Umekula tunda gani leo?

Umekula tunda gani leo?

Screenshot_20220223-093311.jpg
 
Black Diamond Apples from Tibet

The black Diamond apple is a rare breed from the family of Huaniu apples that is cultivated in the Tibetan region of Nyingchi. Despite what the names suggests the apple rather is a purple hue, with white pulp on the inside. Its unique color is due to the region's high altitude of over 3,500 m.
Screenshot_20220305-043711.jpg
 
PEASI

ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binadamu.
Tunda hilo ambalo kwa umbo linafanana na tufaa (apple), lina faida nyingi kwa binadamu iwapo atalitumia mara kwa mara.

Tunda hili limekuwa adimu kutokana na kutostawi katika maeneo mengi hivyo watu wengi hawalifahamu na hata walionapo hawalitilii maanani kama ilivyo kwa matunda mengine kama vile ndizi, embe, papai na mengine.

Tunda hili lina faida mbalimbali katika mwili wa binadamu kama vile kukausha jasho la kwapa kwa wale wenye kutokwa na jasho jingi endapo litaliwa mara kwa mara.

Pia tunda hilo ambalo hulimwa sana katika Mkoa wa Tanga husaidia kupunguza mwasho wa koo na juisi yake ni nzuri skwa kuua mba, hutibu kibofu cha mkojo na uti wa mgongo.

Vilevile tunda hili lina Vitamin A na B ambazo husaidia kuepukana na upofu, pia husaidia kuongeza hamu ya kula na kuboresha mfumo wa fahamu.
Wakati mwingine tunda la peasi husafisha mishipa ya moyo na kutibu mafua ya ndege na husaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri.

Tunda la Peasi husaidia kuongeza kinga za mwili, kuupa mwili nguvu, hupunguza shinikizo la damu, kuzuia mafuta kuganda mwilini (cholestrol), huzuia magonjwa ya saratani, kiungulia pamoja kupunguza homa.

Pia tunda hili likitumika baada ya chakula cha usiku au baada ya kupata kifungua kinywa huweza kuleta matokeo mazuri.

Jarbu kushare na wenzako wapate kujifunza mengi[emoji120]

View attachment 2117282
Najitahdi kuyala maana huku yametapakaa kila nyumba lakini mimi yanafanya meno yangu kufa ganzi
 
Kwa hakika kama kuna mtu kati yetu asubuhi ya leo kala tunda lolote lile basi ni wale waliolala zile hotel zenye bed n breakfast full course. Wengine wetu kwa uchache mno ni wale wafanya diet na kwa uchache zaidi wale wanaotambua umuhimu wa matunda mwilini kiafya. Wengi wetu humaliza mpaka wiki bila kula hata kipande kimoja cha tunda lolote.

Wengi huwa hawali matunda mpaka waandikiwe na daktari kama sehemu ya tiba. Kwao kula tunda ni sehemu ya anasa na kupoteza pesa..

Matunda yana faida kubwa mwilini kiafya kuliko hata nyama. Matunda ni sehemu muhimu ya tiba. Matunda yana uwezo wa kukujenga kiafya na kukukinga na maradhi mengi. Ni afadhali mara mia ukala matunda ya buku kuliko kula mchemsho wa buku 2, Matunda ni tiba ya magonjwa mbalimbali.

Matunda ni sehemu muhimu ya tiba mbadala na ujenzi wa mwili imara na wenye nguvu.
Baadhi yetu hupendelea shurubati zaidi kuliko matunda yenyewe. Ni sawa pia lakini shurubati isiyo halisi inakuwa imechanganywa na vionjo vingine hivyo kupunguza kwa kiasi fulani nguvu ya kutenda.

Huu ni ushauri wangu kwako pamoja na kunywa maji mengi na kupangilia milo yako lakini usisahau kitu hiki muhimu sana TUNDA. Jitahidi kupata kipande cha tunda kwenye kila mlo wako.. kuna siku utanikumbuka na kunishukuru kimoyomoyo
Je, umekula tunda gani leo?

Nimekula "Tunda Special" la Muumin Mwijuma.
 
Viranja embu unganisheni huu uzi na ule wa rikiboy maana unatuchanganya ikishafika jioni 😀😀😀
 
Blue Banana are real.
The blue Java is a hardy, cold tolerant banana cultivar known for its sweet aromatic friut, which is said to have an ice cream-like consistency and flavor reminiscent of vanilla. It is native to Southeast Asia and is a hybrid of two species of banana native to Southeast Asia -- Musa balbisiana and Musa acuminata.
FB_IMG_1647231954957.jpg
 
Back
Top Bottom