Umekosea Prof. Adolf Mkenda: Utendaji mzuri popote sio haki

Mbona logic ya NECTA iko wazi mosi kwamba kutangaza hivyo ni sawa na kutangaza biashara za watu. Kwa sasa mfumo wa utoaji elimu hasa kwa shule binafsi umekuwa ni kibiashara zaidi kuliko kutoa elimu.

Shule zimejikita kufundisha kufaulu mitihani na sio kufundisha maarifa. Watoto kuanzia form one wanasoma kwa mfumo wa maswali na majibu tu. Hata vitabu vingi kwa sasa katika mfumo wa maswali na majibu.
Siku hizi ubora wa shule hupishwa kwa kufaulisha na sio kwa kutoa maarifa bora.

Hali kadhalika kutangaza kwa shule bora wakati mwingine kumekuwa ni kichocheo cha udanganyifu katika mitihani ili shule iweze kuwa na matokeo bora.

Pili, kutangaza matokeo haina tija kwa sababu shule zingine zina wanafunzi wachache zingine zina wanafunzi wengi sana. Unakuta Shule moja binafsi hasa seminary zinawafunzi 20 au 30 wakati shule za kata wanafunzi zaidi ya 200 kwa darasa moja.

Hali kadhalika shule za binafsi huweka masharti ya wastani wa juu ili mwanafunzi aweze kuvuka darasa vinginevyo mtoto atarudia darasa au mzazi umhamishe. Nakumbuka kuna Shule moja wastani wao walikuwa wameweka ni 65 ili mtoto aweze kuvuka darasa.

Kwa serikali huwezi kuweka wastani hata wa 40 vinginevyo zaidi ya nusu ya darasa watakariri darasa.

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
 
Wewe uko hapo Buza kwa Mpalange unasumbua tu watu bure na kelele za Texas.
Mnaongea vitu ambavyo hamfahamu. Mimi niko hapa ni shule zote kuanzia miaka 7 mpaka 18 Grade 2 mpaka 12 kuna mitihani. Kuna mpaka mitihani ya kuingia vyuo
 
Be easy bro this is Africa
 
Kuna ubaya gani kutangaza biashara ya elimu bora na nzuri kwa watoto wetu. Yaani matangazo sasa kwa vijana wetu hawa yatabaki kubeti na ujinga wa hizi kiki za wasanii bila ku balance na umuhimu wa elimu.

Tumefika sehemu kutangaza shule inafanya vizuri ni kitu kibaya🤔 lini tutaacha fikra za kimasikini
 
Tunahitaji matangazo ya shule kwa ufaulu sio shule bora!.

Ubora wa shule ndiyo unaongelea lakini bado ufaulu uwe palepale bila siasa, biashara wala nini matokeo tu. Ni sawa na kusema timu ya Tabora ya mpira iwe ya kwanza kwasababu iweza kucheza ligi bila pesa lakini simba na yanga ziwe za mwisho kwasababu wanapesa nyingi! Haina maana.

Kufaulu pekee sio ubora lakini kama ni ya kwanza basi ni ya kwanza
 

Prof. Mkenda ni waziri mwenye IQ kubwa sana, pengine ndio waziri sahihi zaidi kuwahi kutokea kwenye hii Wizara.

Huyu kumbe ndio maana alishindwa kabisa kuiva chungu kimoja na Kigwangala.
Kweli kabisa. Hata mimi niliambiwa na bibi yake kuwa huyo mjukuu wake (waziri waelimu) ana IQ kupita ya Einstein
 
Hapa moto kama huwezi hoja nenda section ya kiki!
Oky tupe hoja mdogo wangu tuwafikishie wahusika (Viongozi wetu wa chama na serikali) Dodoma!!!!Uzuri wa serikali inapokea maoni yotee kutoka vyanzo mbalimbali na kuyafanyia kazi
 
Oky tupe hoja mdogo wangu tuwafikishie wahusika (Viongozi wetu wa chama na serikali) Dodoma!!!!Uzuri wa serikali inapokea maoni yotee kutoka vyanzo mbalimbali na kuyafanyia kazi
Najua na bahati nzuri ukifuatilia hoja zangu nyingi zinafanyiwa kazi sana na serikali

1. Ushauri kwa Raisi kukutana na Chadema na kufungua mikutano
2. Ushauri wa Raisi kumtoa zittto
3. Ushauri kwenye kilimo

…… records zangu zipo hapa toka 2006. Hapa NIDA nilitoa mawazo kabla haijaanza, mikopo ya bank , afya, kodi, kazi.

Topic zangu zote ni Mawazo tupu
 
Usiwe na wasiwasi mdogo wangu serikali ni watu na watu ndio sisi!!!Sio hoja zako tu bali hoja za watu wote wa JF na platform nyingine zinafanyiwa kazi!!!!!
 
Hayo ni maoni yako mimi siyakubali naona yana ujima wa kufikirika sana
 
Ngoja nikushauri kitu mdogo wangu Kamundu kama kaka!!!Pale mwanzo nilikuambia be easy this is africa!!!Maana yake don't think ur very special than other's here in JF punguza ego na majigambo!!!!!Tunashukuru sana kwa mawazo yako na serikali sikivu ya awamu ya sita itayachukua na kuyafanyia kazi
 
bro, msikilize tena Kwa uzuri. Maelezo ya prof yamenyooka mno,
 
Mbona waziri kaongea point nzito... Take trouble to listen to him
 
Naunga mkono hoja
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…