Umejiandaaje pale Familia yako itakapokutenga?

Umejiandaaje pale Familia yako itakapokutenga?

Huu uzi umenifikirisha Sana, ninajitoa sana kwa watoto wa kaka yangu, mwenyewe hana uwezo wa kumudu mahitaji ya shule, ana watoto sita wawili kwa mama ambaye hakuwahi kuishi nae na wanne kwa mke anayeishi nae, hawa wawili alikuwa anaishi nao bi mkubwa. Hawa watoto wengi wao ni bright, mmoja f4 kapiga div.one ya Saba shule ya kata yupo special school form five pcb, mwingine div.one ya nane anasubiri selection, aliyezingua ni mmoja ana div. 3 na yeye anasubiri selection, mwingine yupo kidato cha Kwanza ila darasa la Saba alipata masomo yote daraja "a" sasa Hawa watanijari kweli Mimi baba yao mdogo, kama watoto wa kuwazaa wanakutelekeza??
 
"Me siwezi kuhangaika kutafuta ada ya mtoto wangu wakati huohuo nitafute na pesa za matibabu yako, uwezo huo sina"
Maneno hayo aliambiwa bibi yangu na mwanae wa kwanza wa kiume( me namuita anko). Bibi akajibu kiunyonge... sawa we endelea kutafuta ada ya mwanao.

Bibi tumemzika mwaka huu mwezi wa kwanza, r.i.p bibi najua uliumia sana.

Vijana tuishi kwa tahadhari sana, tusione sifa kusomesha watoto shule za mamilioni halafu tukajisahau kujitengenezea maisha yetu ya baadae. Watoto wa siku hz hawaaminiki hata kidogo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Daah aisee huyu Kijana atakuwa na mwisho mbaya sanaaa..
 
Hapa issue ni moja tu ,kuwa na pesa uzeeni ....watoto ndio watakuwa wanakupigia simu wanakuja kwako kukutembelea ....! Mimi mwenyewe nimeanza kukwepa simu za mzee maana kila muda ni kuhitaji pesa pesa pesa tu ....hata nikitaka kumpigia hata kama ninasalio huwa nafikilia sanaa....!


Kusema kweli uzeeni kama haitakuwa na vyanzo vyako vya pesa utaonekana kero ...
Nukuuu "hakuna kitu kinatisha duniani kama kuwa old and poor"... Vijana wa leo jiandaeni mapema ili mkizeeka muwe na fedha...
 
Taikon wa Fasihi, hoja yako ni ya msingi sana. Tatizo linakuja pale binadamu tunapojisahau kuhusu maisha yetu ya baadae. Zamani na hata sasa tunamsemo kuwa tunawasomesha watoto wetu kama investment, ila ni vema tukatofautisha investments hizi si zakutegemea tena, binadamu hawa wamebadilika sana siku hizi. Mungu atusaidie tusipate depression kwa mawazo katika uzee kwa changamoto hizi. Chamsingi ni kujiandaa financially na psychologically.
 
Huu uzi umenifikirisha Sana, ninajitoa sana kwa watoto wa kaka yangu, mwenyewe hana uwezo wa kumudu mahitaji ya shule, ana watoto sita wawili kwa mama ambaye hakuwahi kuishi nae na wanne kwa mke anayeishi nae, hawa wawili alikuwa anaishi nao bi mkubwa. Hawa watoto wengi wao ni bright, mmoja f4 kapiga div.one ya Saba shule ya kata yupo special school form five pcb, mwingine div.one ya nane anasubiri selection, aliyezingua ni mmoja ana div. 3 na yeye anasubiri selection, mwingine yupo kidato cha Kwanza ila darasa la Saba alipata masomo yote daraja "a" sasa Hawa watanijari kweli Mimi baba yao mdogo, kama watoto wa kuwazaa wanakutelekeza??

Fanya bila kutegemea malipo
Hakuna malipo hapo Mkuu. Huo ndio ukweli.

Ikiwa mtu anasomeshwa na wazazi wake na bado anawazingua sembuse Baba Mdogo sijui mjomba
 
Taikon wa Fasihi, hoja yako ni ya msingi sana. Tatizo linakuja pale binadamu tunapojisahau kuhusu maisha yetu ya baadae. Zamani na hata sasa tunamsemo kuwa tunawasomesha watoto wetu kama investment, ila ni vema tukatofautisha investments hizi si zakutegemea tena, binadamu hawa wamebadilika sana siku hizi. Mungu atusaidie tusipate depression kwa mawazo katika uzee kwa changamoto hizi. Chamsingi ni kujiandaa financially na psychologically.


Siku za mwisho upendo utapoa.

Embu fikiria, mwanamke uliyemtolea mahari, uliyemtunza, akazaa watoto, ukawatunza mpaka wakakua, afu Leo hii wote wanakubadilikia. Inasikitisha Ila hiyo ndio Hali halisi kwenye familia nyingi
 
Mimi mbona nimesha tengwa na mke na watoto kabeba, kilichobaki sijabembeleza tena arudi nimeamua kukomaa na maisha na kuifaidi pesa yangu sasa. Nataka niishi maisha mazuri ya kuifaidi hela yangu.
 
Taikon wa Fasihi, hoja yako ni ya msingi sana. Tatizo linakuja pale binadamu tunapojisahau kuhusu maisha yetu ya baadae. Zamani na hata sasa tunamsemo kuwa tunawasomesha watoto wetu kama investment, ila ni vema tukatofautisha investments hizi si zakutegemea tena, binadamu hawa wamebadilika sana siku hizi. Mungu atusaidie tusipate depression kwa mawazo katika uzee kwa changamoto hizi. Chamsingi ni kujiandaa financially na psychologically.

Unamaanisha nini unaposema unasomesha mtoto kama investment ?
 
USIMTEGEMEE MWANADAMU ( hii inaenda hadi kwa watoto na wazazi wako)
Mtegemee Mungu peke yake

Usisomeshe kwa lengo la kuja kusaidiwa baadae bali somesha kwa lengo ka hao Watu wajitegemee mbeleni!

Ukianza kuwaza kuwategemea unaowasaidia leo USHAFELI TAYARI!

Ujamaa Tanzania ulikufa zamani kwa Viongozi wetu na sasa unakufa kwa Grassroots!

Nchi ya Kibepari haina Misamiati eti Ndugu zangu!
Ni Mimi ni Mimi na Mungu wangu full stop!
Unapotoa unatoa kusaidia Siyo kwa lengo la Kusaidiwa Baadae!

Usijifunze kujitegemea Bali JITEGEMEE!
Unahitaji mambo mawili tuu kusurvive
1. Akili imara yenye akili
2. Uwezo wa Kuzisaka na kujiwekea hazina kiuchumi

Ukitaka akili Tafuta na Soma hivi vitabu
1 48 laws of power
2. 33 strategies of War

Ukiweza kujisimamia Utasimamia kwa akili na kilicho chako

I’m Out!
 
Back
Top Bottom