Umejipangaje wewe na mpendwa wako katika hiki kipindi cha kufunga mwaka?

Umejipangaje wewe na mpendwa wako katika hiki kipindi cha kufunga mwaka?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Maeneo mengine duniani, kuanzia tarehe moja mwezi ujao wanakuwa wako mapumzikoni na wapenzi au wapendwa wao; kwa waliojipanga vizuri, wataenda hata nchi ya mbali akiwa na mwenzi wake au familia yake kuponda maisha kwenye mbuga za wanyama, milima, sehemu za utalii au vivutio mbalimbali n.k, kutokana na kile alichokikusanya mwaka mzima. Na baada ya sherehe ya mwaka mpya kuisha, urejea makwao, na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.

Huku kwetu imekuwa ni changamoto kidogo; iwe jua, giza, masika, kiangazi, asubuhi, jioni, usiku; bado mtu yuko bize na kutafuta maisha, hakuna kupumzika. Inafikia hatua ya kujiuliza, ni nini umuhimu wa maisha? Je tumekuja duniani ili tuteseke tu? Kwa mtazamo wangu, mi naona tumekuja duniani kutafuta na kuishi vizuri pia, kwa sababu hakuna sehemu nyingine ya kuishi zaidi ya hapa duniani. Kwa maoni yangu, naona turizike na tulichonacho; kutenga muda ili kupumzika na mwenzi wako au familia yako ni muhimu sana, hela huwa hazijai, tutakuwa nazo na tutaziacha.

Swali: Je, umejipangaje wewe na mpendwa wako katika hiki kipindi cha kufunga mwaka?

AllInclusive-Main

 
Tumekodi apartment (it's basically a hotel) moja iko karibu na mto lengo likiwa ni kuvua samaki na kuwachoma jioni. Nimependa chumba, jiko na sebule. Chumba kina dirisha linalolingana na ukuta wake wote unaotazama mto.

Kuna michezo ya tennis, volleyball and golf pia. Wana bustani ya mboga na matunda pia. I love their landscaping and grassy knoll. I also love their fowls. Wamefuga ndege wengi sana. Shida ni ngedere tu. Usipokuwa makini wanaiba chakula usipofunga madirisha ya jikoni.
 
Tumekodi apartment (it's basically a hotel) moja iko karibu na mto lengo likiwa ni kuvua samaki na kuwachoma jioni. Nimependa chumba, jiko na sebule. Chumba kina dirisha linalolingana na ukuta wake wote unaotazama mto. Kuna michezo ya tennis, volleyball and golf pia. Wana bustani ya mboga na matunda pia. I love their landscaping and grassy knoll. I also love their fowls. Wamefuga ndege wengi sana. Shida ni ngedere tu. Usipokuwa makini wanaiba chakula usipofunga madirisha ya jikoni.
Nipo chumba cha jirani mkuuu,,,,
 
Tumekodi apartment (it's basically a hotel) moja iko karibu na mto lengo likiwa ni kuvua samaki na kuwachoma jioni. Nimependa chumba, jiko na sebule. Chumba kina dirisha linalolingana na ukuta wake wote unaotazama mto. Kuna michezo ya tennis, volleyball and golf pia. Wana bustani ya mboga na matunda pia. I love their landscaping and grassy knoll. I also love their fowls. Wamefuga ndege wengi sana. Shida ni ngedere tu. Usipokuwa makini wanaiba chakula usipofunga madirisha ya jikoni.
👏👏👏 safi sana wengi tunatamani iwe hivyo
 
Tunaenda Kilimanjaro Golf course , Ngorongoro
Serengeti

Tukitoka hapo tunaenda Daslam ni Asikwambie mtu tu tu Beer Beer tunabadili tu mara Maison mara CTFM
Itabidi utualike kwenye hiyo safari
 
Kwa kifupi mleta mada hayo uliyoongea mwafrika hayamuhusu

nimetoka kutafakari muda si mrefu,Jana nilikesha nikatoka asubuhi jamaa alipokuja kunitoa shift yangu ya usiku ,nikasepa home mida ya saa mbili asubuhi nikiwaacha makuli wanabeba mizigo.Nikarudi kazini kuelendelea na night shift yangu ilikuwa mida ya saa moja usiku nawakuta makuli walewale ndy wanamalizia kubeba mizigo kisha wagawane hela saa mbili usiku..nilikaa chini nikasema yaani hawa jamaa wameanza kubeba mizigo saa moja asubuhi,Mimi nikaenda kulala narudi usiku bado nawakuta wanabeba Tu alafu kwenye mgao unakuta mtu anapata elfu 20 dah!!

Maajabu hawa jamaa ukiwaambia kuanzia tarehe 24 Hadi Hadi tarehe 2 January hakuna kazi tunaenda Kula sikukuu wanapiga sn kelele kwmb wataishi vp kipindi chote hiko cha wiki moja!!

Yani mtu mweusi duniani anateseka na mbinguni akifika unakuta anahesabiwa makosa alafu unakuta anaenda motoni [emoji23]..kuna muda maisha unaweza Kusema hayana maana yoyote Kwa hii race yetu

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kifupi mleta mada hayo uliyoongea mwafrika hayamuhusu

nimetoka kutafakari muda si mrefu,Jana nilikesha nikatoka asubuhi jamaa alipokuja kunitoa shift yangu ya usiku ,nikasepa home mida ya saa mbili asubuhi nikiwaacha makuli wanabeba mizigo.Nikarudi kazini kuelendelea na night shift yangu ilikuwa mida ya saa moja usiku nawakuta makuli walewale
Kila kitu kinawezekana mkuu, inategemea na uongozi wa kampuni kama watatoa bonus kwa wafanyakazi si mbaya. Hili jambo linategemea na utashi wa boss husika, unavyompumzisha mtu unatakiwa pia umpatie namna ya kujikimu siku mbili tatu; na nina uhakika huyu mfanyakazi atakaporudi atakuwa na morali ya kufanya kazi vizuri zaidi. Tatizo tulilonalo sisi weusi pamoja na wahindi, mifumo yetu mingi ni ya kinyonyaji, tuko tayari mtu afanye kazi masaa 24/7 kwa ujira mdogo
 
Back
Top Bottom