea wazembe.
Wewe unesha kata hicho kitambulisho,kwa maandalizi ya kustaafu ?
 
Marehemu bibi yangu mpaka anafariki alijua Nyerere ni cheo cha kuongoza nchi. Alikua anafukuza “Nyerere wa sasa ni nani”?
Mna matatizo kwenu, ulishindwa Nini kumwelewesha kwamba Nyerere ni mtu siyo cheo? Nyumba nzima hamna aliyekuwa na akili za kumwelewesha Bibi yenu Hadi anafariki?
 
Jiulize mwanachi wa Arusha,Mbeya,Kawe,Iringa mjini,Mbeya mjini wamefaidika nini kuwa na wabunge wa Chadema??
Mengi,hata kuweza kuwakumbusha mnapokosea ni mafanikio makubwa Sana
 
Sijafaidika chochote maana hata kwenye biashara wateja wanakimbià napo TRA wanasumbua. Aaaaagh
 
Muulize na jirani yako ni kitu gani binafsi kimembadilikia katika maisha yake tokea aichague CCM 2015 hadi leo,kiasi ya kwamba anafuraha ya kuipa tena CCM kura yakemfaida gani ya kujivunia yeye kama yeye mpiga kura wa kawaida tu,kama hakuna mabadiliko tokea 2015 hadi leo kwanini asiipeleke kura yake kwa Tundu lissu na kutoa kipimo cha miaka mitano ijayo ?

Maana kuichagua CCM miaka nenda miaka rudi upo palepale inamaana hako kachama hakana faida na wewe ni kujisumbua tu wanafaidika wenye viti na meza wewe mlala hoi huna unalolipata zaidi ya kunyanyaswa na makodi yasio na kichwa wala miguu,ni wakati sasa wakuachana na tabia ya kuipa kura ccm wakati hakuna wala hupati faida.
Mishahara haipandi,vyeo kwa wakubwa tu walewale wanahamishwa huku wakipelekwa huku,wewe usioonekana na chama hiki achana nacho.
Mimi nimemuuliza mwanachadema mmoja akanijibu hivi
 
Wengi wanaitetea ccm bila sababu yoyote ya nsingi yaani wanasumbuliwa na umbumbu.

Ni wale wanadhani Tanzania ni ccm bila ccm na Tanzania haipo

Wasikilize viongozi wako

 
Jiulize mwanachi wa Arusha,Mbeya,Kawe,Iringa mjini,Mbeya mjini wamefaidika nini kuwa na wabunge wa Chadema??
Zaidi ya matusi, kugomea bunge,kutukana Serikali na watendaji wake hakuna. Chama cha Mbowe kina nini cha kuwapa watanzania?. Faru John?.
 
Wanachama wa CHADEMA, wanafaidika nini na hiyo saccos wakati michango na ruzuku anakula mwenyekiti pekee na hakuna wa kuhoji. Mkiitwa manyumbu ni sahihi kabisa, mtakamuliwa mpaka akili zirudi mahali pake.
 
Tundu Lissu hana sifa za kuongoza Tanzania
hawa wagagagigikoko tunaowapa kura zetu tokea mfumo wa vyama vingi, CCM hawajatubadilisha tuko palepale tunasota na maisha ya kuokota maembe na kutia viraka,hawana faida ,na ukiangalia sana CCM wanawazidishia umasikini wanannchi,kwa maana toka uanze kuipa kura CCM badala ya kusonga mbele unajikuta unaludi nyuma.

Sasa iliwezeka kuona CCM wanasifa za kuwapa kura matokeo yake upo palepale,utaniambiaje kuwa CCM wana sifa za kuendelea kupewa tena kura usilete makelele ya kujenga dalaja na ndege hizo wanapanda waliozinunua ndio wanaomiliki magari na hela za kupandia ndege.

Maisha yangu kijijini na mitaani ni yaleyale tokea haka kachama ka CCM nikipe kura ,mwaka huu kwa kuwa CCM hawakunibadilisha wamenizidishia umasikini bora nipeleke kura kwa Chadema niwaone nayo miaka mitano yao kama watavurunda kuliko CCM bado vipo vyama vingine,ila CCM mimi nisie na kiti wala meza kura yangu naipeleka kwengine na sio kubahatisha ni haki yangu na nahitaji wapigiwa kura na vyama vyao waiheshimu kura yangu.
CCM ni walewale hawana jipya na wamefeli kuinua hali yangu mimi Mtanzania mpiga kura wa kawaida ,nafaidika nini niwape kura yangu..
 
