Umekosa akili mpaka unakwenda kulala kwa mwanamke

Umekosa akili mpaka unakwenda kulala kwa mwanamke

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (60)✍️
Kama unahonga wewe honga lakini usidhani kwamba unapendwa sana kuliko wenzako. Usifikiri kuwa wewe uliyehonga Jiko la Gesi ni mjanja sana kuliko aliyehonga Kitanda. Au wewe uliyehonga simu ni mjanja sana kuliko anayehonga salio.

1. Kisa umemnunulia mwanamke Feni la Tshs 50,000 ndo unapata ujasiri wa kwenda kulala nyumbani kwake, tena unalala na boksa tu.
SWALI: Je, unamjua aliyenunua zile sofa?

2. Kisa umemnunulia mwanamke Gunia la mkaa la Tshs 70,000 ndo unapata ujasiri wa kwenda kulala nyumbani kwake usiku kucha.
SWALI: Je, unamjua aliyenunua lile Jiko kubwa la Gesi?

3. Kisa umemnunulia mwanamke TV ya Tshs 270,000 & King'amuzi cha Tshs 79,000 ndo unapata ujasiri wa kwenda kulala nyumbani kwake, tena umebeba na mswaki wako.
SWALI: Je, unamjua aliyenunua kile Kitanda cha milioni mbili?

4. Kisa umemnunulia mwanamke Kapeti (zulia) la Tshs 100,000 ndo unapata ujasiri wa kwenda kulala nyumbani kwake, tena umetundika taulo lako mlangoni.
SWALI: Je, unamjua aliyenunua lile Kabati la nguo?

✍️Mwanaume mjanja halali kwa mwanamke hata kama anamhonga vitu vya ndani. Lakini mwanaume mpumbavu ndiye anadhani yeye pekee anapendwa. Anakwenda kulala kwa mwanamke, mwishowe anafumaniwa ndani anakatwa mapanga.

Right Marker
Dar es salaam
 
100% Point.
Mwanaume usilale kwa Mwanamke, Wanawake Vitu vyao vingi ni vya kuongwa, sasa jiulize wewe unamchango Gani ktk hicho chumba, waza mbali atakapojua mwanaume mwingine ktk hicho chumba, unaeza kuta mko wanaume 10 mwanamke mmoja
 
Hii ishu tushakubaliana kua mwanaume(serengeti Boy) ana ruhusiwa kulala kwa mwanamke endapo mwanamke huyo ni Mshangazi
#Rejea kongamano la vijana lililofanyika Mwaka 2023
 
Hii ishu tushakubaliana kua mwanaume(serengeti Boy) ana ruhusiwa kulala kwa mwanamke endapo mwanamke huyo ni Mshangazi
#Rejea kongamano la vijana lililofanyika Mwaka 2023
Hakuepo kwenye kilele cha Kongamano la vijana ila Cha kumshauri 2024 asikose mzungumzaji mkuu atakua Baltasar Ebang
 
100% Point.
Mwanaume usilale kwa Mwanamke, Wanawake Vitu vyao vingi ni vya kuongwa, sasa jiulize wewe unamchango Gani ktk hicho chumba, waza mbali atakapojua mwanaume mwingine ktk hicho chumba, unaeza kuta mko wanaume 10 mwanamke mmoja
Kabisa...haman mwanamke mwenye mwanaume mmoja
 
IMG-20241108-WA0160.jpg
 
Sema hao uliokua nao na sio kwamba hakuna mwanamke mwenye mwanaume mmoja na sio kila mwanamke anahongwa vtu vya ndan wwng n jitihada za maisha tu
Wewe bwana wewe bwana mwanamke mwenye mume mmoja ni bikira maria tuu. Hawa wengine wote duniani unaowaona including mama yako na mama yangu wote Wana wanaume zaidi ya mmoja . Sasa kama wewe unataka bliv otherwise do so at ur own peril
 
Sema hao uliokua nao na sio kwamba hakuna mwanamke mwenye mwanaume mmoja na sio kila mwanamke anahongwa vtu vya ndan wwng n jitihada za maisha tu
Hakuna mwanamke anaye ishi kigeto mwenye mwanaume mmoja acha kujidanganya.
%99.99999999 ya wanawake walio panga geto wanategemea nyapu zao kuishi mjini.
 
Wewe bwana wewe bwana mwanamke mwenye mume mmoja ni bikira maria tuu. Hawa wengine wote duniani unaowaona including mama yako na mama yangu wote Wana wanaume zaidi ya mmoja . Sasa kama wewe unataka bliv otherwise do so at ur own peril
Oya maza angu ni mzee age go hana mwanaume tafadhali bana 💪
 
Huu ni ukwel mtupu japo kina mario watakuja kupinga!!na mbaya wanaume tukifumaniana huwa ngumu kuelewana zaid ya ngumi kwanza na wengne kupakana mafuta!!bora ulale kichakani kuliko kulala kwa mwanamke
 
Back
Top Bottom