Umejiandaa vipi na maisha ya uzeeni (Retirement)?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Wana jamvi uzima na afya uwe kwenu nyote.

Hapa siongei na wavulana na vijana wa hovyo. Bali naongea na vijana na watu wazima wenye kujitambua haswa.

Ni ukweli pasina shaka kuwa maisha ya ujana yanapita upesi sana. Kama usipojiwekea malengo ya huko mbeleni utaishi maisha ya tabu sana.

Wala sio Siri wengi wa wazee tunao waona leo hii wanaishi maisha Duni, taabu na mateso walipitia nyakati kama zetu za utoto,ujana na utu uzima Hadi uzee.

Wengi wao wanaishi Kwa sonona na stress ya Hali juu mno ni vigumu kuwatofautisha na chizi.

Hivyo ukiona vile ni Vyema na haki nawewe ukajipanga Kwa ajiri ya kesho Yako.

Ningependa katika Uzi huu tupeane mbinu za kuwekeza Ili badae tuje tuishi maisha mazuri tukicheza na kuimbia wajukuu zetu kama baadhi ya wazee wanavyoishi Leo hii.

Ni furaha iliyo je uzeeke ukiwa na uhakika wa maisha mazuri na afya njema kabisa.
FB_IMG_1646668789770.jpg
 
Maisha haya tuishi tu mkuu, kujiandaa hakuishi, nilipokuwa nasoma,unauliziwa swali umejiandaa je na maisha baada ya kusoma? umejiandaaje na maisha ya ndoa? umejiandaaje na malezi ya watoto? Uko kazini umejiandaaje na maisha kazi ikiisha? ukienda kanisani, Yesu akija leo umejiandaa je, au kama sio Yesu, Ukiwa msibani utasikia mwenzetu ametangulia sisi tuliobaki tumejiandaa?.

MKuu tuendelee tu kuishi, utakapokutiwa ndo hapo hapo
 
Ni hakika mkuu usemavyo. Binafisi kilicho nisukuma kuleta Uzi huu Kuna baadhi ya wazee enzi zao walikuwa na maisha mazuri hasa!

Mimi Kuna baba yangu mkubwa Sasahivi anauza ugoro na tumbaku miaka ya 90+ alikuwa na fuso 3 maduka na alikuwa mtu maarufu sana. Bahati mbaya hakubahatika hata kusomesha mtoto mmoja.

Maisha anayoishi Kwa Sasa unamuonea huruma.Naimani anajutia sana lakini ndo hivyo Hana namna tena
 
Binafsi napenda kuishi sasa , kila ukiwaza kesho utajikuta kesho unawaza kesho kutwa na kuendelea na kushindwa kuishi sasa na maisha yako yote ukajikuta umeishi ukiwaza siku inayofuata bila kuishi siku uliyopo.
 
Alipopata pesa hakuongeza mke?
 
Maisha haya tuishi tu mkuu, kujiandaa hakuishi, nilipokuwa nasoma,unauliziwa swali umejiandaa je na maisha baada ya kusoma? umejiandaaje na maisha ya ndoa? umejiandaaje na malezi ya watoto? Uko kazini umejiandaaje na maisha kazi ikiisha? ukienda kanisani, Yesu akija leo umejiandaa je, au kama sio Yesu, Ukiwa msibani utasikia mwenzetu ametangulia sisi tuliobaki tumejiandaa?.

MKuu tuendelee tu kuishi, utakapokutiwa ndo hapo hapo
ila kujiandaa uzeeni ni muhimu hii itawapa afadhari watoto wako na watu wengine wa karibu,kuwa mzee haina maana uje uwe tegemezi kwenye kila kitu watoto wako watakuwa na majukumu yao kulea familia zao,nakuwafanya watoto wao wafikie ndoto zao.

si utamaduni sana kwa familia zetu zakiafrika kusingatia hichi kitu ila ni wajibu wa mzazi kuhakikisha mtoto anakuwa salama toka siku umemzaa mpk siku unaaga dunia mtoto wako anatakiwa awe proud kuwa alikuwa na mzazi ambae hakuwa tu na fikra za kufikiri kila mtoto ni wajibu kumsaidia mzazi!,na kama wazee walikuwa masikini hivyo ni jukumu la watoto kuja kukutoa kwenye hilo dimbwi..
inatakiwa tupambane watoto waje wale raha,wakue vyema,waone maisha ktk namna tofauti nao wakawajibike kwa watoto wao.
 
Binafsi napenda kuishi sasa , kila ukiwaza kesho utajikuta kesho unawaza kesho kutwa na kuendelea na kushindwa kuishi sasa na maisha yako yote ukajikuta umeishi ukiwaza siku inayofuata bila kuishi siku uliyopo.
Ndio ishi leo maana ya kesho huyajui, principle ya maisha ni kuishi leo, sio jana wala kesho, namna unavyoishi leo ndio itaonyesha picha kesho itakuaje, ukiishi kesho itakushughulisha sana sana
 
ila kujiandaa uzeeni ni muhimu hii itawapa afadhari watoto wako na watu wengine wa karibu,kuwa mzee haina maana uje uwe tegemezi kwenye kila kitu watoto wako watakuwa na majukumu yao kulea familia zao,nakuwafanya watoto wao wafikie ndoto zao.

si utamaduni sana kwa familia zetu zakiafrika kusingatia hichi kitu ila ni wajibu wa mzazi kuhakikisha mtoto anakuwa salama toka siku umemzaa mpk siku unaaga dunia mtoto wako anatakiwa awe proud kuwa alikuwa na mzazi ambae hakuwa tu na fikra za kufikiri kila mtoto ni wajibu kumsaidia mzazi!,na kama wazee walikuwa masikini hivyo ni jukumu la watoto kuja kukutoa kwenye hilo dimbwi..
inatakiwa tupambane watoto waje wale raha,wakue vyema,waone maisha ktk namna tofauti nao wakawajibike kwa watoto wao.
mkuu huo uzee wenyewe una hakika wa kuufikia?
 
Back
Top Bottom