Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 1,973
- 2,239
Hakuna jamii yeyote Duniani ambayo kuna usawa kwenye kila kitu. Hata hapa Marekani watoto wa George H Bush wamekuwa maarufu na kuwa Governors na mmoja Raisi kwasababu babu yao alikuwa tajiri, baba akawa tajiri akaweza kuwasomesha shule nzuri sana na kuwapa elimu bora. Hii haina maana kwamba hawa watoto ambao wamekuja kuwa Maraisi wanavipaji kuliko wengine lakini wameweza kupata fursa ambazo ni ngumu kupata mtoto wa masikini. Hii hipo sehemu nyingi sana. Yule mtoto wa Kikwete ingewezekana asiwe lawyer kama angezaliwa mtwara vijijini kwa familia masikini lakini haibadilishi ukweli kwamba mtoto wa kikwete kamaliza chuo kikuu cha Dar law school. Na kwakutumia hili huwezi kusema mtoto wa kikwete ambaye kamsomesha ni sawa tu na yule ambaye hajapata elimu kijijini kwasababu wana vipaji vya kuzaliwa sawa!
Kwa namna hii huwezi kuacha kutangaza shule na matokeo kwasababu tu wanafunzi wengi wa shule hizo na walimu wanapitia magumu sana kulinganisha na wengine.
Mimi mfano nilisoma Ilboru O-level wakati tulivyokuwa Ilboru watoto wa kutoka Arusha School walikuwa wanatuzidi mwanzoni kwasababu ya mazingira yao lakini sisi tuliongeza jitihada na kulingana na hata kuwapita. Huwezi kutumia kisingizio hiki kuacha kutangaza ukweli. Sasa ina maana tutaanza kupeleka watoto kusoma Udaktari ambao hawajafaulu? au kuendesha ndege ambao hawajafaulu kwasababu kama hizi?
Mbona logic ya NECTA iko wazi mosi kwamba kutangaza hivyo ni sawa na kutangaza biashara za watu. Kwa sasa mfumo wa utoaji elimu hasa kwa shule binafsi umekuwa ni kibiashara zaidi kuliko kutoa elimu.
Shule zimejikita kufundisha kufaulu mitihani na sio kufundisha maarifa. Watoto kuanzia form one wanasoma kwa mfumo wa maswali na majibu tu. Hata vitabu vingi kwa sasa katika mfumo wa maswali na majibu.
Siku hizi ubora wa shule hupishwa kwa kufaulisha na sio kwa kutoa maarifa bora.
Hali kadhalika kutangaza kwa shule bora wakati mwingine kumekuwa ni kichocheo cha udanganyifu katika mitihani ili shule iweze kuwa na matokeo bora.
Pili, kutangaza matokeo haina tija kwa sababu shule zingine zina wanafunzi wachache zingine zina wanafunzi wengi sana. Unakuta Shule moja binafsi hasa seminary zinawafunzi 20 au 30 wakati shule za kata wanafunzi zaidi ya 200 kwa darasa moja.
Hali kadhalika shule za binafsi huweka masharti ya wastani wa juu ili mwanafunzi aweze kuvuka darasa vinginevyo mtoto atarudia darasa au mzazi umhamishe. Nakumbuka kuna Shule moja wastani wao walikuwa wameweka ni 65 ili mtoto aweze kuvuka darasa.
Kwa serikali huwezi kuweka wastani hata wa 40 vinginevyo zaidi ya nusu ya darasa watakariri darasa.
Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app