Asante sanaKaribu Sana Mkuu.
Daah aisee huyu Kijana atakuwa na mwisho mbaya sanaaa.."Me siwezi kuhangaika kutafuta ada ya mtoto wangu wakati huohuo nitafute na pesa za matibabu yako, uwezo huo sina"
Maneno hayo aliambiwa bibi yangu na mwanae wa kwanza wa kiume( me namuita anko). Bibi akajibu kiunyonge... sawa we endelea kutafuta ada ya mwanao.
Bibi tumemzika mwaka huu mwezi wa kwanza, r.i.p bibi najua uliumia sana.
Vijana tuishi kwa tahadhari sana, tusione sifa kusomesha watoto shule za mamilioni halafu tukajisahau kujitengenezea maisha yetu ya baadae. Watoto wa siku hz hawaaminiki hata kidogo
Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Nukuuu "hakuna kitu kinatisha duniani kama kuwa old and poor"... Vijana wa leo jiandaeni mapema ili mkizeeka muwe na fedha...Hapa issue ni moja tu ,kuwa na pesa uzeeni ....watoto ndio watakuwa wanakupigia simu wanakuja kwako kukutembelea ....! Mimi mwenyewe nimeanza kukwepa simu za mzee maana kila muda ni kuhitaji pesa pesa pesa tu ....hata nikitaka kumpigia hata kama ninasalio huwa nafikilia sanaa....!
Kusema kweli uzeeni kama haitakuwa na vyanzo vyako vya pesa utaonekana kero ...
Huu uzi umenifikirisha Sana, ninajitoa sana kwa watoto wa kaka yangu, mwenyewe hana uwezo wa kumudu mahitaji ya shule, ana watoto sita wawili kwa mama ambaye hakuwahi kuishi nae na wanne kwa mke anayeishi nae, hawa wawili alikuwa anaishi nao bi mkubwa. Hawa watoto wengi wao ni bright, mmoja f4 kapiga div.one ya Saba shule ya kata yupo special school form five pcb, mwingine div.one ya nane anasubiri selection, aliyezingua ni mmoja ana div. 3 na yeye anasubiri selection, mwingine yupo kidato cha Kwanza ila darasa la Saba alipata masomo yote daraja "a" sasa Hawa watanijari kweli Mimi baba yao mdogo, kama watoto wa kuwazaa wanakutelekeza??
Taikon wa Fasihi, hoja yako ni ya msingi sana. Tatizo linakuja pale binadamu tunapojisahau kuhusu maisha yetu ya baadae. Zamani na hata sasa tunamsemo kuwa tunawasomesha watoto wetu kama investment, ila ni vema tukatofautisha investments hizi si zakutegemea tena, binadamu hawa wamebadilika sana siku hizi. Mungu atusaidie tusipate depression kwa mawazo katika uzee kwa changamoto hizi. Chamsingi ni kujiandaa financially na psychologically.
Kuna tofauti kubwa kati ya hawa wawili mkuu, acha jamaa awe hivi na yule vile.Mkuu nitumie namba yako nikuunge kifurushi cha week.nakukabithi rasmi uwe mrithi wa mshana Jr.