Wamefaidika na nidhamu kwa watumishi kwa hiyo wako nayo nyumbani saizi wanalia ugali
 
Wanachama wa Chadema, wanafaidika nini na hiyo saccos wakati michango na ruzuku anakula mwenyekiti pekee na hakuna wa kuhoji. Mkiitwa manyumbu ni sahihi kabisa, mtakamuliwa mpata akili zirudi mahali pake.
Sizungumzii habari ya Chadema nipo na maisha ya mwananchi wa kawaida sana,amefaidika nini,amebadilika nini zaidi ya kupigika na hali ya maisha ,hakuna faida aliyoipata katika utawala wa CCM,anayohaki ya kutafuta sehemu nyingine ni uhuru wake lakini sio kulazimishana,mara hii akichagua chama kingine nini kosa lake,hatumii daraja wala si mpanda ndege hayo hayamuhusu wakati kula yake ni ya shida ,hajafaidika na chochote na utawala wa ccm.

Harafu unamwambia chagua CCM unawazimu.
 
Nami najiuliza ni kitu gani nitafaidika nacho nikimpa kura Lissu, kwa maana hiyo, CHADEMA, ambacho nimekikosa katika miaka 5? Je, kuna ushahidi gani kuwa nitakipata hicho nisichokijua?

Mimi ni:
√ mjasirimali mdogo nilikuwa nakimbizana na mgambo sasa hivi nafanya biashara pasipo bughuza;
√ mzazi wa kipato cha chini kabisa sikuweza kuwasomesha watoto wangu sasa wako shule;
√ mkulima nilikosa soko kwa sababu ya ubovu wa barabara lakini sasa wachuuzi wengi hufika kununua mazao yangu;
√ mwanakijiji nilikuwa napata shida ya maji safi na salama, sasa tumechimbiwa kisima maji si shida tena;
√ fundi kuchomelea kijijini sikuwa natumia ufundi wangu kwa kukosa umeme, sasa nimeanza kazi hiyo inanipatia kipato cha kukimu maisha yangu na familia;
√ mwanafunzi wa chuo niliyekuwa nacheleweshewa mkopo wa masomo sasa naupata kwa wakati;
√ mfanyakazi mwajiriwa nimepunguziwa kodi hivyo kipato halisi kimeongezeka;
√ mkazi wa Arusha sikuwa na matumaini usafiri wa reli ungerudishwa sasa nasafiri na kusafirisha mizigo yangu kwa nauli ndogo ninayoweza kumudu, fedha inayobaki naifanyia shughuli zangu nyingine za maendeleo;
√ na kadhalika.
 
Ivi ni kweli CCM inaweza kutuletea maendeleo yani kuwa na pesa mfukoni na maisha kuenda?? Kazi ya serikali nikutujengea miundo mbinu ili sisi raia tuweze kufanya kazi katika mazingira mazuri... Na kutengeneza fursa kwa vijana tuweze kujiajiri au Kuajiriwa!!

Vijana tuache uvivu wakati wewe unasema CCM haijakuletea maendeleo kuna mwenzio anajenga nyumba ya pili sasa ndani ya iyo miaka mitano ya JPM!!! tukiwa na mipango mizuri ya maisha tutasonga ila ukweli ni kwamba vijana sisi wa sasa niwa vivu haikuwai kutokea!!!

Ivi ni kweli mnaamini Lissu akiwa Rais maisha yatakuwa bora? Tujikite kwenye kutafuta pesa wakuu ila ukweli me kila nikijiwazia kuhusu lisu au chadema bado hawawezi kutawala Tanzania.... Waendelee kuwa wabunge ili watawala wasijisahau ila sio kiti cha uraisi
 
Binafsi afya yangu imeimarika SANA, nakunywa Mirinda nyeusi kama kiburudisho, zile swagga light my weekend sinaga, na chakula changu nabadili mboga za majani, nguna mchicha, dona kabichi, ubwabwa chainizi, mchemsho wa tembele n.k

#Ubwabwa_kuku
#Twende_na_Rungwe

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hiki chama cha kijani kibichi CCM yaani wameishadanganya watu mpaka wameishiwa hoja kabisa , serikali ya viwanda hewa , ahadi hewa , kazi wanayoiweza Ni utekaji ,uuaji ,na upotezaji watu .
 
Back
Top Bottom