Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Maeneo mengine duniani, kuanzia tarehe moja mwezi ujao wanakuwa wako mapumzikoni na wapenzi au wapendwa wao; kwa waliojipanga vizuri, wataenda hata nchi ya mbali akiwa na mwenzi wake au familia yake kuponda maisha kwenye mbuga za wanyama, milima, sehemu za utalii au vivutio mbalimbali n.k, kutokana na kile alichokikusanya mwaka mzima. Na baada ya sherehe ya mwaka mpya kuisha, urejea makwao, na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.
Huku kwetu imekuwa ni changamoto kidogo; iwe jua, giza, masika, kiangazi, asubuhi, jioni, usiku; bado mtu yuko bize na kutafuta maisha, hakuna kupumzika. Inafikia hatua ya kujiuliza, ni nini umuhimu wa maisha? Je tumekuja duniani ili tuteseke tu? Kwa mtazamo wangu, mi naona tumekuja duniani kutafuta na kuishi vizuri pia, kwa sababu hakuna sehemu nyingine ya kuishi zaidi ya hapa duniani. Kwa maoni yangu, naona turizike na tulichonacho; kutenga muda ili kupumzika na mwenzi wako au familia yako ni muhimu sana, hela huwa hazijai, tutakuwa nazo na tutaziacha.
Swali: Je, umejipangaje wewe na mpendwa wako katika hiki kipindi cha kufunga mwaka?