Umefika wakati wa Simba kutafuta Msemaji mwingine

Simba ndio mabingwa wa ligi yako mara mbili mfulululizo, Simba ndio timu pekee iliyofika robo fainali ya Champions League Msimu uliopita, na ikasababisha Tanzania kuongeza timu kutoka mbili mpaka nne.

Simba ndio inayoongoza ligi yako mpaka na ndio timu yenye takwimu bora kuliko timu zote,hebu niambie nikitu gani kilichokuongoza wewe hadi kufikia kuiita Simba ni sifuri. Ondoa mihemko nipe takwimu.

Binafsi kuna mambo anayafanya manara mimi sipendezwi nayo pia nafikiri anamihemko iliyopitiliza, lakini vilevile Kuna Maisha baada ya Simba ndiyo anayojaribu kuyatengeneza akiamini kua vyeo nivyakuja na kuondoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utakuwa unachanganya kati ya Msemaji na Mhamasishaji. Tuliisema sana Yanga ilipokuwa na "msemaji" ambaye kwa sasa ni DC Arumeru, nayo ulikuwa hivi hivi kama Dar Modern Taarabu. Hatuwezi kuwa na watu kwenye nafasi zisizowatosha, Manara ni mzuri na muhimu kwa Simba lakini si katika nafasi ya Msemaji wa timu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa wanaompinga ni timu pinzani maana anawakera sana kwa maneno, yani Manara ni moja ya wasemaji ambao timu yako ikicheza na Simba SC lazima ujiande kukerwa 😂 na hii ndio maana halisi ya shabiki. Na mashabiki huwa tukikosa kitu kama kombe ambalo ni la karibuni basi tunatafuta tulipowazidi wenzetu ili mradi tuwe tu juu na ndio Manara anachofanya anawaringishia wapinzani vitu kama followers ambayo siyo kitu kikubwa sana ila lengo ni kuwakera tu wapinzani. Kiukweli huwa na-enjoy tambo zake pale Instagram japokuwa sishabikii Simba SC. Huyu na Masau Bwire ni moja ya wasemaji wenye maneno ya kukera sana, nikisikiaga ni Simba SC na Ruvu Shooting lazima nitafute interview zao niwasikie wanasema nini. Mzee wa mpapaso huwa anabisha hadi ukweli na ndio maana halisi ya ushabiki. 😂
 
Labda sijui mengi kuhusu hayo ila wenye timu wakiona hafai watamtoa maana wao ndo wanaona umuhimu wake.
 
Ungewauliza wanaodhani kwamba usemaji wa uropokaji kama wa Manara, Kifaru, Nugas, Bwire, n.k.: Wanawajua wasemaji wa TP Mazembe na El Ahly? Au wa Real Madrid, Man U, Bayern Munich? Washabiki wa timu hizo wanawajua wasemaji wao? Hawapati habari muhimu kwa wakati mwafaka? Kuna yeyote anaweza kutupa nukuu moja ya mipasho baina ya msemaji wa Real Madrid na wa Barcelona? Au wa Man U na Man City?
 
Hili swali nisha wahi uliza kwenye kilinge nikakosa jibu, tuna haribu mpira wetu kwa mambo ya kijinga kijinga tu tumejaza waropokaji ambao hawana maana.. kwa wenzetu walio tuzidi kila kitu hawana haya mambo sisi tunayatoa wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, usemaji huo wa kukera kama unavyouita una msaada kwa timu inaposhiriki michezo ya kimataifa?

Au ndio hayo tunaishia kulambishwa tano tano na wanachama kuumia? Nadhani mleta mada hakusema Manara hafai, bali katika usemaji wa timu sio level yake yeye anafaa katika uhamasishaji huko ambako maneno ya taarabu, nyodo hata matusi ni ruksa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa kabisa. Mpira sasa hivi ni ajira kubwa sana na biashara nono ndio maana watu wanawekeza mabilioni ya fedha zao. Makampuni makubwa yanajihusisha na mipira. Hivyo ni serious business ambayo kama kuna ujinga ujinga acha uwe katika level ya ushabiki sio cheo chochote official cha Club.

Lazima tutoke huko na kuingia level nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyura bhana! Nugaazz kawaangusha kashindwa kumfunika Manara.
 
Uswahili swahili wa Haji ni kielelezo cha Mikia SC ni ya aina gani.
Angalia issue ya Uchebe. Mwishowe haijulikani wanataka kitu gani.
 
Wape salaam, mafumbo ya akina Hadija Kopa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha ajabu watu wanaotaka manara aondelewe ni yanga utajua ni jins ghan huyu bwana ni mwiba kwao mbona sijawah sikia simba wakisema tena atolewe[emoji28] yanga achen kuingilia mfumo wa simba tuachieni simba yetu mwachen Manara wetu na hakuna point unaweza fananisha timu zetu na ulaya hii ni league tofauti aina ya ushabikiaj wa mpira ni tofaut na utamaduni tofauti.

Hizo team ambazo hazina wasemaje kama manara kimataifa zimefika wapi. Manara katujazia uwanja apa tumecheza kwa moral sana Wacongo na Wazambia hawakuamini tumefika robo fainali.

Vyura wameona wivu sana na wanatambua nguvu ya manara wanaona njia pekee ni kumuombea aondoke.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Uneducated liar. Ndiyo sifa kuu za Haji.
Mashabiki wake wako level moja na yeye. Ni wengi kama nzige. Wasipuuzwe kirahisi.
 
Hoja zako hazina mashiko kabisa hivyo Manara ataendelea kuwa msemaji wa Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…