Umefika wakati wa Simba kutafuta Msemaji mwingine

Mshangai

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2008
Posts
468
Reaction score
1,086
Nadhani kwa Manara kuwa msemaji wa klabu kama Simba wakati umemtupa mkono asukuriwe kwa aliyofanya na sasa apewe jukumu hilo mtu atakaye kwenda kisasa.

Uswahili swahili wa Kariakoo level hiyo imeshapitwa na sasa tuwe kama klabu zingine kubwa barani Afrika. Kama Haji Manara kafikia level ya kina Steve Nyerere kuzungumzia followers wa Instagram na Facebook kama kipimo cha maendeleo, basi kuna kasoro kubwa sana.

Manara bado ana mentality ya kuwa Simba kuifunga Yanga ndio mafanikio ya klabu yetu, hata kama itafungwa matano matano huko nje ni sawa tu.


Msemaji wa Simba SC, Haji Manara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshangai,
Hahahaha umeongea la maana ingawa utapingwa na wengi. Mimi siyo Simba ila kwa klabu kuwa na msemaji Kama yule wa mipasho no fedheha kwa klabu...yeye Kila muda ni mipasho tu kwa Yanga utafikiri klabu hizi ni za taarabu...upo wakati Yanga nayo wakati wa manji ilikuwa na msemaji wa Aina hiyo, dah..Simba itabidi wakae chini na kuchukua hatua..ingekuwa ni nchi nyingine huyo manara angekuwa ameshafungiwa kitambo.
 
Hivi taarabu na ngonjera za yule jamaa aliyezoea kuzunguka mapori hajazisikia je? Au Nyani haoni kundule....!
 
Manara yuko kwa maslahi yake binafsi, na anajua bila kuizungumzia yanga hawezi kuwa maarufu, yanga ndio inayompa pesa za matangazo, simba sijui kwa nini hawalitambui hilo, hana habari na simba yeye kila siku yanga tu, tatizo simba mbumbumbu wengi hawajui manara anajijenga yeye binafsi hajengi timu
 
Kwani msemaji wa ccm anazungumzia chama gani!
Yule wa Arusha sasa iv atagombea ubunge, kwa kujijenga kupitia kuizungumzia chadema.
Ni kawaida na ni formula ya maisha.
 
Ukweli ni kwamba Manara ni miongoni mwa watu wanaochangia kuijenga simba mitandaoni na kuiharibu uwanjani.....amekua muongo muongo kuipa sifa timu isizokua nazo na kuonekana bonge la timu mitandaoni ila uanjani sifuri....Simba wapitakiwa kuanza na huyu kabla ya Uchebe waliomtoa kwa dhulma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Manara anafanya kazi yake vizuri tu nadhani ana-play part yake vizuri sana kama msemaji na shabiki. Kama ni taarifa huwa anatoa na huwa tunaziona zikiwasilishwa rasmi kutumia akaunti za Simba SC au kupitia vyombo vya habari.

Manara ni shabiki wa Simba SC damu-damu kama ambavyo hujieleza, hivyo tambo zake na maneno ya kejeli kwenye kurasa zake binafsi ni kama tu ambavyo mashabiki wengi hufanya kwenye maisha ya kishabiki. Vitu anavyo-post Manara kwenye page yake Personal ni haki yake kama shabiki ikiwa tu havunji sheria za mitandao na nchi. Simba SC wana mtu sahihi kabisa.

Sishabikii Simba SC wala timu yoyote inayoshiriki ligi za Tanzania. Nimetoa maoni kama shabiki tu wa mpira wa miguu.
 

Well said wengi wanaomping hapa sio simb ni yanga hawa wanakereka na maneno yake kama mambo kasema kwenye page yake binfas ni mawazo yake binfs so sijui kinachowauma ni nn, mwachen afanye kaz yake.

Manara ni msemaj anayesababisha mashibik wengi wa simba wanajaaa uwanjan hakik ni muhamishaji namba moja Tanzania. Pili, ndugu zetu nao wamekuwa wanyonge sana kipind cha nyuma wakiwa na ten wakaona wamtafute msemaj mwenye maneno kama Manara, which they have failed sasa wanaona watumie njia ya kumuondoa kabisa.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…