Umejiandaa vipi na maisha ya uzeeni (Retirement)?

Umejiandaa vipi na maisha ya uzeeni (Retirement)?

Hili ni tatizo kubwa, ukikutana na mzee anaishi maisha magumu lazima tu alikuwa anashughulika na chini ya wanawake enzi zake
Na alikuwa na mashamba mengi sana vile hakusomesha Watoto wake waliomba awagawie urithi kabla hata hajafa na alipowagawia tu wengi waliuza na yeye kubaki na shamba kidogo sana na akauza pia
 
Ndio ishi leo maana ya kesho huyajui, principle ya maisha ni kuishi leo, sio jana wala kesho, namna unavyoishi leo ndio itaonyesha picha kesho itakuaje, ukiishi kesho itakushughulisha sana sana
Hizo kesho, kesho kutwa ni illusion tu wala haina uhalisia na ipo kwenye fikra tu , na ni kitu tuliunda tu ili tupangilie mambo
 
ila kujiandaa uzeeni ni muhimu hii itawapa afadhari watoto wako na watu wengine wa karibu,kuwa mzee haina maana uje uwe tegemezi kwenye kila kitu watoto wako watakuwa na majukumu yao kulea familia zao,nakuwafanya watoto wao wafikie ndoto zao.

si utamaduni sana kwa familia zetu zakiafrika kusingatia hichi kitu ila ni wajibu wa mzazi kuhakikisha mtoto anakuwa salama toka siku umemzaa mpk siku unaaga dunia mtoto wako anatakiwa awe proud kuwa alikuwa na mzazi ambae hakuwa tu na fikra za kufikiri kila mtoto ni wajibu kumsaidia mzazi!,na kama wazee walikuwa masikini hivyo ni jukumu la watoto kuja kukutoa kwenye hilo dimbwi..
inatakiwa tupambane watoto waje wale raha,wakue vyema,waone maisha ktk namna tofauti nao wakawajibike kwa watoto wao.
Ndicho nacho kiwaza Kila Leo hiki.
Nifedheha kubwa sana kumaliza mwendo katika Hali ya umasikini wa kupindukia Ili Hali hapo awali uliishi vizuri.
 
Ni wazo zuri kuja na hoja fikirishi ya namna hiyo;

Uzee unatisha

Uzee unaambatana na upweke pamoja na changamoto za kipato pamoja na maradhi.

Ni vyema kujiandaa na Uzee ukiwa bado una nguvu

Binafsi najitahidi kulinda afya Kwa kuepuka tabia hatarishi ambazo Kwa namna Moja ama nyingine zinaweza kuhatarisha afya Kwa kuleta magonjwa ya Uzeeni.

Pili nimeanza kujiwekeza, Kwa kufanya miradi itakayokuwa inaniingizia hela hata wakati wa Uzee.

Nisingependa kuwa Mzee msumbufu Kwa watoto wangu.

Niko mbioni kujikatia bima ya maisha, japo ni ghali lakini nitakata kwaajili yangu na Mke wangu
 
Wapo ila ukiishi sasa vizuri hata sasa yako tena itakua nzuri . Sasa kila siku ukiishi ukiwaza kesho kesho ikifika ukawaza kesho kutwa na hivyo hivyo bila mwisho, lini utaishi sasa yako?
Tuombee uzima na afya tu jamaa yangu. Uzeeni ni kubaya sana. Hata hivyo Huwa hukai karibu na wazee kuchota mawili matatu ndo utakubaliana Nami
 
Ni wazo zuri kuja na hoja fikirishi ya namna hiyo;

Uzee unatisha

Uzee unaambatana na upweke pamoja na changamoto za kipato pamoja na maradhi.

Ni vyema kujiandaa na Uzee ukiwa bado una nguvu

Binafsi najitahidi kulinda afya Kwa kuepuka tabia hatarishi ambazo Kwa namna Moja ama nyingine zinaweza kuhatarisha afya Kwa kuleta magonjwa ya Uzeeni.

Pili nimeanza kujiwekeza, Kwa kufanya miradi itakayokuwa inaniingizia hela hata wakati wa Uzee.

Nisingependa kuwa Mzee msumbufu Kwa watoto wangu.

Niko mbioni kujikatia bima ya maisha, japo ni ghali lakini nitakata kwaajili yangu na Mke wangu
Wazo lako liwekewe lamination. Umenena vyema sana.
 
Pale kati ni chanzo cha migogoro ukipaendekeza na unajua kiafrika Afrika mwanaume anapambana kutafuta hela ili apate mwanamke mzuri au kumfanya mwanamke akae asiondoke mwisho wa siku ni kuangukia pua
Sahihi kabisa... ukitumia ubo"0 kuchagua mke lazima yakupate ya kukupata tu
 
Back
Top Bottom